Mwanamke aolewa na wanaume wawili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke aolewa na wanaume wawili

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Che Kalizozele, Jul 24, 2011.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani hapa, Veronica Saleh ‘Mama Kaela' (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

  Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa' wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

  [​IMG]
  Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela' (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

  Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, zililifikia gazeti hili na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

  Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji ya iitwayo kayoga.

  Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

  Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

  "Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. "Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni," alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

  Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

  Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

  Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

  Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

  "Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

  "Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine," anasema mmoja wa majirani hao.

  Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

  Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

  Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba' wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

  "Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

  "Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana," alisema Katekista Abel.

  Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

  Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

  "Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?" alihoji.

  "Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?" alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

  Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.

  Ndugu wa Arcado wao wanalaani kitendo cha ndugu yao kuolewa na mama huyo, wakidai kuwa walishamshauri na kumuahidi kuwa endapo ataachana na mama huyo watamwozesha mwanamke mwingine, lakini yeye Arcado, amedai kuwa yuko tayari kufa, lakini si kuachana na mama huyo, kwani ndiye ubavu wake wa maisha.

  "Sasa tumebaki tunamwangalia tu huyu ndugu yetu Arcado, tumemshauri, lakini mkaidi, hatusikilizi. Basi nasi hatuna la kufanya zaidi ya kumwangalia," alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa Arcado. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Florence Katobasho, alikiri kuwa mwanamke huyo anaishi kinyumba na wanaume wawili na wanaishi kwa amani kwani hajawahi kufikishiwa malalamiko yoyote kuhusu wanandoa hao.

  "Ni ukweli usiopingika, kwamba Mama Kaela anaishi na wanaume hao wawili … lakini kwa kuwa sijafikishiwa malalamiko yoyote kuhusu maisha ya wanandoa hao, mimi kama kiongozi hapa sina la kufanya na siwezi kuwafukuza, kwa kweli wanaishi kwa amani, mengine ni yao," alisema Mwenyekiti wa Kijiji.

  Source: Habarileo

  Kwanza sikuwahi kuwaza hii kitu inawezekana.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. l

  lasix JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  mmmh makubwa haya.kweli duniani kuna mambo...
   
 3. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  No comment....
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Revolutionary woman! Amecome openly kuliko wengi wetu wenye wapenzi wa siri watatu or more! Big up waume wa mama kaole kwa kuishi kwa kuelewana!

  Imagine threesome chumbani? May be they won't reach that extent!
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  hao wanaume watakuwa wanamtegemea huyo mwanamke kiuchumi...njaa mbaya sana.
   
 6. Pawaga

  Pawaga JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  yah hapo ni njaa tu inawasumbua hakuna la zaidi.
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Mhhh hii kali pia iliwahi tokea mwanamke mmoja sinza-afrika sana kuwa na ndoa ya wanaume wawili na wote anawahudumia bila ya wao kujijua!!duuh ana ubavu huyu bibie maana standard inatakiwa kwa wiki umuingilie mkeo mara 4 sasa hao wawili ina maana mara 8 kwa wiki duuh anawezaje kila siku kutoa mzigo?
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  industrial revolution
   
 9. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hahahahahha, Njaa haina Baunsa
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mwanamke si chombo cha kushiriki mwanaume mbili labda kwa siri lakini cyo kwa wazi km inavyosomeka thread hii,Mi nafikiri ni njaa tu.
   
 11. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani hapa, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

  Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

  Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

  Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, zililifikia gazeti hili na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

  Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji ya iitwayo kayoga.

  Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

  Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

  “Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

  Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

  Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

  Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

  Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

  “Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

  “Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

  Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

  Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

  Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

  “Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

  “Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.

  Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

  Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

  "Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.

  “Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

  Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.

  Ndugu wa Arcado wao wanalaani kitendo cha ndugu yao kuolewa na mama huyo, wakidai kuwa walishamshauri na kumuahidi kuwa endapo ataachana na mama huyo watamwozesha mwanamke mwingine, lakini yeye Arcado, amedai kuwa yuko tayari kufa, lakini si kuachana na mama huyo, kwani ndiye ubavu wake wa maisha.

  “Sasa tumebaki tunamwangalia tu huyu ndugu yetu Arcado, tumemshauri, lakini mkaidi, hatusikilizi. Basi nasi hatuna la kufanya zaidi ya kumwangalia,“ alisema mmoja wa ndugu wa karibu wa Arcado. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Florence Katobasho, alikiri kuwa mwanamke huyo anaishi kinyumba na wanaume wawili na wanaishi kwa amani kwani hajawahi kufikishiwa malalamiko yoyote kuhusu wanandoa hao.

  “Ni ukweli usiopingika, kwamba Mama Kaela anaishi na wanaume hao wawili … lakini kwa kuwa sijafikishiwa malalamiko yoyote kuhusu maisha ya wanandoa hao, mimi kama kiongozi hapa sina la kufanya na siwezi kuwafukuza, kwa kweli wanaishi kwa amani, mengine ni yao,” alisema Mwenyekiti wa Kijiji.
   
 12. M

  Mwera JF-Expert Member

  #12
  Jul 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni,na hii ni dunia ya mwisho.
   
 13. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,577
  Likes Received: 925
  Trophy Points: 280
  Hii ni kiboko!
   
 14. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mmmmhh...?!?!
   
 15. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sani kumbe inawezekana
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  Jul 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  It is about time!

  Inafurahisha kusoma kuwa mwanamama huyu ndiye mwenye kauli ya mwisho. Haya kwa wakina Sophia Simba ambao wamekuwa wanaimba mwanamke 'akiwezeshwa- anaweza' wakapate tuition kwa huyu mama kuwa huitaji nyenzo toka kwa mtu mwingine kufanya kile unachotak.

  Hongera mama kwa 'kuoa'waume wawili!
   
 17. M

  Masuke JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkisikia wanasema haki sawa kwa wote mnadhani wanamanisha nini?, ni pamoja na hayo, du ila huyo mama ni kiboko.
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  afadhali amefungua njia. mtendwa akitendwa huona kaonewa eh? tungejee network ambayo itakuwa wazi. yaani mke ana waume 2, na hao waume nao kila mmoja ana mwanamke wa nje. na hao wanawake wawili kila mmoja wao ana mwanaume wake. ngoja nitengenezee network model!
   
 19. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hilo limbwata balaa
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  sijawahi ona wala kusikia kitu kama hiki.......
   
Loading...