Mwanamke kakimbia na akili yangu

Mwanamke kakimbia na akili yangu

RAGNAR LOTH

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
698
Reaction score
1,605
Wana MMU leo mtashangaa sijaja nimelewa sana humu ndani, niko mtaratibu sana tofauti na siku nyingine. Ningelewa nadhani humu leo pasingekalika.

(Nilikua na mke) sijui kama bado ninae. Tangu siku naiacha familia yangu, kazi, heshima yangu mtaani na kazini, na ndani ya nyumba vimeporomoka kama ukuta wa tope ulionyeshewa mvua.

Mwaka 2016 mwezi wa tano nilianza kua na ukaribu na mfanyakazi mwenzangu kazini, ni binti huyo. Niliidanganya akili yangu kua sitoweza kuitelekeza family yangu kwa sababu yake lakini muda ukawa ni mwamuzi. Mahusiano yalianza na kushika kazi kiasi cha kuondoka nyumbani wiki 2 au tatu bila kutia mguu.

Huyu mwanamke nikiri aliichota akili yangu na ikachoteka. Alinijali sijpata kujaliwa na mke wangu kabla kama vile. Akanipa hadi na visivyotolewa. Family yangu muda huu ilishanililia vya kutosha, Ilikua ni swala la muda tu director wangu wa kazini kuanza kugundua madudu ya kazi zangu. Wafanyabiasha wako sensitive sana na kazi zao, baada ya miezi miwili tu "I was demoted at work".

Mshahara wangu uliporomoka zaidi ya nusu. Nyumbani ikawa siku nikirudi nataka wife anifanyie nilivyokua nafanyiwa na mwanamke yule (kunipa visivyopeka), Nakumbuka baada ya kama siku tatu mfululizo kunikatalia uchafu wangu nilimlazimisha nikambaka na kutimiza haja yangu na kutokomea kwa mchepuko.

Sauti ya kilio chako ule usiku haitokaa initoke akilini. Muda huo mapenzi na mdigo yalipungua zaidi ya punguzo la mshahara wangu. Nikawa simwelewi, anaweza kutoka usiku akaniacha nimelala akarudi asubuhi, nikiuliza anazua tafrani.

Kumbuka muda huo ni mwezi wa kumi niko na mdigo. Mapenzi na mdigo yalifika ukingoni nikaamua nirudi kwangu. Nikawa mtu wa mawazo sana kazini ndipo uchapombe ulipoanza. Hata kile kimshara kidogo nilichobakisha nakitumia kupiga ulabu. Nimepata sana ajali za pikipiki njiani usiku uso umejaa makovu. Muda si muda nikaona unyonge wa mama Yasi haupo tena na kapata ujasiri wa gafla, sikujali, nilichokua nawaza ni ulabu tu.

Siku moja nimelala chumbani kwangu usiku nimelewa ingawa akili yangu inafanya kazi nikasikia sauti ya kiume lounge ndani ya nyumba. Sikuweza kuamka nikafata yangu na tulishatengana na mama Yasi vyumba muda sana kumbuka. Asubuhi nikaamka kama kawaida kuelekea kazini natoka nje nakuta gari aina ya Range Vogue nje kwangu ndani ya geti langu. Nikapanda pikipiki yangu bila kufumbua mdomo wangu kuuliza aliyopo ndani. Jioni kama kawa piga ulabu rudi nyumbani nimejichokea hata kula sili.

Siku ya tatu leo naongea, nimeamka asubuhi nimeoga tayari chumbani kwangu natoka kuelekea kazini nakutana na jamaa kafunga taulo anaelekea bafu za public za familia ndani kwangu akitokea chumba analala mke. Simjui na sijawahi kumuona. Nikamwacha lakini niliamua walau niulize kinachoendelea kwa mama Yasi, niliingia bila hata kugonga chumbani mule na kumkuta akiwa kakaa kitandani. Kumuuliza kulikoni mwenzangu, nilichojibiwa ni kwamba.
"NIFUATE YANGU NIACHE KUFATILIA MAMBO YA WATU YATANITOKEA PUANI"

Nilipandwa na hasira nisijue cha kufanya, lakini baada ya kufikiri mawili matatu nikaamua niondoke nikaenda kujikomoa na ulabu sikwenda hata kazini. Jana na leo sijanywa hata tone la pombe natafakari cha kufanya.

Nimeona niwashirikishe wana MMU mnipe akili kwa sababu nahisi mwanamke kaondoka na akili zangu.
 
Duh...!! Nina bahati sana leo kukuta akili yako haijachanganyika na pombe... Ngoja ni komenti usiku hu huu kabla hujaenda kupiga vitu vyako ... Na kabla hujalewa tena tafadhali kamwombe radhi FaizaFoxy ulichomfanya ile siku unakumbuka lkn Mkuu..??
 
Keno myayaongee na mama Yasi iliwezekana kapimeni HIV


Ni kweli kabisa afya yangu imezorota kupita kiasi. Lakini sidhani kama kurudiana naye itawezekana tena. Kinachoniuma sio yeye kua na mtu mwingine lkn kumleta ndani kwangu ndo kunakonifanya nifikirie siku moja nirudi nimelewa niwangojee waingie ndani nichome nyumba moto nitokomee nikafie mbali .
 
Duh...!! Nina bahati sana leo kukuta akili yako haijachanganyika na pombe... Ngoja ni komenti usiku hu huu kabla hujaenda kupiga vitu vyako ... Na kabla hujalewa tena tafadhali kamwombe radhi FaizaFoxy ulichomfanya ile siku unakumbuka lkn Mkuu..??


FaizaFoxy ndo nani kijana?
 
Mh! Kweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu.

Ni kweli kabisa afya yangu imezorota kupita kiasi. Lakini sidhani kama kurudiana naye itawezekana tena. Kinachoniuma sio yeye kua na mtu mwingine lkn kumleta ndani kwangu ndo kunakonifanya nifikirie siku moja nirudi nimelewa niwangojee waingie ndani nichome nyumba moto nitokomee nikafie mbali .
 
Kweli muda ndio kila kitu, na ukiendelea kuusubiri muda badala ya kuongea na mkeo ipo siku utakuta rambo lenye nguo zako nje ya Geti.. Natumahi umesoma huu ujumbe kabla hujapiga tena Ulabu
 
Mh! Kweli asiyesikia la mkuu huvunjika guu.


Hii ni dharau kubwa Mkuu. Nimemfanyia mengi mabaya lkn kwa hili analolifanya linanipa akili mpya sio ile niliyokua nayo mwanzo
 
Kweli muda ndio kila kitu, na ukiendelea kuusubiri muda badala ya kuongea na mkeo ipo siku utakuta rambo lenye nguo zako nje ya Geti.. Natumahi umesoma huu ujumbe kabla hujapiga tena Ulabu


Umesomeka Joblee. Asante kwa muda wako. Na mimi sitasubiri ifike kote huko
 
Anahitaji mwanamume sawa lkn sio ndani kwangu, hata kama niko mlevi kiasi gani kulimezea nashindwa
Waambie wahame yeye na mr range watoto wako utalea mwenyewe au ukubali kuwa houseboy wao iko siku watakwambiab usafishe range wao bado wamelala
 
Wanawake wapole ndiyo tulivyo revange yetu ni ya maumivu sana kuna ex mmoja alinitenda sana amerudi anataka tulianzishe majibu niliyompa alinilaani na kuniblock kwenye simu yake


Ni kweli wanawake muda mwingine tunawatibua wenyewe lkn hata revenge nayo ina mipaka ujue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom