Mwanamke anastahili KIPIGO au UPENDO? Ooh !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke anastahili KIPIGO au UPENDO? Ooh !!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Zabron Erasto, Jul 9, 2011.

 1. Z

  Zabron Erasto Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanamke inasemwa katika vitabu vitukufu si kiumbe cha kupigwa, kunyanyaswa, kusimangwa au kubughudhiwa. Mwanamke ni pambo la nyumba, nuru ya macho, asali ya roho, kato la kiu, upepeo wa jasho fukuto la baridi, safina baharini, ndege angani, gari nchi kavu, barafu ya moyo na furaha ya maisha. Bila mwanamke hakuna furaha katika maisha. Kama wanawake wote waliopo watapotea au kuangamia basi itakuwa dhahama tupu katika dunia. Ijapokuwa walimwengu walisema mwanamke ni kivuli cha ugomvi. Bado mwanamke alikuwa
   
 2. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  mwanamke anastahili kipigo au upendo???
  swali kama kipima joto.
   
 3. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  anastahili vyote. cha kwanza upendo, ukimpata utatakiwa kumtengeneza aendane na wewe hapo katika kumtengeneza ndio pagumu sana na huwa panaishia kipigo, baadaye yeye akishajiona kuwa yuko chini yako na anatakiwa kukusikiliza wewe baba wa kuendesha nyumba, yaani baba kichwa cha familia, atashuka chini,atakuwa mpole na hapo unatakiwa umpende na kumfurahisha, mdekeze na mpe raha ya maisha,....yeye atakishi na kufurahia maisha yote, lakini akijua kuwa kuna mipaka fulani hivi kati yako na yeye, yaani hatakikwi kuvuka mipaka akivuka msijeanza vurugu.....

  mwanamke yeyote ambaye hajawahi hata kusukumwa tu, ajue bwanake ni *****....watu wawili mliokulia familia mbili tofautitofauti wote meno salasini na mbili mkija kuishi pamoja wakati wa kusomana lazima migogoro itakuwepo, na kunakuwa na kushindana fulanifulani kila mtu anataka kuonyesha yeye fulani, na mwingine anaweza kutoka na tabia za kwao anazileta pale...so hapa kipigo huwa kinatokea...hata kama wanawake humu ndani watasema si kweli, wanaweka siri tu moyoni, washakula kipigo na bado wanawapenda waume zao.....

  baba mpole ni *****, ukiona hata mama hamtishii mtoto kwamba, acha utundu baba anakuja...basi ujue mwanaume wa nyumba hiyo ni *****, limbwata limemmaliza...
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wapo wanawake bila kipigo hawaendi kabisa na heshima hakuna

  but mimi na prefer mwanamke ambae mnazungumza yanaisha....
  kupigana sometimes inakuumiza hata wewe.....

  if u are cruel to someone,u are hurting yourself in process too
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli mgando sio kwenye maziwa tu....
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Hii imekaa kama kiukweli ukweli kabisaa sitaki niharibu hapa. Nisisitize tu kwamba mwanamke akijua kwamba yeye lazima ashuke na mwanaume awe baba kichwa cha familia na nyumba basi hakutakuwepo kipigo. Ila kama mke naye anataka kufanya maamuzi ya kibaba na kutaka kutawala ujue vrugu zitaanza na mwathirika mkuu huwa mwanamke yaani anaambuliwa kipigo. Hiki kipigo ni muhususi kumfanyia adjustment ili arudi kwenye line yake na siyo kumwonea( yaani ni sawa na kufungua nati iliyolegea na kuikaza upya).
   
 7. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  You're right 100% ; wanawake wa namna hiyo kwenye red ni very very few mkuu na hili linaleta shida sana. Mwanamke mnapooana unamweleza kabisa huwa sipendi hiki wala kile vivyo hivyo naye anakueleza dislike na donts zake. Baada ya miaka miwili tu ya ndoa anaanza kufanya yale uliyomkataza na ukimwonya anakuwa mkali na hapo hurudia mara kwa mara. Inategemea sasa wewe ni mwanaume wa namna gani; kama mnywaji huamua kukaa baa hadi usiku ili akija akute mke kesha lala na kama si mnywaji ndo hulazimisha mkewe amweelewe na hapo lazima kipigo kitaanza kama bado wife haelewi.

  Nawauliza kina mama mlioko humu katika situation kama hiyo hapo juu mnategemea mwanaume afanye nini?
   
 8. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  au vipi, si bora tuseme ukweli tu tuwasaidie wengine ambao wanataka kuingia kwenye ndoa?
   
 9. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwanamke hastahili kupigwa, mwanamke ni mkarimu sana hasa mwenye mapenzi ya ukweli,kama amekosa muite pole pole umueleza atakuelewa,mwanamke hupigwa kwa busu,na mapenzi sio ngumi kumbuka kua ulimuoa hukumnunua kwao sasa kwanini umpige?
   
 10. M

  MORIA JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mwanamke hasthili kipigo hapo unatengeneza kitu ingine kabisa hasa ukiwa na watoto wa kike na wakaona/akawahadithia jinsi unavyomtandika, hapa ndipo unatengeneza hatia na hawa binti kushindwa ktk ndoa zao siku za mbeleni..,vile vile ukatili kupita humfanya mama kuwa baridi kutofika kileleni
   
Loading...