Mwanamke anaomba ushauli, baada ya kukimbia ndoa yake

Mwanamke anaomba ushauli, baada ya kukimbia ndoa yake

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
4,007
Reaction score
5,970
Mama wa mtoto mmoja, niliolewa lakini nilishindwana na mume wangu kutokana na tabia zake za umalaya, alikua ni mtu wa wanawake sana nikaamua kuondoka na kudai talaka.

Tuliachana mwaka juzi mwanzoni, nilikaa mwenyewe kama mwaka mmoja hivi lakini kutokana na upweke nikatafuta mtu wa kujituliza nae ambaye ni mume wa mtu.
Huyu Baba ananipenda na ananijali sana na nina furaha. Tatizo, napata wivu sana kila akienda kwa mke wake, yaani naumia mpaka nashindwa hata kufanya kazi zangu, naomba nisaidieni, nifanye nini? Yaani anapoondoka nakua naumia sana naishia kulia tu, mke wake yuko mkoa mwingine, hivyo akiwa huku muda mwingi anakua kwangu.
Akiwa huko hataki hata nimpigie simu anadai kuwa mke wake atajua, lakini mimi akiwa kwangu anaweza kupigiwa simu na mke wake wakaongea hata masaa mawili; ni haki hii kweli? Nimekua nikiumia sana, nashindwa kuvumilia, naomba ushauri, natamani nimpigie simu mke wake ili nimuambie kuwa tuko wawili ili angalau niwe na amani, niwe na uhuru wakumpigia simu akiwa huko na mke wake. Jamani, nateseka.
 
Aisee yaani Umeacha mumeo.. then umeenda kutafuta waume wa wenzio.

Umeruka mkojo umekanyaga mafiiii
 
Back
Top Bottom