Mwanamke jifunze uvumilivu

Mwanamke jifunze uvumilivu

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
6,114
Reaction score
5,397
Habari wana MMU,

Kuna jambo linanitatiza,Jana amekuja wifi yangu mke wa kaka na kilio nikajua amefiwa kumuliza haya kumezidi nini? Anasema anataka kuachwa amesha choka na kuona SMS kwenye simu ya mumewe za mapenzi na hivi karibuni aliona msg na picha za mtoto kwenye simu ya mumewe akafatilia mpaka akajua kama mumewe ana mtoto mwengine.

Sasa amehama nyumba na anataka talaka yake, hapo alipo yeye ni mkubwa kuliko bro, ameolewa mwanzo ana watoto wawili na akazaa watatu na bro. Nilichomwambia astahimili alee watoto wake. Hakuna ndoa yenye raha moja kwa moja leo tamu kesho chungu

Na istoshe watoto wake anasomeshewa, maisha sio mabaya anayoishi tatizo la mumewe ajitahidi kumuomba mwenyezi mungu atatulia, anasema moyo wake hauchukui tena anataka talaka yake na watoto wake wawili kawachukua lakini mmoja karudi anasema anataka kuishi na ndugu zake.

Nimemwambia wifi anipe muda bro amesafiri akirejea nitaongea nae lakini ameshikilia talaka. Bro amesema talaka sio tatizo atampa aseme jengine. Lakini waungwana mie sitaki waachane sababu watoto watapata tabu, mama wa wifi nae nimeongea nae kanichamba utadhani mie ndio nilomuoa mwanawe sasa hapa nimebakia njia ya panda hata lakumwambia akanielewa sinaaaa.

Naomba mnisaidie mawazo ili hawa watoto waishi na wazazi wao kwa salama na amani.
 
Acha kabisa mkuu chukulia ni ww unakuta sms kama hizo kwa wife wako labda na mtoto wa mwisho unagundua sio wako lazima aumie hata kama aliolewa na watoto wa5
mKuu sisemi ni rahisi lakini astahmili kwa ajili ya wanawe sasa angalia 2kids na mume wa kwanza ,3kids na mume wa pili
what is next? na kwenye ndoa hakuna raha tupu na tafran pia ipooo,mie mkuu nimeletewa mtoto wa miezi mi 2 siku narudi
Honeymoon niliona kama naonewa,lakini nimestahmili na maisha yanakwenda...
 
Acha kabisa mkuu chukulia ni ww unakuta sms kama hizo kwa wife wako labda na mtoto wa mwisho unagundua sio wako lazima aumie hata kama aliolewa na watoto wa5
Wewe ni ME au KE?
 
Waache waamue wenyewe.. (Yani jiweke pembeni).
Lasivyo utabeba lawama zisizo zako
 
Uvumulivu huo unaotaka awe nao wifi yako ni wa aina gani?
Wifiyo kasema kachoka kuona message za wanawake katika simu ya mumewe,na kama haitoshi kaka yako kazaa nje kabisa.

Nimeshtuka kaka yako alipokubali kutoa talaka kirahisi.
Ni wazi amemchoka wifi yako ndio maana kashindwa hata kumficha mtoto wake wa nje.
Lengo lake lilikuwa hilo (mkewe aombe talaka) na limeshafanikiwa.
Wifi yako akiendelea kung'ang'ania hiyo ndoa atateseka sana.

Hivi kusomeshewa watoto ni nini?Ndoa maana yake ni makhaba yaliyokomaa yaliyopelekea ndoa.
Kama makhaba hakuna tena ndoa ya nini?
Jamani wanawake tuachane na hii kasumba ya kunga'ang'ania mateso kwa kigezo cha "kulea watoto, watoto watateseka"
Kama hakuna mapenzi tena katika ndoa hakuna cha zaidi ya kuachana.

Ni kweli, lazima apate tabu ya kuishi bila mume na watoto bila ya baba lakini amani ya moyo ni zaidi ya yote,mwisho wa siku maisha lazima yaendelee.
Period
 
Huyo Mwanamke atulie tu asiwe na maamuzi ya haraka ya kukimbilia talaka.

Nnavyojua ndoa si lelemama na asitegemee mazuuuri tu bila changamoto.

Ingawa sijaoa ila naamini kukimbilia kuachana ndio tatizo kubwa zaidi hasa kwa watoto.
 
