Mwanamke auawa kikatili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke auawa kikatili

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Feb 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,612
  Trophy Points: 280
  Mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30 ambaye hakutambuliwa jina lake, ameuawa kikatili na kisha kukatwa sehemu zake za siri na watu wasiojulikana.

  Mwili wa mwanamke huyo umegunduliwa asubuhi ya Februari 16, mwaka huu, katika kitongoji cha Magema, kijiji cha Nyamarembo, kilometa kama sita kutoka makao makuu ya wilaya ya Geita ukiwa umewekwa chini ya mti mkubwa ukiwa bila nguo.

  Mwili huo uligunduliwa na mwanamke aliyekuwa katika matembezi yake na kisha kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na kuibua hofu kubwa katika mji wa Geita na vitongoji vyake, huku wengi wakilihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.

  Mwenyekiti wa kijiji hicho, Alexi Evaristi, amesema kuwa baada ya kugunduliwa kwa mwili huo walitoa taarifa polisi ambao walifika katika eneo hilo pamoja na daktari na baada ya uchunguzi mwili huo ulizikwa jirani na eneo ulipookotwa kutokana na kutotambuliwa.

  Hata hivyo, baadhi ya wananchi, akiwemo Twikalehe Bwire ambaye ni kiongozi wa shina namba 4 lilipotokea tukio hilo, walielekeza shutuma zao kwa waganga wa kienyeji ambao wameibuka kwa wingi katika maeneo hayo licha ya serkali kufuta leseni zao.

  Kwa upande wake, Kamanda wa Ulinzi wa Jadi katika kitongoji hicho, Sung'ho Gamaya, pamoja na kulihusisha tukio hilo na imani za ushirikina, alidai kuwa maiti hiyo ilihamishiwa eneo hilo baada ya mtu huyo kuuawa sehemu nyingine tofauti.

  Alisema katika eneo ulipokutwa mwili huo hapakuwepo na dalili zozote za kuwepo kwa pukurushani, hali inayowafanya waamini huenda mwili huo ulipelekwa eneo hilo baada ya kuuawa na kunyofolewa sehemu ya siri.

  Tukio hili limekuja huku kukiwa na ongezeo la waganga wa jadi wanaodaiwa kuendesha huduma hiyo kwa kuhamahama ikiwemo kufikia katika nyuma za wageni na kuzungunguka mitatani na vijijijini kutafuta wateja.

  Afisa Utamaduni Wilaya ya Geita, Mufungo Pharesi, alipotakiwa kuzungumzia kuwepo utitiri wa waganga wa jadi wilayani humo wakiwemo wanaodaiwa kutoka nje ya nchi, alisema hatambui kuwepo kwa waganga hao kwani vibali vyote vilishafutwa.  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mzizi naye anapotea jukwaa duh.
   
 3. kiagata

  kiagata Senior Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  poleni wana-Geita kwa msiba huo.Hata hivyo mtu anafariki hata ndugu na jamaa kushindwa kumtambua?,au hakuaga nyumbani?.
   
Loading...