Mwanamke Kutotongozwa…. JAMANI Tatizo nini?

hahaha.... Si nilikwambia kua huyo Fatma alikua anataka? Alafu shem si kuna ile ambayo wanaume huangalia kama atapata hapo anapo papenda ama lah! Akiona kua chances are slim wala hata haangaiki kabisa! lol
Ewaaaa!

Hakuna kitu mwanaume anachoogopa kama kupigwa kibuti. Ndo maana huwa haingizi neno kama mtongozwaji mwenyewe anaonekana katia pamba sikioni....

Mwanaume anayeingia kichwa kichwa afu akalimwa kibuti basi huyo SI MWANAUME BANA!
 
Kid sis mimi naamini saana the way wajipotray ndio hasa the way wachukuliwa.... Take note kama wewe watongozwa kila siku ya Mungu then kuna tatizo ambalo laweza kua ni wewe mwenyewe (maybe uvaaji), mazingira uliopo na mazoea yako dhidi ya walo kuzunguka. Naamini kua mwanamke ukijiheshimu na waonekana wajiheshim wale walo kuzunguka ikitokea kuna anae taka kukutongoza lazima ajipange kwanza.... na kama wanaokutongoza wajipanga kwanza haiwezekani kua utatongozwa ile mara kwa mara.... For watakuepo wale watakutamani but wataridhia kula kwa macho....

Umenipata dear?
Nimekuelewa Big SISY,na ni kweli huwa wanajipanga hakurupuki kwa kuogopa vya mbavu,

Ila hawa wanaume bana hata hawaeleweki unakuta hata umeongozana na mdada kavaa ile km kamkusudia mtu,
Cha kushangaza ww ambae umejivalia zako kawaida ndio unapata usumbufu yule mwezio wakishachekean pale mkapita ndio basi lkn ww mwingine ndio lijamaa linaenda kujikoki mistari anakuibukia upya!!!!

Labda hapa tuseme kuna aina za tongozo,means kuna zile za serious na zile za kupigiana makele bara baran kutokana na uvaaji wa mtu,mie hizo za makelele bara baran sikutan nazo kwa namna ya uvaaji wangu,

Mie hapa naiongelea ile ya serious ambayo haihusiani labda na kumtega mtu kimavaz,isitoshe unajikuta unatokewa hata na watu wanaokufahamu ww umeolewa au uko kwenye relation!!!
 
Ni matatizo tu ya hapa na pale ya kidunia babu lakini namshukuru Mungu niko salama............oooppsss sorry ADI kwa kuwa off topik......babu huyo
Orayt.... pole kwa matatizo. Ila hayahusiani na mitongozo wala mafumanizi, right?

Sori ADI fo zis ofutopiki, (Source: Kbd)
 
Kuna rafiki yangu amewahi kuniambia mapenzi ni sanaa (art) kama sanaa nyingine ingawa hii hufanywa na watu wengi zaidi. Sasa kwa hawa wasotongozwa/ -tongozeka AD my sis it is their very own duty to learn the theories na kuchagua paradigm ya kufanyia kazi and be cautious upon entering the volatile practical ground

Mapenzi ya kweli sio art.... Siamini hili Ole..... Ila tu nakubalisana na hio ya kwamba they should learn the theories....lol... Kazi kweli kweli! lol

Hivi kwani lazima kutongozwa bana? Mzukie mwenyewe tu, khaa mbona mbwembwe nyingi sana!!

Kipipi sijasema ni lazima.... Na kuna raha bana mwanamke uzukiwe sio umzukie.... hawa kaka zetu hawachelewi kusema kwanza ulinitongoza mwenyewe! lol

AD,
Kumbe msipotongozwa nalo ni tatizo hata kama mnajua jibu litakuwa yes or no depending on many different issues?

lol.... Ndahani bana.... Ndio usitongozwe kabisa?? Ilo kwa kweli ni tatizo. Labda kama tayari you have your own....
 
Duhhhh
Mi nimesikia na nimeona wasichana/wanawake wanatongozwa hadi usumbufu.
Sijawahi sikia mwanamke ambae hajawahi tongozwa kabisa ...

Bi mkubwa,

Habari yako binafsi kwanza....

Huyo mwanamke ambaye hatongozwi huyo tena ni kiboko ua labda hajui matumizi ya mtandao.....

Maana siku hizi unatongozwa na mtu hata hamjuani matongozo meeengi mpaka uanshangaa huyu mtu ananijuaje mimi kama ni jini je???

