Mwanamke ananikatalia kumuona mtoto

Mwanamke ananikatalia kumuona mtoto

Jumla ya hela zote ambazo aliwahi kumtumia ni 215,000!!! [emoji15] [emoji15] [emoji15]

Yap, na hizi nilituma siku moja aliugua ghafla akawaelekeza waliompeleka hospital wanipe taarifa ndo nikatuma 115000 maana nilikosa ruhusa nikashindishwa kwenda
Next time aliniomba kwa ukali sana nimtumie hela kwamba hana hela ya matumizi ndo nikatyma kilo, lkn mahusiano hayakuwa mazuri muda wote mpk sasa.
 
Kama ulivyoshauriwa na mkeo mtarajiwa usimtelekeze mtoto. Endelea kutuma hela za matunzo ya mtoto. Wakati utafika wa kumuona mwanao
 
Yap, na hizi nilituma siku moja aliugua ghafla akawaelekeza waliompeleka hospital wanipe taarifa ndo nikatuma 115000 maana nilikosa ruhusa nikashindishwa kwenda
Next time aliniomba kwa ukali sana nimtumie hela kwamba hana hela ya matumizi ndo nikatyma kilo, lkn mahusiano hayakuwa mazuri muda wote mpk sasa.

Mkuu huon km wewe nj tatizo!!?kitu gani kikubwa hpo??kwnn uciende kwa wazaz wke ukafata taratibu ili ulee mwanao???coz binti hawez kusaliti wazazi wke kwa sababu yko bado ypo chin yao na ndo wanamuhudumia kwa ukarbu!!!!unataka shortcut utasubir sna na kuna wazazi wanamcimamo,ukiona vp chukua ushaur hpo juu futa kilA kitu anza upya yaan ufanye km huna mtt!!!!!
 
pole, ila nimejaribu kuangalia sababu za wewe kuachana naye hazina mashiko flan hivi inshort huna msimamo na ukipata changoto unaikimbia na una kiburi, hupendi kujishusha hii tabia itakuumiza sana. nenda ukawaone mkubaliane kiroho safi namna yakumlea mwanao hivi neno samahani ni shingapi? hadi uchoke kuja huku ungeshayamaliza
 
Hiyo mimba ya miezi nane si mbaya... question
Sababu zote tatu ulizotoa hazina maana, mara dini, mara kabila mara ananibana.... question
huonekani uko serious kabisaaa.... question
jumla ya matumizi yote ni 215,000/- mkuu umefungua ledger kabisa ya matumizi ya huyo dada? ni mtaji huo? .... question!

Its either umetunga story au you are very immature
 
Nna imani mpaka unataka kuoa umeshakua Mwanamme kamili wakuweza kuchukua majukumu,elewa kua mwanamke
nikiumbe dhaifu sana na hasa anapokua mama,mzazi mwenzio amekua na kiburu sababau ya kosa labda na hakupata ushirikiano wako wakati ma ujauzito na niamini mda ule unahitaji sana kua na mwenzio mlie shiriki lile tendo ili mfurahie
kila mtoto wenu akikua tumboni ila yeye hakupata,jaribu jaribu kuondoa EGO na hutokosa au hutaumia uki apologies
kwa mzazi mwenzio wala kwa mazazi baba yake na mama mtoto wako, zaidi utafaidika,kua karibu sana na mtoto wako na
hata huyo unae muoa utamuelewa kwenye mapungufu yake, sisemi usimsikilize Baba lakini kumbuka yeye nafasi yake kwa
mtoto wako ni Babu wewe ni BABA wa mtoto,am sure unataka umpe mwanao maisha bora kwa kadri ya uwezo wako,
unaposema umegundua wewe si mgumba,je kama yule akiwa ndio mtoto wako wa mwisho hutopata tena mtoto utajisikiaje?
jee mke utakae oa akiwa hawezi kupata ujauzito?

Usiwe hivyo mwenyezi mungu ndio anajua maisha ya kila mtu usikubali kumuacha mtoto wako akakosa malezi na
Mapenzi ya Baba,waache wao wawe kibri lakini wewe unafanya kwa ajili ya mtoto wako na kumbuka Sio lazima
Ushinde kila ugomvi kushindwa nako pia ni ushindi sababu umekubali matokeo... sorry kama ntakua nimesema sana..
Nasupport.. 100%
 
Kwanza nikupe pole kwa kuuziwa mbuzi kwenye gunia nasema hivyo kwa kuwa kama mlikutana mwezi wa august alitakiwa ajifungue mwezi mei tena sio tar za mwanzo nakusihi usiwe na papala za kukubali hicho kiumbe utalea mtoto asiye wako.Kama unataka una maswalo mengi tafadhali tutawasiliana
 
