Leo nimeletewa malalamiko na dada mmoja anayeishi nyumba moja ya kupanga na yanamhusu mama mmoja ambaye ni mpangaji mwenzie huyu dada akiwa na shida lets say mkaa,chumvi,sukari akienda kumwazima mpangaji mwenzie(huyo mama )anampimia.
Mfano; akiazima mkaa anampimia kwenye mfuko wa sh hamsini au sukari anampimia kwenye kikombe then anamwambia huyo dada akisha nunua amrudishie kwa kipimo kilekile chakushangaza akirudisha anapokea anaweka ndani lakini huyu mama akizima hatakiberiti harudishi hata, akipimiwa mkaa harudishi cha ajabu zaidi hanunui mkaa anaishia anaazima mpaka gunia linaisha na yeye akija kununua mkaa harudishi.
Kunabaadhi ya siku akimuona huyo dada hayupo jikoni anaingia na kujichukulia chochote na kuondoka sasa imefikia point huyo dada amemchoka na hajui afanyaje coz huyo mama hata ndugu zake wakija kuomba mkaa anawapimia na kuwaambia warudie wa kisha nunua sasa huyu dada anaomba ushauri aishije na huyu mama ili wawe na mahusiano mazuri.
Kiberiti,!! Sukari vijiko kadhaa!!! Vipande vya mkaa!! Chumvi!!
Hilo balaa....baadhi ya mazingira ukishayatengeneza ni shida tupu. Mazoea ya kipuuzi tu.ila kwa kuwa wote wana uhitaji unataka ushauri wa nini sasa? Huyo mama anaomba, huyo dada pia anaomba! So acha waendelee kuombana na kusaidiana!
Hayo ndio maisha ya nyumba nyingi za kupanga mjini. Wengine wanatumia njia hizo katika kubana matumizi, dada asipokuwa makini atabeba gharama za maisha za mpangaji mwenzie. Dawa ni kuwa makini tu na matumizi yake na ikibidi amweleze mama ukweli ili waende sawa.
Amchane live tuu.huyo mama ka ana akili za kutosha atajishtukia.ila ndo kavile vinaingilia sikio la kushoto na kutokea la kulia basi kazi ipo.ajitoe tuu faham kufungia vitu vyake coz atabaki kunung'unika buree tuu mwisho akonde.
kumbuka wanaishi nyumba mmoja raque so kumpa za uso anaona kama huyo mama atachukia kwa kifupi anataka apate wazo ambalo akilifanya huyo mama hatakasirika lakini ataaelewa
Cha kwanza ajitahidi ahakikishe vitu vinakuwa ndani muda wote, ajitahidi ktk hili ili asiwe anakwenda kuomba omba tena, muache huyo mama aombe, ila akizidi amnyime na kumpiga marufuku, hasa hiyo tabia ya kuingia ndani na kujichukulia tu vitu hovyo
Mimi Namshauri Ampe Tu Bila Kutarajia Kurudishiwa Kama Hawezi Kufanya Ukarimu Huo Huyo Dada Akija Kumuomba Asimpe!Ili Asiendelee Kupata Dhambi Za Kusengenya, Duniani Kusaidiana Malipo Kwamungu!