Mbunge wa SIKONGE, Juma Nkumba ambaye anasifika kwa kuwa na vindevu kama Adolf Hitler au Bobby Mugabe, ameamua kuonyesha makucha yake jana jioni kwenye Mkutano wa Sungusungu hapa SIKONGE kwa kupiga marufuku akina Mama kujisaidia haja ndogo wakiwa Wamechuchumaa au Kuchutama.
Hili Swala limesababisha shida kubwa sana kwa akina Mama wa Sikonge na wakuja ambao hawana uwezo wa kuwa na vyoo vya kisasa vya kukaa kama vile vya watu wa majuu au mijini.
Jitihada kubwa zinafanywa kwa sasa ili kuwasiliana na
KIKUNGU wa JF ili aweze kusaidia mambo ya kisheria yanasemaje na Mtetezi wa haki za akina Mama wa SIKONGE ambaye pia ni member wa JF aitwaye
Kaunga akishirikiana na kiranja wa zamani wa Shule ya Msingi Chabutwa ambaye sasa amekuwa Mkulima kwa mara ya pili na yeye pia akiwa Member wa JF kwa jina la @ELNINO , wamesema watahakikisha hili jambo linafikishwa hadi kwa Jaji Mkuu na Mwanamuziki wa Rock wa Band ya U2 aitwaye BONO ili kutangaza Sikonge kama Kivutio kikubwa cha Utalii duniani kwa kuona Wanyama Mbugani na akina mama wakifanya vitu vyao bila kuvunja sheria ya Mbunge.
Pichani, Mama akiachia Maji bila kuvunja AMRI ya Nkumba.
Jeuri ya Nkumba inaletwa zaidi na Pesa ndefu aliyonayo ambayo kwa sasa hadi amefungua Chuo Kikuu chake hapa SIKONGE chenye jina lake. Chuo hicho chenye hadhi ya juu, kimemfanya awe anaabudiwa hapa Sikonge.
Pichani ni BUS la Chuo cha Nkumba na kulia ni Nkumba mwenyewe.
Hii habari imeandikwa leo 01/04/2013.