Mwanamke Je ushawahi kuwa na mahusiano na mwanaume mwenye tabia ya upekepeke....?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
dating-online.jpg



Sisi binadamu tuna tabia na mienendo inayotofautiana. Mara nyingi huwa tunatambuana kwa tabia au mienendo yetu wenzetu huita personality. Miongoni mwa tabia au personality inayowachanganya wanawake ni ile ya introvert, mimi ningependa kuiita upekepeke kwa kiswahili nadhani neno hilo linaweza kufaa katika kuelezea tabia hiyo.

Mtu mwenye tabia ya upekepeke, wakati mwingine watu huweza kumdhania kama ana aibu hivi, lakini si kweli watu wenye tabia ya upekepeke hawana aibu kama inavyodhaniwa bali ni watu ambao huishi katika dunia yao kifikra, wanapenda sana kuzingatia mawazo yao ya kina na fikra zao.

Mara nyingi hawapendi kujichanganya kwenye mikusanyiko ya watu na kama inatokea kufanya hivyo basi ni kwa wale watu ambao anawafahamu kwa undani. Wanasaikolojia waliowafanyia utafiti watu wenye tabia za namna hii waligundua kwamba pale watu wenye tabia za namna hii wanapojumuika katika mikusanyiko, hupoteza nguvu zao (kumbuka kwamba sisi tunazo nguvu zinazotuzunguka lakini huwa zinatofautiana kwa mtu na mtu, ndio maana wapo wanaoweza kuona yale yatarajiwayo kwa njia ya maono).

Baada ya kujumuika katika mkusanyiko wa watu kwa muda mrefu kidogo kwa mfano katika sherehe fulani hivi watu wenye tabia hii ya upekepeke (Introvert) huhitaji muda kuwa peke yao ili kurudisha nguvu zao walizopoteza (recharge)

Watu wenye tabia hizi wanaelezewa kwa kifupi kama ifuatavyo:

· Wanapenda sana kuwa peke yao
· Ni watu wanaozingatia sana mawazo yao
· Wanapenda na wanafurahia kutazama jambo na kulielewa kwa undani
· Wanavutiwa na uwezo walio nao wa kupima jambo na kulielewa kwa undani
· Siyo watu wa kuonyesha waziwazi hisia zao chungu, mara nyingi huwezi kujua hata kama wamekerwa na jambo,
· Ni wa kimya na wanaopenda kujitenga na mikusanyiko ya watu wasiowafahamu kwa undani na ndio sababu wengu huwadhania kwamba wana aibu au wanatawaliwa na msongo wa mawazo
· Wanapenda kujichanganya sana na watu lakini wale wanaowafahamu vizuri
· Wanapenda sana kupima jambo au mambo kwa kuchunguza kwa makini na kwa undani ili kupata majibu sahihi

Kwa wanawake wenye tabia hizi huwa haziwasumbui wanaume lakini kwa wanaume wenye tabia hizi mara nyingi wanawake hupata taabu sana kuwazoea, kwa sababu wanawake ni viumbe wenye kujali hisia na wanapenda sana kusikilizwa tofauti ana wanaume ambao kwao kila kitu ni powa tu.

Ni vigumu sana kwa wanaume wenye tabia hizi kupata wenzi wenye muafaka wa kujenga familia kwa sababu wanawake wengi hushindwa kuwaelewa na hivyo uhusiano kuvunjika,

Hapa chini nitaeleza wanaume wenye tabia hizi katika mahisiano:

shutterstock_152085611.jpg


1. Kuwakubali kama walivyo:

Jambo muhimu kwa mwanamke anapokuwa na uhusiano na mwanaume mwenye tabia ya upekepeke ni kumkubali kama alivyo, yaani bila masharti

shutterstock_151685072.jpg


2. Hupenda kupewa nafasi:

Watu wenye tabia ya upekepeke hupenda kupewa nafasi, ingawa kwa kawaida kila mtu anahitaji kupewa nafasi ya kuwa peke yake na kutafakati mambo yake akiwa peke yake lakini watu wenye tabia hii hupenda kupewa nafasi zaidi na kwa muda mrefu, pale ambapo labda mpenzi wake anamuhitaji yeye ndio kwanza anahitaji kuwa peke yake akitafakari mambo yake au akisoma kitabu cha maarifa fulani ambacho kimemvutia

couple-at-the-club.jpg


3. Kutovutiwa na mazingira ya aina fulani:

Kuna baadhi ya mazingira ambayo hayawavutii wanaume wenye tabia ya upekepeke. Kwa mfano kwenda club kucheza mziki, mikusanyiko ya watu asiyowafahamu, au kuzungumza katika hadhira ya watu asiyowafahamu, huwaweka wanaume wenye tabia hii katika wakati mgumu

15.jpg


4. Wagumu kushiriki katika mazungumzo:

Kuna wakati mwanamke anaweza kujikuta anaanzisha mazungumzo na mpenzi wake mwenye tabia ya upekepeke akajikuta anabeba mazungumzo yote peke yake. Tabia hii huwakera sana wanawake na mara nyingi wanawake huweza kuvunja ushusiano na mwanaume wenye tabia hii. Ni wanawake wachache sana wanaoweza kukubaliana na hali kama hiyo na kama watakuwa wamewafahamu wapenzi wao.