Nenda kwao tu kaonane na wazee wake, ufuate taratibu zao watakazokupa. Ukiona zinakubana sana, chagua sheria kupata haki yako kwa mwanao.
Kuna wanawake wanapenda kuwatumia watoto wao kwenye relationship kama mwanamme hakupendi yani hamna sababu then the best way ndo hiyo yako paulo
 
Laki 2.5 unalia!? Yalinikuta, M8 mhaya kala,duka nimepanga anauza badae aambiwa mtoto siyo wangu. Siku za nyuma kaanza tena, oh marumizi ya mtoto lakini nikiimba tu picha ya mtoto anaishia mpaka wiki ndo atanisemesha tena; sasa yamenikuta siyo nilisikia kwa watu! Ukiendeleza ujinga huo hutafanya jambo lolote. Kama unaoa oa tu! Mtoto si ana baba yake? Kama ni wewe utapewa. Kama si wako atapewa mwenzio. Mama yake ndo anajua mtoto wa nani. We una uhakika? Tulizana kaka! Walinichamba hapa ila we endelea na mambo yako. Tena kwa raha zako.Ingekuwa umekataa kumsaidia nisingekuelewa. Umenyimwa af unang'ang'ana!
 
dogo wewe kigeugeu..hata tukikupa ushauri baba yako anaweza kukuambia usifuate ushauri wa jf. Jibu maswali haya kisha nijuwe dozi ya ushauri inayokufaa usije ukajiuwa bureee.
1- umri wako ni gani?
-DOGO UMEJIBU UNA MIAKA KARIBIA 30YRS...ILA TABIA YAKO INAREFLECT KIJANA MWENYE UMRI TEGEMEZI WA WAZAZI..BADO HUJAKUWA KIAKILI KIASI CHA KUFANYA MAAMUZI YAKO BINAFSI BILA KUTEGEMEA WAZAZI WAKO...REFER MAMA HAKUPENDA KABILA LAO, BABA AKANIAMBIA ACHANA NAYE ETC.
2- unaishi kwako au kwa wazazi wako?
-DOGO UNAISHI KWAKO SABABU UMEAMIA MWANZA KIKAZI..NINA WASIWASI KAMA BADO UNGEKUWA MKOA MMOJA NA WAZAZI UNGEKUWA AU ULIKUWA UNAISHI KWA WAZAZI..MTOTO WA MAMA (REFER UMESEMA NI MTOT WA PEKEE WA KIUME)
3- kwanini unataka kuoa? je wazazi wamekulazimisha au wewe mwenyewe umeamua?
- UMESEMA UMEAMUA MWENYEWE...INAWEZEKANA NI KWELI ILA KWA WELEDI WANGU NAONA KAMA UNAKIMBILIA KUOA SABABU YULE ULIMTIA MIMBA NA UKAWA PRESSED KUMUOA ILA DINI, KABILA NA JEURI NDIO VIKAKURUDISHA NYUMA. HUYU UNAYETAKA KUMUOA MWEZI WA 8 NAYE NI KATIKA LILELILE SUALA LA KUKURUPUKA KUTIMIZA LENGO LA KUOA. LAKINI KUMBUKA...NDOA SIO KITU CHA KUKIMBILIA, INAHITAJI UTULIVU NA KUJIULIZA MASWALI MENGI KAMA WHY, WHAT, WHEN, WHO NA KADHA WA KADHALIKA.
4- kwenu wewe ni mtoto wa ngapi kuzaliwa na mko wangapi?
- DOGO UMESEMA WEWE NI MTOTO WA PEKEE WA KIUME...UKO SAHIHI, UNA TABIA HIZO ZA HAO WATOTO NA MARA NYINGI HUWA HAZIKO TOFAUTI NA WATOTO WA KIUME WA MWISHO "LAST BORN / SINGLE BORN SYNDROMES" NYIE HUWA MUNADEKEZWA KIASI KWAMBA MUNAKUWA WATOTO WA MAMA NA MUNALELEWA MPAKA MUNAPOKUWA KWENYE NDOA AU MAHUSIANO YENU. REFER..BABA SAID THIS, MOM SAID THAT...HUNA UTEGEMEZI WA FIKRA YANI BADO NI MTOTO MPAKA UNAINGIA KABURINI AU WAZAZI WATANGULIE...HUWA MUNAKUWA NA WAKATI MGUMU SANA KWENYE NDOA ZENU...MUNAENDESHWA NA WAZAZI WENU.
5- kwanini hukutaka kwenda kwa wazazi wa mwanamke uliyemtia ujauzito?
- SIJARIDHIKA NA JIBU LAKO ILA KWA MAELEZO YAKO YA AWALI WEWE NI KIBURI NA JEURI...ILA KUMBUKA KAMA MKRISTO UNATAKIWA KUWAHESHIMU BABA NA MAMA UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI...WAZAZI WA MZAZI MWENZIO NI WAKWAKO PIA..NDIO MAANA WANAITWA BABA NA MAMA MKWE. DOGO HUNA HESHIMA IN SHORT UNATAKIWA UBADILIKE..HESHIMA KITU CHA BURE.
6- una uhakika kuwa mimba ni yako? kivipi?
-UMETOA JIBU JEPESI SANA...NAKUIBIA SIRI NYEPESI TUU...KILA MWANAMKE ANAPOJIFUNGUA HUPENDELEA BABA WA MTOTO WAKE AWEPO AU BASI AJUWE KUWA ANAJIFUNGUA..HAIJALISHI UGOMVI MKUBWA KIASI GANI. CHUNGUZA UPYA MAANA HATA TAREHE ZA HIYO MIMBA ZINATIA SHAKA.
7- ulitumia kipimo gani kujua mimba ni ya wiki 2?
-MIMBA NYINGI ZINAKUWA DETECTED BAADA YA MWEZI MMOJA...WATAALAMU WATANISAIDIA KUNIPINGA...HIYO YA WIKI MBILI NI UONGO.
8- nisaidie level yako ya elimu?...diploma degree masters au phd?
-ELEMU INAKUTOSHA KUFANYA MAAMUZI MAKUBWA NA MAGUMU ZAIDI YA HAYA ULIYOLETA TUKUPATIE USHAURI...NAPATA WASI KAMA ULIPATA ELIMU NA INAKUSAIDIA AU ULIENDA CHUO KUPATA VYETI UPATE AJIRA.
KAZI KUBWA YA ELIMU NI PAMOJA NA KUTATUA MATATIZO YANAYOKUKABILI KWA KUTUMIA RASILIMALI ZILIZOTUZUNGUKA....NATIA SHAKA ELIMU YAKO KAMA INAFANYA HAYO.

