Mwanamke apigwa na glass usoni baada ya kuongea kiswahili Marekani

bizzle for shizzle

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
1,012
741
Mwanamke mmoja raia wa Marekani mwenye asili ya Afrika amemsamehe mtu aliempiga na bilauri (glass) ya kunywe bia usoni baada ya kumsikia akongea kiswahili.

Asma Mohhamed Jama aliekua pamoja na familia yake wakipata chakula cha usiku mgahawani mnamo Oktoba 30,2015 nchini Marekani alisikika akiongea lugha ya kiswahili ndipo Jodie Burchard-Risch (43) alipompiga kwa kumrushia bilauri usoni na kukimbia ambapo na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za uso wake ikiwa ni pamoja na kwenye pua,siko la kulia na mdomoni.

Bi.Asma aalitangaza mbele ya Mahakama kuu mjini Minnesota,Marekani kuwa amemsamehe aliempiga na kusema kuwa utofauti wa rangi,lugha na dini uliopo miongoni mwa binadamu si kitu kwani binadamu wote ni sawa na kumtaka Jodie Burchard-Risch kuchagua kuwa na upendo kwa kila mtu badala ya kuwa na chuki ambayo mwisho wa siku huwa chanzo cha madhara.

Bi.Asma anadai kuwa tukio hilo limebadili maisha yake kwani hapo awali alikua akipenda kutembea ila kwa sasa hatoi mguu ndani kwenda popote akiwa mwenyewe.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo amehukumiwa kwenda jela miezi 6 na atakua chini ya uangalizi kwa muda wa miaka mitano.
 
huko marekani huwa kuna vituko sana.sasa sijui angesikika anaongea kiarabu ingekuaje.
 
Habari ya mwaka 2015 tena October wewe unaleta leo takribani miaka miwili sasa. We have only some hours kwenda 2017 tena huna aibu unatoa habari kama hii. Nyie ndo wale wanafunzi mwalimu akifundisha mnakaa mwaka mzima hadi kuja kuelewa.
 
Back
Top Bottom