Mwanamke kumkimbia mume maisha yakiwa magumu na kurudi yanapokuwa mazuri

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,491
Habari wanabodi,

Nimeleta mada hii tujadili tuone ni wapi mtu anapokuwa sahihi na wapi mtu anakosea.

¤ Mkataba wa ndoa unawataka wanandoa kuvumiliana katika SHIDA na RAHA.

¤ Sasa chukulia mmeoana halafu inafikia mahali maisha yanakuwa magumu hata milo miwili inashindikana, hivyo mwanamke anaamua kumkimbia mumewe.

¤ Mwanaume anapobaki mwenyewe anaparangana japo maisha yanarudi kwenye mstari, na hapo mwanamke anaanza kutaka kurudi tena kwa nguvu kwakuwa bado ni mke halali? Usahihi wa huyu mwanamke ni upi.

Kabla hajaingia kwa nyumba, mwanaume alikuwa vizuri na pengine mwanamke alichangia ufukara katika familia hiyo kwani alipoondoka, mali zilirejea, na yeye akataka kurejea tena. Je kama wewe ndo mwanaume utampokea tena?

Tuangalie pande zote.

Karibu tuchangie.
 
mh,hapo hamna kitu Ndugu.Mwanaume alioa sura mwanamke aliolewa na pesa ndo lugha gongana inapotokea
 
mh,hapo hamna kitu Ndugu.Mwanaume alioa sura mwanamke aliolewa na pesa ndo lugha gongana inapotokea
ni shida! Pengine unaweza ukakuta kulikuwa na upendo wa dhati tu, maana unapozungumzia SHIDA na RAHA, na hujamjaribu mpenzi wako katika shida, siku ikitokea ndipo utakumbuka ile ahadi ya kuvumilia shida ilitoka moyoni ama mdomoni.
 
MTAFUTE WANAWAKE WACHAPAKAZI SIYO UNAOA MWANAMKE ANAKAA NYUMBANI TU HAFANYI SHUGHURI YEYOTE ILE HATA WAZO LA BIASHARA HANA NDO MATOKEO YAKE HAYO MUME UNAKWAMA YEYE MBIO
 
MTAFUTE WANAWAKE WACHAPAKAZI SIYO UNAOA MWANAMKE ANAKAA NYUMBANI TU HAFANYI SHUGHURI YEYOTE ILE HATA WAZO LA BIASHARA HANA NDO MATOKEO YAKE HAYO MUME UNAKWAMA YEYE MBIO
wapo wachapakazi ila siyo nyota njema. Hv kuna wanawake wenye mikosi?
 
wapo wachapakazi ila siyo nyota njema. Hv kuna wanawake wenye mikosi?
WAPO AISEE UNAKUTA KUNA MWANAMKE MCHAKARIKAJI HATARI ILA MWANAUME WAKE CHENGA TUPU HAYA MAMBO NIMEYAONA SANA MKUU I WISH NIWE NA MWANAMKE WA AINA HII ILI MAISHA YASONGE MBELE
 
Shida hazivumiliki msikie tu shida, pia inategemea mwanamke umemtoa katika mazingira gani? na njia gani ulitumia kumpata kuna njia zenye kumfanya mwanamke ajihisi bora na kutamba mbele za wenzake kwa yale madeko unayo mdekeza siku ukiwa na rumba juwa hatangoja In Shaa Allaah zako lazima atashika njia. Shida upelekea watu kutamani kuzaliwa mbwa Chicago kuliko kuwa binadamu Tanzania.
 
Kila jambo lina sababu, hata anaeingia katika ndoa ana sababu... Inapotokea sababu imeisha na hakuna sababu ya kuongeza sababu, basi sababu humuondoa mtu
 
Shida hazivumiliki msikie tu shida, pia inategemea mwanamke umemtoa katika mazingira gani? na njia gani ulitumia kumpata kuna njia zenye kumfanya mwanamke ajihisi bora na kutamba mbele za wenzake kwa yale madeko unayo mdekeza siku ukiwa na rumba juwa hatangoja In Shaa Allaah zako lazima atashika njia. Shida upelekea watu kutamani kuzaliwa mbwa Chicago kuliko kuwa binadamu Tanzania.
kwanini inakuwa vigumu sasa mwanzoni hakuweki sawa kuwa shida haivumiliki? Shida ikitokea anasepa, ikiisha anapata wapi ujasiri wa kutaka kurudi?
 
Habari wanabodi,
Nimeleta mada hii tujadili tuone ni wapi mtu anapokuwa sahihi na wapi mtu anakosea.

¤Mkataba wa ndoa unawataka wanandoa kuvumiliana katika SHIDA na RAHA.

¤Sasa chukulia mmeoana halafu inafikia mahali maisha yanakuwa magumu hata milo miwili inashindikana, hivyo mwanamke anaamua kumkimbia mumewe.

¤Mwanaume anapobaki mwenyewe anaparangana japo maisha yanarudi kwenye mstari, na hapo mwanamke anaanza kutaka kurudi tena kwa nguvu kwakuwa bado ni mke halali.

?usahihi wa huyu mwanamke ni upi. Kabla hajaingia kwa nyumba, mwanaume alikuwa vizuri na pengine mwanamke alichangia ufukara katika familia hiyo kwani alipoondoka, mali zilirejea, na yeye akataka kurejea tena. Je kama wewe ndo mwanaume utampokea tena? Tuangalie pande zote.

Karibu tuchangie.

Umesahahu pia kuna Wanaume ambao maisha yakigoma huwarudisha wake zao nyumbani kwao, hao nao vipi?
 
