Mwanamke kuomba pesa kwa mwanaume aliyezaa nae....!!!!

Mwanamke kuomba pesa kwa mwanaume aliyezaa nae....!!!!

Runner

Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
85
Reaction score
13
Habari wana JF,kuna jambo ambalo kwangu mm linanitatiza kidogo,utakuta kwamba mwanamke ameolewa hali akiwa tayari alishakuwa na mtoto na mwanaume mwingine kabla ya kuolewa,jamaa aliyemuoa alikubali kumlea mtoto katika hali yoyote ile,ila walikubaliana tu kwamba school fees baba mwenye mtoto ndio litakuwa jukumu lake,maisha yaliendelea lakini baadae mwanamke anaanza kuomba pesa kwa yule mwanaume aliyezaa nae na akiulizwa anasema ni ya vitabu au vitu vya mtoto,na kila mara ataomba pesa hata mara mbili au tatu kwa mwezi,na haitumiii kama vile alivyotoa sababu (vitabu/vitu vya mtoto)........Sasa hapa mimi najiuliza,hii ni sawa kwa huyo mwanamke kufanya hivyo hali ikiwa kwamba yule mtoto anapata kila kitu kotoka kwa yule baba anayemlea?....akiulizwa sana jibu lake ni kwamba "Yule ni baba wa huyu mtoto na atabaki kuwa baba wa mtoto na anawajibu wa kutoa pesa ya matumizi pale inapohitajika.
Wana JF naomba mchango wenu wa mawazo kwenye hili,je imekaa sawa hii au?
 
Hapo inategemea tokea mwanzo mlikubaliana vipi,ila haipendezi
 
Si sawa kbs,inaonekana huyo mwanamke ana kaujeuri flani na tamaa pia.inafaa achimbwe biti la kufa mtu na mumewe
 
Mh! Wanawake kama hao ndiyo wanawaaribia wenzao ambao wameshazalishwa, so inakuwa Tabu kupata mwanaume mwingine wa kumuoa, kwa sababu ya kusikia na kusoma Tabia za wanawake kama hao.
Back to the topic, huyo mwanamke ana tamaa, pia inaonyesha hamheshimu mumewe, maana kama mtu alikuzalisha na akakuona hufai, ukapata wa kukusitiri, ni ya nn basi uendelee kumfuata? kama ataweza kuomba pesa za matumizi, ni kwa nn asikuoe huyo wa mwanzo ambaye amemzalisha? Hii inawezekana hata mapenzi wakarudia kufanya, maana anamkaribisha ukaribu ambao hauna ulazima. Na pia kama walielewan na mumewe kuwa atamsaidia kumtunza mtoto huyo, basi na yeye ajishughulishe kutafuta school fee ya mwanae, na asimfuate kabisa baba wa mtoto, ili kulinda ndoa yek, na Heshima pia.
Kwa kweli huyo dada anamakosa sana, na anamdharau mumewe.
 
Hizo pesa ni kwa matumizi yake huyo mama
si sahihi kabisa, ila ampe tu coz mtt ni wake!

Akenajo...",jamaa aliyemuoa alikubali kumlea mtoto katika hali yoyote ile,ila walikubaliana tu kwamba school fees baba mwenye mtoto ndio litakuwa jukumu lake"........Kama uliisoma hii thread vizuri
 
Lisa labda nikwambie kidogo background ya huyo mwanamke...jamaa aliyemzalisha mara ya kwanza kabisa aliwahi kumpa ujauzito then akamlazimisha kuitoa mimba,mwanamke akakubali,baada tena akabeba mimba (ambaye mtoto ndo huyo aliyepo mpaka sasa hivi) jamaa akamlazimisha tena aitoe ile mimba bila mafanikio,jamaa alianza kumtesa na kumfukuza yule mwanamke kuwa hamtaki kwa kuwa alikuwa ni "material woman" na hawezi kuishi na mwanamke kama huyo.....mwishoni mwanamke akarudi kwao,akajifungua huku jamaa akikana kwamba mtoto si wake,baadae jamaa akajirudi akamkubali mtoto na kuamua kutoa posa amuoe yule mwanamke.....lakini baada ya kutoa posa jamaa alipotea kama muda wa miezi minne na kuja kujitokeza alikuwa ametangaza ndoa na mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni rafiki na huyu mwanamke tunaemuongelea hapa,na mpaka sasa ndo mke wa huyo jamaa.
 
Sasa wewe baba uliyezaa hutaki kumtunza mwanao?
Labda baba alikubali kwa sababu alikuwa anataka kumuwin yule dada sasa kampta na hataki tena.
Toa matumizi kwa mwanao mwanzo mwisho bila mipaka!
 
Runner, Mungu anasema kila ukitoa ndo anakupa zaidi.