JF unatongozwa, FB unatongozwa, Twita unatongozwa nk basi ni vurugu tupu

Nyie warembo msijione kua mna bahati (or call it whatever) ya kutongozwa na ukadhani wanawake wote hutongozwa hivo hivo.... Wengine wanakosa wa kuwatongoza......lol

@Dena....

Wifi hivi unafikiri ni wangapi wanatumia JF, FB na twitter katika jamii yetu? Ni wachache mno.... kutongozwa kwenye mtandao ni rahisi saana (thou haijawahi nitokea :wink2:); Lakini wapo wale katika jamii hapati watu wa kumtongoza.
 
Lol. . mapenzi na mahusiano dah! mapenzi yanarun dunia! sababu nyingi zinasababishwa na infriority complex ya kaka zetu! mwanamke ajifanyishe wa chini ili atongozwe? yani ingekuwa kwa mila zetu mwanamke unaweza ukaanza ingekuwa bora sana jamani!

Twande
Hapo kwenye bold hapo ni kwamba kila mtu anataka a user friend now adays si suala la kujifanyisha wa chini NO....ni hoja ya kujiweka katika a common ground level !!!!! Ukijibagua na wengi expect kubaguliwa na wengi in return, kuna ka usemi "wa matawi ya juu" haka kanawalevya wengi wake kwa waume kama dada wa matawi ya juu ni sawa na yuko busy na safari ok....ila hakuna a common grounder anayependa co-pilot...so you enjoy flights wakati wenzako wana enjoy togetherness and vice versa.....so umsubiri wa matawi ya juu mwenzako naye if it happens akiwa free ndo akupe 1 hour treat then akaendelee na mitkas yake.........coz kwa mwanaume (akishakuwa wa matawi) likely anakuwa na familia tayari.....so why the hell wasting resources for non-sense and danger??????

Unajua plug and play????? Simaanishi kuwa simplistic ila lazima ujue kucheza na biti no matter who you are othewise waweza DODA mchana kweupe ukilaumu inferior complex za wanaume kumbe watu siku hizi hawana time ya kupoteza

Hata nyimbo siku hizi zimebadilika
Zamani; Africa unite, Prison, No woman no cry, Liberia nakadhalika za kusaka uhuru
Siku hizi; Wine Gal, Hold my hand, My love is wicked, 03bone n clyde, my boo etc etc

Unakuta demu kang'ang'ana ooonh m beautiful.....atanipa nini yule.....kazi yake haitoshi hata mafuta kwa mwezi......mwanaume gani hatumii hata IseyMiyake (akimaanisha designer notes)....yaani bora plasticity tuuuuu

Plain fact ni kwamba any responsible dude with focus n plan anakuwa engaged sana na mambo ya maisha kuliko hizo chase with NO rewards....mtu hajibu salamu....anaingia kwenye lift hasalimii.....huyu ndo umfikirie kuwa partner......ukiumwa atalala hospitali huyu kukuona uki-puke akusaidie??????

Jamani ukweli ni kwamba the way you present yourself before people has a lot to tell, do and even label you!!!!!!
You btter lie low so that you get embraced (itakayopelekea kutongozwa) by all characters ili uew na mawanda mapana ya kuchagua kilicho bora kwako

KALAGA BAHO wazaramu wanasema
 
wengine nasikia huwa wanaoga mtoni saa kumi usiku maji ya bariiiiiidi kama barafu ile watongozwe
Fidel80 nadhani anajua vizuri

Condoreza una vituko wewe!! lol.... Dah! hii dawa kiboko na itabidi Fidel aieleze zaidi aisee....lol

Lol. . mapenzi na mahusiano dah! mapenzi yanarun dunia! sababu nyingi zinasababishwa na infriority complex ya kaka zetu! mwanamke ajifanyishe wa chini ili atongozwe? yani ingekuwa kwa mila zetu mwanamke unaweza ukaanza ingekuwa bora sana jamani!

hahaha.... Twande mila zina evolve ujue... Waweza jitoa muhanga na kuevolve hio mila..... lol... Ingawa in the long run lazma ikusumbue.....

Hii sredi bado inaendelea au tuianze uchakachuzi?

Sori ADI for zis schupid ofutopiki lakini inayodizevu ka-LIKE kamoja.

:iamwithstupid::iamwithstupid:

ODM mbona uchakachuzi niliona kama umeanza kitambo? lol... Have a kick off it! lol

Habari zako mamii?