shutterstock_149437310.jpg


5. Huchukua muda mrefu kutatua migogoro ya ndoa:


watu wenye tabia ya upekepeke hujitahidi sana kuepuka kwa gharama yoyote kusigishana katika mahusiano, hususan kusigishana kunakoweza kupelekea kuwa na hisia chungu. Unaweza kuona pia kwamba watu hawa huchukua muda mrefu kutatua mogogoro katika mahusiano yao. Sio kwamba wana dharau, la hasha ni kwamba,wanapenda kufanya mchakato wa kumaliza mgogoro huo. Watu hawa muda ni kitu muhimu sana, wao huamini kwamba kila jambo linahitaji muda ili liweze kutatuliwa kwa umakini

Couple-Bed.jpg


6. Inapotokea kutofuatiana, mwanamke ajiandae kunyimwa haki yake ya tendo la ndoa:

Licha ya wanaume wenye tabia ya upekepeke kuhitaji muda wa kuwa peke yao pale inapotokea kutofautiana na wapenzi wao, lakini pia mwanamke asishangazwe na kitendo cha kunyimwa unyumba pale atakapohitaji. pale mwanaume mwye upekepeke anapohisi kutishwa au kuwekwa kiti moto, miongoni mwa maamuzi atakayochukua ni kutokutoa ushirikiano kwa mwenzi wake pale litakapokuja swala kujamiana. Inahitaji muda na mwanamek kurudisha mawasiliano ili kumrudisha mwanaume katika hali yake ya kawaida ili aweze kushiriki tendo la ndoa.


shutterstock_144807271.jpg


7. Mnapohudhuria sherehe jitahidi kuwa karibu naye wakati wote:

Wakati mtakakapokuwa na mtoko na mwanaume mwenye tabia ya upekepeke a mtakapokuwa mmehudhuria sherehe, mwanamke anatakiwa ajitahidi kuwa karibu na mpenzi wake muda wote wa sherehe. Wanaume wenye tabia ya uepekepeke wanajihisi kuwa wapweke hata pale wanapokuwa wamezungukwa na watu wasiowafahamu. Kwa kuwa naye karibu wakati wote hujihisi yuko salama.


couple.jpg


8. Kuwa na subira:

Wanaume wenye tabia ya upekepeke pia huchukua muda mrefu kufanya maammuzi, kama nilivyosema hapo awali kwamba, muda kwao ni kitu muhimu sana katika kufanya maamuzi. Mwanamke anaweza kujikuta amekuwa na mitoko mara kadhaa na mwanaume mweye tabia hii lakini bado akabaki na kitendawili kama jamaa amemkubali au hajamkubali. Wanaume wenye tabia ya upekepeke wana kawaida ya kujivuta sana katika kufanya maamuzi hususan katika kujenga uhusiano na mwanamke kuliko inavyotarajiwa. Kama mwanamke amegundua kwamba mwanaume anayetoka naye ni mwenye tabia ya upekepeke, basi anatakiwa awe na subira

couple-talking.jpg


9. Muulize kama kuna jambo linakutatiza, usimsemee:


Kama mpenzi wako ni mwenye tabia za upekepeke na kuna jambo linakutatiza muulize na usimsemee hisia zake. Wanaume wenye tabia ya upekepeke hawapendi kusemewa hisia zao, ni vyema ukamuuliza maswali na akikujibu yapasa utulie na kutafakari majibu yake kuliko kutafuta tafsiri unayoijua wewe na kumuhukumu, hamtaelewana.

Maya-and-Darnell1.jpg


10. Kamwe usije ukamzodoa hadharani:

Wanaume wenye tabia ya upekepeke huwa hawapendi kuwa kivutio kwa watu, hivyo kama mko kwenye mtoko, jitahidi sana kuepuka kutofautiana naye kutakakopelekea kurushiana maneno hadharani na kuvuta watu kuwaangalia. Ni vyema pia ukaepuka kumshtukiza na sherehe ya siku yake ya kuzaliwa karika mghahawa uliojaa watu wengi hatakuelewa na badala ya kufurahi atachukizwa na kitendo hicho kitu ambacho hata wewe hakitakufurahisha

couple-talking-pf.jpg


11. Mweleze kuhusu mwaliko mapema:


kaqma kuna tukio mahali fulani yaweza kuwa ni kazini kwako au kwa rafiki yako ambapo ungependa muongozane na mwenzi wako, basi mweleze mapema ili aweze kuamua kama atahudhuria au la. Lakini ni vyema ukamuweka wazi kwa kumweleza kwamba ana uamuzi wa kuhudhuria au kutohudhuria ili asijione kama unamlazimisha


calendar.jpg


12. Weka ratiba kama una mazungumzo muhimu:

Ni kawaida mtu na mpenzi wake wanapokuwa kwenye mitoko kuzungumza, lakini pale ambapo unaona kuna mazungumzo muhimu na yanayohotaji tafakuri, ni vyema kumweleza ili ajue kuliko kumshtukiza. Wanaume wenye tabia ya upekepeke wako makini sana katika kutofautisha mazungumzo ya kawaida na yale yanayohitaji tafakuri.


black-couple-do-men-wait-or-move-on.jpg


13. Unatakiwa kumsoma na kujua kile kinachoingia akili mwake:

Mwanamke mwenye uhusiano na mwanaume mwenye tabia za upekepeke anatakiwa ajue kumsoma na kumjua vizuri, ili kuepuka kutoautiana naye.

wenn3379516.jpg


14. Kamwe usimshtukize kumkuanisha na maafiki zako wapya:

kama umepata marafiki wapya na ungependa umkutanishe nao, ni vyema ukamweleza mapema lakini si vibaya ukawaeleza marafiki zako kuhusu tabia ya mpenzi wako ili wasije wakamchangamkia kupita kiasi na kumsababishia kujihisi kutokuwa salama au kutahayari.

Kwa kifupi ni kwamba, wanaume wenye tabia ya upekepeke, ni vigumu kubadilika, na siyo lengo langu kuwataka wanawake wawe watumwa wa wanaume wenye tabia hii. Lengo langu ni kuwasaidia kuwajua wanaume wenye tabia hizi na kujua namna ya kuishi nao. kama mnaweza kumudu sawa kazi kwenu, lakini kama hamuwezi basi achia ngazi maana usije ukajidanganya kwamba utambadilisha mwanaume mwenye tabia hiyo. Ni sawa na kujidanyanya mwenyewe...........

Copy to: Paloma, Lisa, Kongosho, mimisa, gfsonwin, snowhite, Nivea, miss wa kinyaru, Passion Lady, Lady doctor, King'asti, AshaDii, BADILI TABIA, charminglady, Asnam, Preta, Arabela, KOKUTONA, Madame B, MadameX, jouneGwalu, Asprin, Bishanga, HorsePower, sosoliso, DEMBA, mwekundu, Elizabeth Dominic
 
Kuna tabia zingine ukizijua huwa hazisumbui. Kwa mfano ukiwa na mume wa hivi au mke, kuwa kama yeye ili msikerane vinginevyo sisi waongeaje nahisi tutakwerwa zaidi.
 
Mh!! Kabla sijasoma hilo neno 'pekepeke' nikajua wale wapenda kupekua mambo ya mwenzie ,kumbe ni kinyume Loh! Asante Mtambuzi kwa kunipa new msamiati!! Nahsi kama nnahako katabia em ngoja nijichunguze tena!!
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaaaa!
Umeonaeee!!!
Lakini mbona nyengine kama katuonea vile!!!
Ngoja akuje atueleze vizuri!

Mh!! Kabla sijasoma hilo neno 'pekepeke' nikajua wale wapenda kupekua mambo ya mwenzie ,kumbe ni kinyume Loh! Asante Mtambuzi kwa kunipa new msamiati!! Nahsi kama nnahako katabia em ngoja nijichunguze tena!!
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi kwa maelezo yako haya ina maana hao wanaume wa aina hii wanahitaji wanawake ambao wataishi maisha wanayoishi hao wanaume.. Yaani mke anakuwa anakwenda na mood ya mumewe.. kama mume yuko na furaha basi na mke atakuwa na furaha.. Kama mume anahuzunika na mke nae atahuzunika.. Kama mume ata-introvert feelings zake basi mke atatulia bila ya kuuliza wala kum-nag mume wake mpaka pale mume atakapofunguka tena.. Najua wanawake wa aina hiyo wapo wengi na aina hii ya wanawake ndo watakaoweza kuishi na wanaume "pekepeke"..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mtambuzi ahsante kwa uzi mwanana, naomba umalizie tafadhali ili ni print na kumpelekea mke wangu, labda itapunguza ugomvi wa kila siku kwa kujua yuko na mwanaume wa aina gani.
 
ninauhakika kwa tabia hii ni watu wa kujiamini sana katika mapenzi hawakurupuki so kama chaguo the make the perfect one
 
Ila watu wa tabia hii watu wengine huwatafsir tofauti kabisa!mimi nilishapata kulalamikiwa kuwa ninaringa but I came to know kuwa nijitahid kujichanganya na watu wakati nikiwa chuo,duh aisee

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mtambuzi...

niliposoma hii mada nimegundua uzuri wa mwanaume huyu .... itakua ni mzito kucheat.............

maana mpaka ajishauri kutongoza, ajenge ukaribu , ajiridhishe na kuanza mahusiano..... safi sana aisee
Ahsante kwa kunikumbusha, hili nalo nililisahau.
 
am totally introvert ila mimi is to much ni mchoyo,bia nataka nijinunulie mm tu,penye kujumuika naona nakosa amani labda mkusanyiko uwe wa lazima na muhimu,Is there any psycological treatment?
Ngoja nifanye utafiti, huenda wanasaikolojia wana tiba.

Nitaleta majibu baadaye
 
Back
Top Bottom