Yani huyo mtoto anaweza kuwa anakuletea baraka hapo na wewe hujui, tuliza ball kijana we endelea kumhudumia tu mtoto wa mke wako:biggrin:
 
hapo jamaa asiwe mkali akiombwa pesa ya matumizi kwa mtoto,ni kutoa tu mwanzo mwisho kwani mtoto ni wako,kama unauchungu na mwanao basi kamkomboe ukae naye wewe ili huyo mwanamke asikusumbue tena,
huyo jamaa anayeishi na mwanao hawezi kuwa na uchungu kwa mtoto asiye wake,atajifanya kumsaidia mtoto kwa lengo la kumfurahisha mke wake ili apate kupewa penzi zaidi
 
Majibu ya huyo dada ni sahihi kabisa, lazima wababa wote tubebe majukumu ya kutunza watoto wetu hata kama wanaishi na baba wa kambo. Pia kumbuka HAWALA haachiki, labda huyu dada kakumbuka koni ya mzazi mwenzake.
 
Namanyele........huyu jamaa anayeishi na mtoto ambaye si wake hana tatizo na yeye ndio anayelalamika kwamba kwann mkewe amuombe pesa jamaa aliyezaa nae wakati yeye anamuhudumia kwa kila kitu?
 
ilipaswa anapotuma fedha ya ada atume pesa kamili...ya ada vitatu uniform schoolbus na kila baada ya muda fulani ni vyema ikiwa kila mwezi atume pesa kwa ajili ya mtoto (akubaliane na baba mlezi na mama mtoto kuhusu hilo) sio kumwachia majukumu mwanaume mwenzio ingawa hapo na mke anakosea kuomba omba kila mara. Ingawa anapaswa achunguze labda baba mlezi kapunguza huduma kwa mtoto......

hapo jamaa asiwe mkali akiombwa pesa ya matumizi kwa mtoto,ni kutoa tu mwanzo mwisho kwani mtoto ni wako,kama unauchungu na mwanao basi kamkomboe ukae naye wewe ili huyo mwanamke asikusumbue tena,
huyo jamaa anayeishi na mwanao hawezi kuwa na uchungu kwa mtoto asiye wake,atajifanya kumsaidia mtoto kwa lengo la kumfurahisha mke wake ili apate kupewa penzi zaidi

Wakati mwingine hao akina mama na wao nahisi wanaangalia upepo, coz wanawakatalia hao watoto, sijui ili waendelee kuwa mtaji?!
 
Hapo huyu mwanamke anaua ndege waawili kwa jiwe moja. Mtoto hapa anatumika kama kiunganishi halali kati yake na x wake. Mshauri huyu baba mlezi aweke pipaka ya kuwasiliana hawa watu tena achunguze vizuri kwani nahisi hawa x wanakumbushiana ya zamani au kwa lugha za mtaani wanasema kutengeneza face ya mtoto; Akili kumkichwa hapa wife wake analiwa kwa kofia ya mtoto huku yeye akiwa mshenga. Ogopa, ogopa ogopa mtu na x kuwasiliana hapa hamna kutongozana ni kuambiana na kufanya.
 
Lisa labda nikwambie kidogo background ya huyo mwanamke...jamaa aliyemzalisha mara ya kwanza kabisa aliwahi kumpa ujauzito then akamlazimisha kuitoa mimba,mwanamke akakubali,baada tena akabeba mimba (ambaye mtoto ndo huyo aliyepo mpaka sasa hivi) jamaa akamlazimisha tena aitoe ile mimba bila mafanikio,jamaa alianza kumtesa na kumfukuza yule mwanamke kuwa hamtaki kwa kuwa alikuwa ni "material woman" na hawezi kuishi na mwanamke kama huyo.....mwishoni mwanamke akarudi kwao,akajifungua huku jamaa akikana kwamba mtoto si wake,baadae jamaa akajirudi akamkubali mtoto na kuamua kutoa posa amuoe yule mwanamke.....lakini baada ya kutoa posa jamaa alipotea kama muda wa miezi minne na kuja kujitokeza alikuwa ametangaza ndoa na mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni rafiki na huyu mwanamke tunaemuongelea hapa,na mpaka sasa ndo mke wa huyo jamaa.
Kama unaweza kumshauri mwambie aachane naye, na asimame kwa miguu yake mwenyewe na alee mwanae bila kumtegemea huyo mwanaume, maana alishamuonyesha tangu mwanzo kuwa hamtaki, anatakiwa kuelewa hilo.Pia mwambie amheshimu mumewe wa sasa ambaye alimpenda bila kujali anamtoto nje ya ndoa na akamuoa.
 
Mwanamke ana tamaa.
Kuzaa na mtu haimaanishi kageuka ATM, period!

Na akiendelea kumuomba atamfunua sasa hivi
 
Back
Top Bottom