Daaah hata sina la kusema, ila ukweli kuna matongozo mengine mpaka mwenyewe unasema hiki nini! Kunalijamaa limoja lilinitongoza kwa sms akidai alinishindwa kuniface yaani niliona aliniudhi sana na alinifanya nijiulize mara 10 10 kwa nini mimi? Niliona kama amenidharau sana.

Lakini mwisho wa siku............"Never get Angry. Never make a Threat. Reason with people"

Mie mzima na nimefurahi kukuona.... ila tu umenifurahisha ume manipulate hadi kuweza chakachua sig yangu iweze kubali maelezo.... hahahaha.....

Illa kuna mtu akikutongoza lazima urudi kijijini kufanyiwa sadaka ya kutoa nusks.... lol
 
  • Thanks
Reactions: Kbd
Asante AD for this post. Mie langu moja tu, hivi, kutongozwa ni kitu cha kidini au? Yaani , kinakubalika kidini ?==> na hence muongozo kuwa ni lazima itoke kwa wanaume tu?
Au ni a generic term ambayo inaweza kutoka hata kwa wanawake?

Hofu yangu kubwa ni kuwa , kama ni jambo linalotakiwa kutoka upande mmoja, tiyari lina set precedence na mazingira yanayompa superiority m-gender mmoja dhidi ya mwingine.

Na hasa tukizingatia kuwa wanaume wana list yao ya 'wanavyovipenda' au kuvitamani kwa jenda hii ingine na hali kadhalika, wanawake huwa wana yao, na bado kuna vigezo-changia-kote i.e vinavyokubalika na ku feature katika list zote mbili.
Mfano, mwanaume atavutwa na umbile na sura ( asilimia kubwa, sijasema wote, kabla hamjanitovoga na bisbisi machoni), atapenda labda mwenye haya kidogo , though wengine wanapenda macho makavu, wengine wanapenda mwanamke independent ila eti awe submissive ( hapo inakuwaga ngumu kubalansisha ikwesheni ila ndo hivyo)etc.
Wanawake nao hupenda ( walio wengi) security in a man - mara nyingi hili hupimwa na juhudi ya kazi , mara nyingine pesa , na historia ya mafanikio maana hiyo pia itamu assure maisha bora ( sio wote jamani); uaminifu ( kigezo kigumu kabisa), un-mkatili ( sijui ndio mpole, au sijui nini but antonym ya mkatili- hapa nakumbuka lile tangazo la kwenye luninga la mwanaume ambaye akiingia home, hadi watoto wanajificha katika makapu) .

Lakini pia kuna vile vigezo changia kote kama uaminifu na ukweli ambavyo havina jinsia.
Na hapa natoa heshima ( pay respect, lol) to ukweli kuwa sio tongoza zote zitaishia katika ndoa. Najua zingine ni patapotea lakini sijataka kuketi ( ku base) katika utongozaji wa kihuni tu wa tamaa ( one night stands), ila zaidi katika ule utaoleta mahusiano thabiti.
Naomba kuwasilisha
 
Mwanaume kumtongoza mke wa mtu sababu ni nyingi saana na hilo ambalo umesema ni moja wapo. But I do know for a FACT kua mwanaume anaweza penda mke wa mtu na asimtongoze tokana na heshima alo nayo juu yake. For mtu kua mke wa mtu haimaanishi kua wanaume wengine hawawezi muona na ku appreciate her beauty. Hata hivo kuna mwingine akimpenda mke wa mtu anaweza akamtongoza na akamaanisha na sio sababu ya dharau, thou in one in 50. Na pia mke wa mtu hutongozwa tokana na yeye the way alivo ji potray.... Take note: wanaume wengi ambao hutongoza mke wa mtu hufanya hivo kwa kujaribu na si kumaanisha hasa, ila ikitokea kakubali then ratiba itafuata kama kawaida.....

Kwa mwanamke kutongozwa hakukwepeki hata ukijipiga kininja, atakuja ustadhi na kibaragashia atakutongoza, ukijivika sura ya kilokole, pia ataibuka mjuaji ajifanye anakufundisha neno mwisho wa siku anamwaga sera.

Kuna watu wao kazi ni kudeal na wake za watu, na wana kimsemo eti mke wa mtu hana gharama.
Kwa wanawake kutongozwa ni jambo la kawaida (sunnah) kama mnavyosema, tatizo ni kukubali kila unapotongozwa mmh hapo ndio noma kumkubalia kila mwanamme anaekutongoza.

