MWANAMKE ALIYEPO KWENYE CHANGAMOTO HANA UWEZO WA KUFANYA MAAMUZI MAZURI YA UHUSIANO
Na
Comrade Ally Maftah
Wanaume wengi tunaingia katika changamoto ya kuwasaidia wanawake kupata mafanikio wayatamanio na baada ya wao kufika kwenye mafanikio haya wanatutema.
Baada ya utafiti wangu wa kina nimegundua kwamba kuna kundi la wanaume wenzangu tumedumbukia kwenye janga la hiyo na hii ni kwa sababu -:
1. Mwanamke akiwa katika changamoto ya mkwamo wa kiuchumi au kukosa ada ya shule ana uwezo wa kufanya lolote ajinasue, atakuwa tayari kufuata maelekezo yako mpaka atakapofanikiwa.
2. Mwanamke akishafanikiwa anatafuta uhuru wa kimahusiano yaani ampate mtu ambaye ni kweli anampa burudisho la nafsi yake.
KIPI ANAKIFANYA AKISHAFANIKIWA
1. Kukudharau na kukuona upo chini ya viwango vyake kimaisha na kielimu.
2. Kutafuta kasoro zote zilizopita huko nyuma na kuziwasilisha upya na hasa kasoro zinazohusu uwezo wa kumudu tendo la ndoa, ili akuondoe kabisa mchezoni asipate mtu wa kumkanya.
NINI MWANAUME UKIFANYE
1. Msaidie mwanamke kwa kiwango chako ambacho hakitakutoa katika uchumi wako, ukiona majukumu yanakuzidi jichomote katika mtego huo mapema
2. Ikitokea mwanamke umemfikisha sehemu na kakukataa "KAUSHA" hakuna mtu humu duniani atakaa upande wako katika kesi ya hivyo, sana sana kuna mwanaume mmoja yeye na kundi lake litaungana na huyo mwanamke na ndugu wa mwanake kumtafutia uhuru.
KITABU CHA SIASA KAZI MAARIFA KITAZUNGUMZIA HAYO
Ndimi
Comrade Ally Maftah
MSHAURI WA NDOA
View attachment 2899272