Zabron Erasto
Member
- May 29, 2011
- 47
- 3
Mwanamke inasemwa katika vitabu vitukufu si kiumbe cha kupigwa, kunyanyaswa, kusimangwa au kubughudhiwa. Mwanamke ni pambo la nyumba, nuru ya macho, asali ya roho, kato la kiu, upepeo wa jasho fukuto la baridi, safina baharini, ndege angani, gari nchi kavu, barafu ya moyo na furaha ya maisha. Bila mwanamke hakuna furaha katika maisha. Kama wanawake wote waliopo watapotea au kuangamia basi itakuwa dhahama tupu katika dunia. Ijapokuwa walimwengu walisema mwanamke ni kivuli cha ugomvi. Bado mwanamke alikuwa