Kingine kwa mwanamke ni type ya huyo mtongozaji kama anaendana na ww, kama utaona wanakutongoza hamuendani type hapo pia kuna question mark......!

tatizo leo j3 mikazi kibao hata kujiachia katika huu uzi inakuwa tabu.
 
Ni vizuri ukatumia lugha moja tu,(kiswahili au kingereza). kwa kuchanganya hivi wana jamii wanakuona kama Mshamba. Na huyo mwanamke mzuri asietongozwa ana mkosi unaoitwa KIMAVI.
 
Ewaaaa!

Hakuna kitu mwanaume anachoogopa kama kupigwa kibuti. Ndo maana huwa haingizi neno kama mtongozwaji mwenyewe anaonekana katia pamba sikioni....

Mwanaume anayeingia kichwa kichwa afu akalimwa kibuti basi huyo SI MWANAUME BANA!

Shem hapo in blue sio yategemea kweli? mbona your hommie enzi hizo alinitongoza mara 3 nikawa nampa za uso lakini hakukata tamaa mara ya 4 nikaingia line.... :redface: Na I know you know as I know kua ni Mwanaume hasa! lol
 
Nimekuelewa Big SISY,na ni kweli huwa wanajipanga hakurupuki kwa kuogopa vya mbavu,

Ila hawa wanaume bana hata hawaeleweki unakuta hata umeongozana na mdada kavaa ile km kamkusudia mtu,
Cha kushangaza ww ambae umejivalia zako kawaida ndio unapata usumbufu yule mwezio wakishachekean pale mkapita ndio basi lkn ww mwingine ndio lijamaa linaenda kujikoki mistari anakuibukia upya!!!!

Labda hapa tuseme kuna aina za tongozo,means kuna zile za serious na zile za kupigiana makele bara baran kutokana na uvaaji wa mtu,mie hizo za makelele bara baran sikutan nazo kwa namna ya uvaaji wangu,

Mie hapa naiongelea ile ya serious ambayo haihusiani labda na kumtega mtu kimavaz,isitoshe unajikuta unatokewa hata na watu wanaokufahamu ww umeolewa au uko kwenye relation!!!

Sis naona umenipata kabisaaa..... Ninaposema tongozo ni zile genuine tongozo, sio za kulazimisha.... na kutega ni kulazimsha.... atleast that is IMO.
 
Shem hapo in blue sio yategemea kweli? mbona your hommie enzi hizo alinitongoza mara 3 nikawa nampa za uso lakini hakukata tamaa mara ya 4 nikaingia line.... :redface: Na I know you know as I know kua ni Mwanaume hasa! lol
Hehehehe.... kile kibuti chako cha staki nataka?.... Hata mi nlijua tu ulikuwa unakataa kimagumashi...
 
Asante AD for this post. Mie langu moja tu, hivi, kutongozwa ni kitu cha kidini au? Yaani , kinakubalika kidini ?==> na hence muongozo kuwa ni lazima itoke kwa wanaume tu?
Au ni a generic term ambayo inaweza kutoka hata kwa wanawake?

Hofu yangu kubwa ni kuwa , kama ni jambo linalotakiwa kutoka upande mmoja, tiyari lina set precedence na mazingira yanayompa superiority m-gender mmoja dhidi ya mwingine.

Na hasa tukizingatia kuwa wanaume wana list yao ya 'wanavyovipenda' au kuvitamani kwa jenda hii ingine na hali kadhalika, wanawake huwa wana yao, na bado kuna vigezo-changia-kote i.e vinavyokubalika na ku feature katika list zote mbili.
Mfano, mwanaume atavutwa na umbile na sura ( asilimia kubwa, sijasema wote, kabla hamjanitovoga na bisbisi machoni), atapenda labda mwenye haya kidogo , though wengine wanapenda macho makavu, wengine wanapenda mwanamke independent ila eti awe submissive ( hapo inakuwaga ngumu kubalansisha ikwesheni ila ndo hivyo)etc.
Wanawake nao hupenda ( walio wengi) security in a man - mara nyingi hili hupimwa na juhudi ya kazi , mara nyingine pesa , na historia ya mafanikio maana hiyo pia itamu assure maisha bora ( sio wote jamani); uaminifu ( kigezo kigumu kabisa), un-mkatili ( sijui ndio mpole, au sijui nini but antonym ya mkatili- hapa nakumbuka lile tangazo la kwenye luninga la mwanaume ambaye akiingia home, hadi watoto wanajificha katika makapu) .

