Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,609
- 1,734
Hata umpende vipi. Na hata umsifie sana. Tena hata umpikie vyakula vitamu na vinono. Au umnunulie zawadi nzuri nzuri. Vile vile umsaidie kimaisha na kimawazo. Umuimbie nyimbo tamu pia. Siri zako zote za moyoni hali kadhalika umweleze. Walio wako nao wamkubali.
Ila ukimnyima kitu kimoja tu. Yaani kimoja tu atanyong'onyea wee. Kama samaki nje ya maji atatapatapa. Mwanawane hatatulia mpaka apate hicho ulichomnyima. Popote pale atakitafuta - huku, pale na kule. Lo akishakipata rijali atatulia tuli kama maji kwenye mtungi.