9- ndoa ni nini kwa mujibu wa imani yako ya dini?
-SIO MUUMINI WA DINI YA KISABATO ILA NAAMINI KAMA MKRISTO MWENZANGU UNAYETUMIA BIBLIA.....NDOA YA KWANZA ILIKUWA PALE MUNGU ALIPOSEMA KATIKA BUSTANI YA EDENI..."NITAMFANYIA ADAMU MSAIDIZI WA KUFANANA NAYE...KISHA AKAMTIA USINGIZI AKAMTOA UBAVU UPANDE WAKE WA KUSHGOTO NA KUMTENGENEZA KIUMBE WA KUFANANA NAYE..KISHA ADAM ALIVYOAMKA AKAMUITA YULE KIUMBE MWANAMKE/EVA"
-DOGO UNAHITAJI MSAIDIZI WA KUFANANA NAWE...SIO WA KUFANANA NA BABA AU MAMA YAKO, AU BABA AU MAMA YAKE, AU DINI YAKO AU YAKE, AU KABILA LAKO AU LAKE.
HAYA YA DINI, KABILA SIJUI RANGI NA KADHALIKA NI MASUALA YA WAZAZI WAKO..WEWE UNAYEFANANA NAYE NDIO HUYO..ACHANA NA WAZAZI WAKO WALA WAKE.

10- unaoa mwezi wa 8, ulianza lini mahusiano na huyo unayemuoa au ulikuwa nao wawili kwa wakati mmoja?
- DOGO ULIVYOJIBU INAONYESHA HUYU UNAYEMUOA FASTA NI PLAN B..X-GIRLFRIEND WA O-LEVEL. KUWA MAKINI DOGO, TULIZA AKILI NAKUONA UNATOA BOKO UTAJILAUMU BAADAE.
11- unajiona ukiishi kwenye ndoa mpya na wakati unampenda mzazi mwenzio na kutamani kumllea mtoto uliyezaa na mzazi mwenzio?
-DOGO SIO KWAMBA HUJAELEWA SWALI..SEMA UMEONA TABU AU UKAKASI KUJIBU KUWA ITAKUWA NGUMU KUISHI NA MKEO WAKATI UNA MTOTO UNAYEMPENDA UMEZAA NA MWANAMKE AMBAYE WAZAZI WAKO HAWAMPENDI KISA DINI NA KABILA...UKIOA MUKACHELEWA KUPATA WATOTO NA MKEO NAKUONA UKIHAMIA KWA MZAZI MWENZIO KUMLEA MWANAO. ANYWAY UKWELI UNAO MWENYEWE.
12- umemwambia mzazi mwenzio kuwa "kuna mtoto ulizaa na mwanamke mwingine ila umekimbia kumuoa?
lete majibu nikupe dozi ya ushauri.
- DOGO KILA MWANAMKE HUWA NI MZURI SANA NA ANA ROHO NZURI KABLA HAJAINGIA NDANI YA NDOA...ULITAKA AKUAMBIE MWAGILIE MBALI HUYO MWANAMKE NA MTOTO WAKO ILI UMWAMBIE ANA ROHO MBAYA?...MUOE NDIO UJUWE KWANI WASWAHILI WANASEMA MAMA WA KAMBO SIO MAMA.
 