Lakini pia kuna vile vigezo changia kote kama uaminifu na ukweli ambavyo havina jinsia.
Na hapa natoa heshima ( pay respect, lol) to ukweli kuwa sio tongoza zote zitaishia katika ndoa. Najua zingine ni patapotea lakini sijataka kuketi ( ku base) katika utongozaji wa kihuni tu wa tamaa ( one night stands), ila zaidi katika ule utaoleta mahusiano thabiti.
Naomba kuwasilisha

Hapo in blue jamani, mbona sasa mtihani.... Kujua kama ni kidini ama vipi? And then kwa jamii za kwetu hizi naamini kabisa ni vema mwanaume awe ndo mtongozaji thou Mwongozo hata kwa mwanamke hutolewa japo mara nyingi kwa vitendo.

Mandawa umezungumzia vitu ambavo huweza vutia kwa wanaume na wanawake.... Take note kua mara nyingi mwanaueme aweza pata kirahisi yule of his choice (hasa basing on muonekano) kuliko mwanamke... Wanawake mara nyingi you compromise... waona kua this is better or less ya kile nitakacho but sio mbaya....

Tongozo za kuishia ndani ya ndoa ziko wapi? lol.... Mara nyingi togozo zote huishia tu kulalana na mahusiano.... na hio ya one night stand naona haipo katika tongozo ambazo nimelenga.... hahaha...
 
Kutongoza kumepungua sana nyakati hizi...incedentally na hata wanawake wanaohitaji mpaka watongozwe (ili 'watoe mzigo' kwa mfano!:thinking:) pia wamepungua/wanapungua kwa kasi. I will dare to say kuwa trend ni kwa wanawake wengi zaidi kujirahisisha/kufungua milango na hivyo dhana nzima ya kutongoza inapotea. So katika mazingira haya mwanamke anayengoja mpaka atongozwe anaweza kujikuta anangoja milele! Au pengine kama alivyosema AshaDii, inawezekana ni namna tu kutongoza kumebadilika!
Ladba nitoe true story yangu moja - zipo nyingi za namna hii zilinikuta kipindi hicho (na sasa? -mmmhh wife huwa anapita humu mara kwa mara:peep:):

Miaka kadhaa iliyopita, niliwahi kuishi mahala/mkoa fulani nikiwa kijana mdogo tu napata miaka 23 hivi na kwa kazi niliyokuwa nafanya, nilipewa nyumba ya kuishi kubwa tu, mwanzo tukishare na wenzangu wawili lakini baadae nikabakia peke yangu. Sasa kuna weekend moja akaja dada mmoja nyumbani kwangu (sikuwa nimemwalika! lakini ni dada ambaye nilikuwa namfahamu kidogo...ni mtu ambaye hata salamu ni mpaka mpishane karibu kabisa!)..ni mdada mrembo tu lakini kwa kumtizama tu alikuwa ni dada aliyenizi umri - ingawa nilikuwa na reserve shikamoo yangu (baadae katika stori niligundua anaishi kwa wazazi wake, hajaolewa, kanizidi miaka 6 na pia tayari ana mtoto mmoja!)....nikamkaribisha, nikampa muda wangu akasema kilichomleta, nikamsaidia alichokuwa anataka, na baada ya hapo hakutaka kuaga hivyo tukaendela kapiga stori za hapa na pale na muda wake wa kuondoka/au tuseme jua ndio lilikuwa limekuchwa akawa anaaga. Note muda wote huo, sikumtongoza wala kuonesha dalili kama nina nia ya kumtongoza (btw, nilikuwa sipendi ku date wadada walionizi umri sana) ingawa pia sikutaka kuashiria kuwa ningependa aondoke! Kwa kifupi zilikuwa ni stori za kawaida tu ambazo ningeweza kupiga na mwanamke yoyote au hata mwanaume mwenzangu. Na katika muda huo wa kukaa naye tulikuwa tayari tumetengeneza rapport ya aina fulani na hivyo ilikuwa rahisi kufanya 'vi' mzaha/au utani (lightly) kidogo. So wakati anaaga ilikuwa tayari kuna ka giza kameanza kuingia lakini alipokuwa anaaka sio mbali sana kutoka kwangua (some 10mins walk), so maagano yakwa hivi:

Mgeni: Nashukuru kwa msaada wako, Mungu akijalia tutaonana siku ingine.
SMU: Asante sana. Nilifikiri leo unalala hapa!?(ofcourse kwa mzaha/utani tu)
Mgeni: Kwani una kitanda cha wageni? (huku anacheka na kaaibu kwa mbaali!) - alikuwa anajuwa nilikuwa naishi na wenzangu na kwa muda huo wameondoka na vitu vyao (so vyumba vipo almost empty).
SMU: Nyumba mbona kubwa tu hii? Kitanda si nakupisha hata cha kwangu tu au kama vipi tunalala mzungu wa nne!(nadhani hapa ndipo nilivuka mpaka, so far, wa utani/mzaha na huyu dada - yeye alidhani nipo serious!)
Wote: Kicheko!.....kwi kwi kwi!
Mgeni: Nitalala siku nyingine...leo sijaaga nyumbani!
[SMU: Nimeingiwa na hofu kuwa sasa nimelikoroga, of course siwezi kumwambia asije tena!]
SMU: Wape salamu nyumbani
Mgeni: Nitazifikisha. Na wewe karibu nyumbani kwetu.
SMU: Asante (sikumsindikiza zaidi ya nje ya compund ya nyumba yangu!)

Baada ya wiki na nusu hivi, tukakutana na "Mgeni" katika mizunguko ya kazi. Tukasalimiana now kwa sababu ya kuzoeana tukasalimiana kwa karibu zaidi na kuulizana yaliyojiri tangu tulipoachana (kipindi hicho hakukuwa na mobile phones kama sasa maeneo mengi!). Wakati tunaagana Mgeni akasema atakuja nyumbani kwangu jumamosi inayofuata (siku hiyo ilikuwa jtano) - hakusema anakuja kwa shida gani na mimi sikutaka kumuuliza...nilikuja kufahamu baadae kuwa alikuwa anakuja kutimiza ahadi yake ("nitalala siku nyingine"!).

Dah..stori inakuwa ndefu...lakini to cut it short, alikuja hiyo jmosi. Kuna tofauti niliona...siku ya kwanza alipokuja alichagua kukaa kwenye kochi la single lakini mara hii alichagua kukaa lile la double:hand:!!!! na baade aliishia 'kulala' kwenye kitanda changu (...mzungu wa nne or otherwise...hili hatukupata muda wa kujadili tena!)

Lakini ninachotaka kusema ni kuwa kutongoza (actively) kunapungua sana....kuna mawasiliano na makubaliano mengi yanafanyika by implications na body language tu. Kwa mfano kwa namna anavyovaa mwanamke anaweza kutoa ujumbe kwa kukusudia au bila kukusudia fulani kwa 'potentials'! ipo mifano mingi na naamini wanaume wengi humu wanaweza kuwa mashuhuda.
 
Wengine Hawatongozeki na hata ukiwatongoza watakuona kama umechanganyikiwa, Na hiyo hali kwao imezoeleka. Eti Age haina nafasi, Oh please if that the case nafikiria kumtokea Bikidude je ataniona nina akili timamu? Au atahisi zishafyatuka?
 
Kwa mwanamke kutongozwa hakukwepeki hata ukijipiga kininja, atakuja ustadhi na kibaragashia atakutongoza, ukijivika sura ya kilokole, pia ataibuka mjuaji ajifanye anakufundisha neno mwisho wa siku anamwaga sera.

Kuna watu wao kazi ni kudeal na wake za watu, na wana kimsemo eti mke wa mtu hana gharama.
Kwa wanawake kutongozwa ni jambo la kawaida (sunnah) kama mnavyosema, tatizo ni kukubali kila unapotongozwa mmh hapo ndio noma kumkubalia kila mwanamme anaekutongoza.

Kingine kwa mwanamke ni type ya huyo mtongozaji kama anaendana na ww, kama utaona wanakutongoza hamuendani type hapo pia kuna question mark......!

tatizo leo j3 mikazi kibao hata kujiachia katika huu uzi inakuwa tabu.

Pole na kazi Scofield.... Huu uzi upo bana waweza endelea kuchangia hata baadae.... Kikubwa umechangia na baadae unaweza changia tena ukipata nafasi....lol

Nimekupata... post yako, na ndio maana kuta post nimegusia kua ingawa hili la kutotongozwa lipo, sio saana kivile. Na naelewa kua kuna watu wana ma theories na formulae zote za kuweza mpata mwanamke akipania!
 
Back
Top Bottom