Mwanamke Anayetoa Machozi ya Damu Kila Anapolia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
1790150.jpg

Rashida Khatoon Sunday, April 19, 2009 4:12 AM
Mwanamke mmoja nchini India amejipatia umaarufu na kuwa gumzo nchi nzima kutokana na hali yake ya kutoa machozi ya damu kila anapolia. Rashida Khatoon mkazi wa mji mmoja kaskazini mwa India, amewashangaza hata madaktari kwa hali yake hiyo ya kutiririka machozi ya damu kila anapolia.

Kwa siku mwanamke huyo humwaga chozi la damu mara kadhaa.

"Sisikii maumivu yoyote, badala ya machozi ya kawaida, damu zinapotitirika ni kitu cha kushangaza" alisema mwanamke huyo ambaye amekuwa gumzo sana nchini India.

Viongozi wa dini wa India wanadai kwamba mwanamke huyo ni miujiza toka mungu.

Kutokana na umaarufu mkubwa aliojizolea mamia ya watu wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa mwanamke huyo kujishuhudia wenyewe kwa macho yao.

Wageni hao wamekuwa wakimmiminia mwanamke huyo na familia yake zawadi kadhaa kila wanapomtembelea nyumbani kwake.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1790150&&Cat=7
 
duh!!!

sasa kila siku analizwa nini!
machoz yamekuwa kitega uchumi!!
 
Tezi zilizo katika macho hutoa machozi unapolia, wengine wanapocheka sana, ama kuingiliwa na kitu jichoni, sasa huyu tezi zinatoa damu, nadhani kama ingefaa kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kitaalam na madaktari bingwa katika macho.
 
naona yeye kishapata kamtaji kazuri atainua kipato chake so ni ujasiriamali mzuri.
 
Akacheki afya yake.... siajabu ni ugonjwa huo yeye kageuza mtaji
 
akacheki afya yake.... Siajabu ni ugonjwa huo yeye kageuza mtaji


mi nadhani yuko mwezini. (ile bleed ya menstruation). Na sio ugonjwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited:
Ina maana kila watu wanapomtembelea hulia ili kudhihirisha ukweli wa hili jambo? kama ndivyo, nini basi kinachomfanya aweze kutoa hayo machozi kila akipata hao watembeleaji?
 
Hali hiyo ya kutoka machozi ya damu ni miongoni mwa miujiza inayokwenda kwa jina la "Stigimatta" wengine ikiandamana na kutoka damu mikononi, miguuni na ubavuni kama mateso ya Yesu kwani alitoka machozi na jasho la damu.
Iliwahi mtokea mtawa mmoja wa Katoliki Culcutta India. Mara nyingi hutokea kwa sanamu za bikira Maria kuwa na huwa anajitokeza kama alivyowatokea mabinti watatu wa Fatima.
 
Back
Top Bottom