Laki 2.5 unalia!? Yalinikuta, M8 mhaya kala,duka nimepanga anauza badae aambiwa mtoto siyo wangu. Siku za nyuma kaanza tena, oh marumizi ya mtoto lakini nikiimba tu picha ya mtoto anaishia mpaka wiki ndo atanisemesha tena; sasa yamenikuta siyo nilisikia kwa watu! Ukiendeleza ujinga huo hutafanya jambo lolote. Kama unaoa oa tu! Mtoto si ana baba yake? Kama ni wewe utapewa. Kama si wako atapewa mwenzio. Mama yake ndo anajua mtoto wa nani. We una uhakika? Tulizana kaka! Walinichamba hapa ila we endelea na mambo yako. Tena kwa raha zako.Ingekuwa umekataa kumsaidia nisingekuelewa. Umenyimwa af unang'ang'ana!

Ahsante kaka, nami nimekuwa na hofu sana na jinsi anavyojiamini, huenda tupo mtu 2, nadhani ushauri wako unafaa kiasi flani
 

Haya ndugu , lkn niseme tu kwamba Mimi sio such mtoto wa kudeka kama ivo maana nimekuzwa na mama wa kambo baada tu ya kuachishwa nyonyo hivyo dhuruba nazijua hasa nikiandika walaka hapa unaweza tokwa na machozi , lkn pia ni fighter mzuri tu wa maisha , labda Gari ndo sijabahatika ingawa Mungu akijaalia nitanunua 2018,
Ahsante kwa ushauri ingawa sio counselor mzuri maana unamshambilia client kisaikolojia ila sio mbaya maana nimeomba ushauri.nitafanyia kazi
 
Jamani Nashukuru sana Kwa dhati kwa ushauri wenu mzuri uliotolewa hapo juu,
Nimeamua kuufanyia Kazi kuanzia leo asubuhi, kwa kuongea na huyo mdada, nimeamua kumsahau moja kwa moja ila akinitafuta nitamsaidia ila sitowaza kama nina mtoto huko labda akiletwa nitamuexpose kwa DNA test .then nitacomferm kuliko kuamini kwa perception
Ngoja niconcentrate sehemu moja.
 
Hiyo mimba ya miezi nane si mbaya... question
Sababu zote tatu ulizotoa hazina maana, mara dini, mara kabila mara ananibana.... question
huonekani uko serious kabisaaa.... question
jumla ya matumizi yote ni 215,000/- mkuu umefungua ledger kabisa ya matumizi ya huyo dada? ni mtaji huo? .... question!

Its either umetunga story au you are very immature

May labda kwa jinsi ulivonielewa kwa bado sijakomaa ila mi najijua nimekomaa, na Mipango yangu ni thabiti
Documentation kwangu ni muhimu, ninalo file la nyaraka mbali mbali za Manunuzi na mambo mengine
Ninao uwezo mzuri tu wa kuhudumia lkn ndo vikwazo vidogo vidogo
Hiyo sio story ya kutunga ndo hali halisi
 
Kwanza nikupe pole kwa kuuziwa mbuzi kwenye gunia nasema hivyo kwa kuwa kama mlikutana mwezi wa august alitakiwa ajifungue mwezi mei tena sio tar za mwanzo nakusihi usiwe na papala za kukubali hicho kiumbe utalea mtoto asiye wako.Kama unataka una maswalo mengi tafadhali tutawasiliana

Kweli heee! Tulikutakana tareh 06 na 07 Mwezi w 8 2015 kajifungua tarehe 15/04/2016, mbona naona incubation period inaangukia 9 months na siku kadhaa
Ebu nidadavulie mkuu, si unajua papara za kutaka mtoto pia zinaweza kuwa zinasababisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom