Mwanamke huyu sasa nipeni ushauri wa mwisho.

Mwanamke huyu sasa nipeni ushauri wa mwisho.

Mremaaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
293
Reaction score
325
Wanajamvi nawasalimu sana, natumaini wu wazima wa afya na mmepokea mwaka mpya kwa furaha na amani tuzidi kupambana na hali zetu kwa mwaka huu mpya na Mungu atupe wepesi.

Great thinkers wenzangu naja tena mbele yenu kwa kuyaomba mawazo yenu makubwa yenye ufumbuzi wa mambo mengi ikiwamo Afya,biashara, kazi na Mahusiano.

Nashukuruni sana kwa ushauri na mawazo yenu makubwa mazuri katika nyuzi mbili zilizotangulia hapa jukwani mwaka ule wa 2017 zote zikihusu swala la mahusiano kati yangu na mwanamke ninayemtazamia kuwa ubavu wangu wa maisha, mengi mliyonishauri niliyafanyia kazi kwa kuyachambua na kwa uangalifu mkubwa hakika niliweza kutoka hatua moja ya mahusiano yangu na kwenda hatua nzuri na kubwa zaidi, "Leo naja tena kuomba mawazo na ushauri wenu ili niweze kusogea mbele zaidi au kufikia ukomo kufokana na mawazo yenu makubwa nitakayoyapata katika uzi huu"

Twende pamoja wakuu na mkasa huu

"1. Huyu bi mdada aliniomba ushauri tuanzishe biashara ya samaki ili kukuza kipato nikaona ni sawa maana ni mawazo mazuri ya maendeleo lakini nilisita kidogo baada ya kusikia atakayekuwa msimamizi wa shughuli nzima, akashawishi sana mwisho nilikubaliana naye tukaanza kwa kuchangia garama tulichanganya kiasi sawa cha pesa na aliyetakiwa msimamiaji wa biashara hii alikuwa ndugu yake tukatuma hela ili biashara ianze lakini mwisho hatujaambulia chochote sio faida wala mtaji wetu yapata zaidi ya miezi miwili sasa, mwisho akawa anaomba msamaha kwa yaliyotokea kwa kuwaamini ndugu zake na mwisho akataka anilipe kiasi nilichotoa mim nikaona hapana maana tumepoteza wote kwa namna ya kutokukusudia"

2. Ikatokea mara nyingine kuna jamaa anataka afanye naye biashara akataka ampe hela kama laki 5, akaniomba ushauri nikamwoba nionane na mshkaji, baada ya kuonana na mshkaji na kuongea naye nikaona sio mtu tunayeweza kufanya naye biashara nikamwambia tuachane naye, mwenzangu hakunisikia kwa siri kubwa akampa laki 3, bila mim kujua nimekuja kufahamu mambo yalovyomwia magumu hela hairidi wala faida haionekanii, akaniambia nikapambana mwisho nikaambulia ile hela ya mtaji laki 3 nikashukuru Mungu, nikahoji nilikukataza kwanini ulifanya hivyo? Anaishia kuniomba msamahaa, in fact nilikaa tu kimya kama mwanaume ila haikunipendezaa.

3.Kikubwa zaidi akaanza jukumu kubwa la kujenga huko kwa wazazi wake bila kuniambiaa nakuja kugundua mwenyewe, cha ajabu ameanza kujenga hana hata vibali vya kujenga na nyaraka zingine muhimu za ujenzi, mwisho nikamwelekeza vitu muhimu vya kufanya kabla ya ujenzi kafuatia mwisho akafanikisha, tukarudi mezani hee ilikuaje mbona hivyo anaishia kaomba msamaha, nikamezea tu ila naona ugumu mwingine wa vitu kama hivi" (issue sio kukenga issue mipango na taarifa)