Umesahahu pia kuna Wanaume ambao maisha yakigoma huwarudisha wake zao nyumbani kwao, hao nao vipi?
kama wamekubaliana hamna tatizo ila kama ni mwanamke kukimbia, hapana. Kuna wanaume pia hukimbia kwenda kutafuta, akipata anarudi.
 
kama wamekubaliana hamna tatizo ila kama ni mwanamke kukimbia, hapana. Kuna wanaume pia hukimbia kwenda kutafuta, akipata anarudi.

Hivyo basi kumbe wote hukimbiana, siku nyingine jaribu kuangalia pande zote mbili na sio kulaumu Wanawake tu!
 
Maisha ni mitihani tuu,na unapoa au kulewa miezi flani ya kwanza kunakua na misukosuko sana,kufukuzwa kazi ,kukosa maelewano,mara Mchepuko wa zamani kaiga cm usiku basi ilimradi mitihani,sasa kama mwanamke au mwanamme hamjakua makini ndio mwanzo wa matatizo,kuna wanawake wengine au hata wanaume wengine wanakimbia familia zao
kisa mumewake hana pesa anabadilika nakua jeuri kupiliza mpaka ana kufanya mwanamme una changanyikiwa,na mwanamme nae anaweza kutafuta mwanamke wa nje kisa anakwambia mke wangu amebadilika sasa nashidwa kuelewa
amebadilika amekua shetani au anatembelea mikono? nijambo gani ambalo haliwezi kutatuliwa mpaka mtu unachukua maamuzi makubwa kama hayo au mtu anarejeana na Mpenzi wake wa zamani mie ikifikia hapo nakua sielewi kabisaaaaa..
 
Ni katika kutafuta amani huku kila mmoja hataki kijishusha. Pengine Kila mmoja anajiona yuko sahihi na msimamo aliochukua na upande mwingine unawaza hivyo hivyo. Hapo ndo inapoanza timbiri timbiri... Above all, inapotokea mmoja anakuwa mhanga zaidi ya mwingine ndo hupelekea maamuzi ya kumfanya aondoke kwanza au atafute mchepuko au arudi kwa mpenzi wake wa zamani. Ni scenarios nyingi sana... Ila kwa hilo la mtu kukimbia kukiwa na shida ni hatari na inakuwa haina maana ya kuishi katika ndoa.
 
Maisha ni mitihani tuu,na unapoa au kulewa miezi flani ya kwanza kunakua na misukosuko sana,kufukuzwa kazi ,kukosa maelewano,mara Mchepuko wa zamani kaiga cm usiku basi ilimradi mitihani,sasa kama mwanamke au mwanamme hamjakua makini ndio mwanzo wa matatizo,kuna wanawake wengine au hata wanaume wengine wanakimbia familia zao
kisa mumewake hana pesa anabadilika nakua jeuri kupiliza mpaka ana kufanya mwanamme una changanyikiwa,na mwanamme nae anaweza kutafuta mwanamke wa nje kisa anakwambia mke wangu amebadilika sasa nashidwa kuelewa
amebadilika amekua shetani au anatembelea mikono? nijambo gani ambalo haliwezi kutatuliwa mpaka mtu unachukua maamuzi makubwa kama hayo au mtu anarejeana na Mpenzi wake wa zamani mie ikifikia hapo nakua sielewi kabisaaaaa..
ila kweli kabisa mkuu hapo busara, hekima na imani lazima iwepo ili kulishinda
 
Unapo uoa au uolewa inamaanisha kuwa nyiny ni mwili mmoja hata linapokuja suala la shida na raha bado mtadumu na mtaendelea kupendana. Anapokukimbia kweny shida mnakuwa sio mwili 1 tena. Inabid km mwanaume ufikirie sana na uchukue maamuz magum sbb ipo siku 1 atakuua tu utapokuwa na mali nying ili azimiliki. Kiufupi wa namna hiyo mpe talaka tu ili kaishi maisha anayojua yeye.
Kuna wanawake weny gundu na wasio na gundu(wenye nyota ya utajiri). Ndio maana wahenga wakasema ''kosea kujenga nyumba na sio mke''
unaweza kukuta kijana kabla ya kuoa alikuwa ana mali nying sana na mambo yake yanaenda vizur san lkn baada ya kuoa kila kitu kinaharibika, biashara haend, kaz kafukuzwa, magonjwa hayaish n.k
au unaweza kumkuta kijana alikuwa choka mbaya au sio baada ya kuoa mambo yanaenda vizur sana, km alikuwa hana hata baiskel atanunua mpaka gari.
Kimsingi kuwa muangalif ktk suala la kuoa. Tumia akili nying, hisia kias na mshirikishe MUNGU 100%.. Na haya mambo sijui mnaita kunyonya k, m na, kufanya mapenz kinyume na maumbile inawafanya watu wae na roho ya kijambaz ktk mapenz. hamuwez kuelewa ila mtaelewa tu sbb haya mambo ndio yalifanya mji wa sodoma na gomora kuchomwa moto. Haya mambo yanatoa kbs hof ya Mungu na ndio sbb ndoa za siku hazidumu na usaliti umekithir sana. Angalia weng wanaofany hayo mambo huwa rahic sana kuwasalit wapenz wao sbb wamemuacha Mungu na kumfuata shetan na kuhararisha machukizo. Najua mtapinga lkn nyeupe itabaki kuwa nyeupe hata ukiibadili rangi.
Watu hawana hofu ya MUNGU.
 
Back
Top Bottom