Kuu sisemi ni rahisi lakini astahmili kwa ajili ya wanawe sasa angalia 2kids na mume wa kwanza ,3kids na mume wa pili
what is next? na kwenye ndoa hakuna raha tupu na tafran pia ipooo,mie mkuu nimeletewa mtoto wa miezi mi 2 siku narudi
Honeymoon niliona kama naonewa,lakini nimestahmili na maisha yanakwenda...
you have played your part..Mwisho wa siku yeye ndio mwenye maamuzi ya maisha yake.....Usijaribu ''kuuvaa'' uhusika wake sana..Amani ya moyo wake anajua wapi anaipata...
 
you have played your part..Mwisho wa siku yeye ndio mwenye maamuzi ya maisha yake.....Usijaribu ''kuuvaa'' uhusika wake sana..Amani ya moyo wake anajua wapi anaipata...
kweli mkuu ila nisingependa kuona wale watoto wanalelewa na mama mwengine sababau hukui huyo atakae kuja atakua na mapenzi kiasi gani na watoto..
 
Huyo Mwanamke atulie tu asiwe na maamuzi ya haraka ya kukimbilia talaka.

Nnavyojua ndoa si lelemama na asitegemee mazuuuri tu bila changamoto.

Ingawa sijaoa ila naamini kukimbilia kuachana ndio tatizo kubwa zaidi hasa kwa watoto.
Uko sahihi Mkuu na sio mtoto mdogo labda useme ndio ndoa yake ya mwanzo ndoa ya pili alitakiwa asome
kwenye ndoa ya kwanza lakini hata sijui ibilisi gani amemshika...
 
niwe mkweli tu akiwa finacially okey naishi naye na si kwamba namvumilia no naishi maisha kama vile nipo na business partner ndani .. aniguse asiniguse atajiju .. nitakapo mbana ni matumizi ya home na watoto wasome shule nzuri.. uhuni wanafanya ila akishatakiwa kutoa milioni kumi kwa mwaka akili itamkaa sawa.... sema kama hana uwiii nijiweke pembeni sababu soon ataniletea mizigo yake
 
Maumivu ya mapenzi ni mabaya sana bora kuacha kuliko kuja kufa kwa presha au magonjwa
Mkuu I can understand lakini how many times ataolewa nakuachika? Hakuna mzuri wa moja kwa moja
na sio kama namtetea my bro ila yeye akiwa kama mwanamke ajue mbinu za kumzuwia mumewe,talaka sio solution...
 
Kuu sisemi ni rahisi lakini astahmili kwa ajili ya wanawe sasa angalia 2kids na mume wa kwanza ,3kids na mume wa pili
what is next? na kwenye ndoa hakuna raha tupu na tafran pia ipooo,mie mkuu nimeletewa mtoto wa miezi mi 2 siku narudi
Honeymoon niliona kama naonewa,lakini nimestahmili na maisha yanakwenda...
Ni kweli mkuu akitulia atabadilisha maamuzi mwenyewe
 
Mkuu I can understand lakini how many times ataolewa nakuachika? Hakuna mzuri wa moja kwa moja
na sio kama namtetea my bro ila yeye akiwa kama mwanamke ajue mbinu za kumzuwia mumewe,talaka sio solution...
wifi yako kuachika siyo tatizo kwake ... we ndiyo unaona tatizo
 
niwe mkweli tu akiwa finacially okey naishi naye na si kwamba namvumilia no naishi maisha kama vile nipo na business partner ndani .. aniguse asiniguse atajiju .. nitakapo mbana ni matumizi ya home na watoto wasome shule nzuri.. uhuni wanafanya ila akishatakiwa kutoa milioni kumi kwa mwaka akili itamkaa sawa.... sema kama hana uwiii nijiweke pembeni sababu soon ataniletea mizigo yake
Hapo niko na wewe shosti,yeye ana gari nzuri na kila mwaka anabadilishiwa gari,watoto wana gari ya shule na driver wao
wazazi wake kila mwezi mahitaji yanapelekwa mpaka mwenyewe pesa ana chikichia,watoto wake wanasoma Feza school
shida ndogo ndogo hana mume alimwambia aseme anataka biasharagani kasema kusumbuliwa asubuhi hataki...
 
Back
Top Bottom