4.Hili la mwisho ndo lililonifanya nije mbele zenu great thinkers
" Kaja kwangu ohoo mpenzi naomba hela niongezee hela ya ada, asubuhi yake nimetoka kumlipia mdogo wangu ada yupo chuo huko Moshi" (kama nilivyosema katika uzi zilizopita mwenzangu yupo masomoni ingawa ni mtumishi), mwenzangu akaanza ohoo nimemuudhii amekasirika sana, nikajiuuliza sasa jamani kama haya mahusiano ndo ya hivi ndoa inakuaje?? Wenye uzoeefu na mambo haya njoonii!! Kumsaidia ni jukumuu langu lakini ninapokuwa sina namna kwa wakati huo ni kukasirikiwa au kuvumiliana? Jamani hawa viumbee!!

NB: Mambo haya yote yanafanyika bila mipango wala utaratibu wa kutarifianaa na kupanga pamoja , mwisho nikamwambia afanye majukumu yake akimaliza aniambiee (Anadai majukumu yeye hayamzuii kuolewa sasa najiuliza ndoa nin kwa maneno haya si itafika kila mtu atataka afanye yake ndani ya ndoa? Je kuna ndoa ya kudumu hapo?)

Natangiliza shukrani na mnisamehee kwa uzi mrefu sana mawazo yenu makubwa ni muhimu sana kwangu asanteni sana.
Nawasilisha
 
Daah, pole mkuu! Kuna pasua kichwa hapo... kwa uelewa wangu hapo kuna serious problem ya umimi(ubinafsi)

Tuwasuburi manguli watupe mwongozo...
Asante, sawa mkuu ngoja waje wajuvi wa mambo!
 
Muda mwingine tatizo huwa halianzii kwa mabinti tunaotamani/kupanga siku moja wawe Mama wa familia zetu. Chimbuko la tatizo huweza kuanzia katika familia yake katika suala LA malezi, makuzi na mahusiano baina ya wazazi.

Kuna watoto walizaliwa familia ambazo Baba hakuwa akiwajibika katika kuilea na kusimamia mambo ya familia. Kwahiyo Mtoto anakuwa na mtazamo wa kutomuegemea Sana mwanamume kumpa "go ahead" au kushauriana katika maamuzi maana tangu anakuwa hajawahi kuiona hiyo nyumbani.
 
Kwa uelewa wangu siyo mwanamke mbaya ana udhubutu.
Sasa basii kuwa serious mwache kwa muda wa kama miezi 3 au 2 na umwambie sababu
Pima uombaji wake msamaha na anavyotubu akijirudi vya kutosha endeleza game la maisha
 
Sikia Mkuu...ukitaka kumjua mwanamke nikatika suala la pesa.

Hakufai Huyo ....atakupa umaskini kisha atamsha tuu ..subiri siku mdogowe awe amehitim...kwao kajenga ,biashara kajowekeza ,,naye huyo...

Alafu usikute izo.hela.zabiashara alimpa jamaa wake.( aloyempa unamjua ??? )
 
Huna mwanamke hapo..utanishukuru baadae...km mwanamke hawez kukusikiliza ujue una shida kubwa sana kwenye mahusiano yako....huyo kwa akili yake hiyo hata wewe anakuona kama fursa kwa ajili ya kujiinua mwenyewe....ana akili ya maisha ila kwa maslahi yake binafsi..
 
Hapo kuna ubinafsi wa kiwango cha standard gauge.
Tabia hiyo kama hajaitoa kwa wazazi wake hasa mama basi anamshauri wake tena wakike ambaye anamsikiliza kila kitu anachomshauri.
Pengine hakuamini sana na anaona unaweza kumpa ushauri wa kukwamisha mipango yake wakati sio kweli.
Kiukweli naona wingu jeusi limetanda kwenye ndoa yenu na kizazi mtachokizaa kinaweza kupata hayo mapokeo ya ubinafsi wa changu kwanza.
Kwakuwa bado hamjafunga ndoa mna uhuru wa kufanya maendeleo yenu binafsi lakini ni vyema mkaanza kushirikishana ili kupeana ushauri jinsi gani ya kufanya kwa ufanisi zaidi.
Huyo mwanamke bila shaka ni mchaga, samahani lakini.
 
Duh hapo binafsi naona huyo mwanamke anavumilia njaa yake katika huo uhusiano kwa mateso sana ilihali hakupendi kwa dhati. Mwanamke akikupenda kwa dhati ya moyo huwa anasikiliza.
 
Hapo kuna ubinafsi wa kiwango cha standard gauge.
Tabia hiyo kama hajaitoa kwa wazazi wake hasa mama basi anamshauri wake tena wakike ambaye anamsikiliza kila kitu anachomshauri.
Pengine hakuamini sana na anaona unaweza kumpa ushauri wa kukwamisha mipango yake wakati sio kweli.
Kiukweli naona wingu jeusi limetanda kwenye ndoa yenu na kizazi mtachokizaa kinaweza kupata hayo mapokeo ya ubinafsi wa changu kwanza.
Kwakuwa bado hamjafunga ndoa mna uhuru wa kufanya maendeleo yenu binafsi lakini ni vyema mkaanza kushirikishana ili kupeana ushauri jinsi gani ya kufanya kwa ufanisi zaidi.
Huyo mwanamke bila shaka ni mchaga, samahani lakini.
Asante kwa ushauri mkuu, nimekupata sana kwa kwa kifupi hata mama yake mzazi hamsikilizi kuna jambo lingine nilimshauri kumbe kaomba ushauri na kwa mama yake mwisho wa siku hakusikiliza hata mmoja akaanguka nikamwambia nilikwambia akaishia kusema we na mama mawazo yenu yakulaumu badala ya kunifariji! Nikajua kumbe aliombaa ushauri kuwili lakini hakutusikilizaa! Ahaa acha mkuu ni shiida sana! Sio mchanga mkuu!
 
Kwa uelewa wangu siyo mwanamke mbaya ana udhubutu.
Sasa basii kuwa serious mwache kwa muda wa kama miezi 3 au 2 na umwambie sababu
Pima uombaji wake msamaha na anavyotubu akijirudi vya kutosha endeleza game la maisha
Asante kwa ushauri mkuu
 
Hapo ndio wanawake wanapoumiza kichwa...umenikumbusha yule binti aliniomba hela anataka kuanza kusoma masters kumbe kaongezea kanunua passo
Pole mkuu changamoto sana hawa viumbee tuliopewa kuwa wabavu wetu!
 
Wanawake wana makosa na sisi wanaume tuna makosa yetu. Ikiwa hamna muda wa kupeana mashauri na kukubaliana kwenye maamuzi ya maisha yalio wazunguka. Basi hio ndoa yenu itakuja kuwa na changamoto kubwa sana baadae.
 
Hakuna haja ya kumkasirikia mwanaume kisa hajakusaidia, kama huwa anakusaidiaga basi asipokupa jua hana.

Mm sijui mungu atanibariki ndoa ya namna gani? Nikibahatika Mme akanipenda mengine namwacha afanye kama bonus maana sio lazima.

Mahusiano bana wengine wanalilia kupenda wengine kusaidiwa? Kusaidia utashi wa MTU unless kuna ulazima, mfano kwenye ugonjwa
 
Hakuna haja ya kumkasirikia mwanaume kisa hajakusaidia, kama huwa anakusaidiaga basi asipokupa jua hana.

Mm sijui mungu atanibariki ndoa ya namna gani? Nikibahatika Mme akanipenda mengine namwacha afanye kama bonus maana sio lazima.

Mahusiano bana wengine wanalilia kupenda wengine kusaidiwa? Kusaidia utashi wa MTU unless kuna ulazima, mfano kwenye ugonjwa
Kumbe bado jimbo lipo huru?? Nakuja tuyapange
 
Back
Top Bottom