Mwanamke aliyechezesha akili za scientists

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Bwana mmoja mfanyabiashara aliishi na mke wake kwa muda wa mwaka mmoja bila kufanikiwa kupata mtoto, kwa kuwa jamaa ana uwezo kidogo na yeye ndiye jicho la familia, mama mkwe na mawifi wakaanza vi maneno. Yule bwana alimpenda sana mke wake, wala hakutaka kusikiliza maneno ya ndugu, mke wake alikuwa kabisa yeye hana tatizo ila aligundua jamaa amebeba joka la kibisa.

Mke alimuomba mume wake amletee kijana mtoto wa ndugu ili apate kijana wa kumtuma, na mume wake akisafiri pia asiwe mpweke, kwa sababu jamaa alikuwa anasafiri sana kwa shughuli za biashara.

Yule bwana alikwenda kijijini kwao akaomba kijana mmoja ambae amemaliza darasa la 12 (form IV), kwa ahadi kuwa atamuendeleza na mafunzo ya VETA. Kijana alipofika nyumbani mama alikuwa anamlia timing mume wake, akitoka tu anagawa mechi kwa kijana, hakukua na mapenzi tena alimtisha yule kijana "ukimwambia mtu mambo haya utarudi kwenu".

Haikuchukua hata miezi miwili baada ya kijana kufika mama akainua mimba, mume alifurahi sana, mtoto alizaliwa. Walipofika watoto watatu, kijana alishamaliza mafunzo yake, alipata kibarua na alitafuta chumba chake akaanza maisha yake. Mama alimwambia biashara kati yao imekwisha.

Biashara za baba mwenye nyumba zilianza kwenda vibaya, na aliona huko waendako sio kuzuri, aliamua akatafute maisha Marekani. Baada ya kuwasili kule wenyeji wake walimshauri kuomba ukimbizi.

Alipofanikiwa aliwaambia watu wa uhamiaji ana mke na watoto watatu bongo. Ikabidi mama apeleke watoto ubalozi wa Marekani kwa DNA samples.

DNA zilirudi yule baba siye baba wa watoto, wanasayansi wakamuuliza hawa watoto uliwazaa na mke wako? Akajibu ndio basi wakawapa visa mama na watoto wake. Walipofika kule mama aliombwa awaeleze wanasayansi sayansi alotumia. Mama alitiririka yote! Mume alibaki ametoa macho.

Mwisho wa yote mume akasema hawa watoto tangu wanazaliwa niliwapenda kama wa kwangu na hata kuja kwangu huku ni kuwatafutia wao maisha, hawa ni watoto wangu.

Ukiomba VISA unapima DNA?
kila anaeenda Marekani anakutanishwa na scientists? au sijaelewa?

Mkuu, nimepata kulisikia hilo lakini linawahusu wakimbizi tu. Wasomali walikuwa wanatumia mwanya wa kuingiza watu nchini Sweden na mchezo umekufa baada ya utaratibu huo wa DNA.

Visa ya kawaida tu sidhani.
 
Nina mashaka na hao wanasayansi waliomizwa vichwa na hili suala kwani naona kama lipo simpo sana kwani inaonyesha dhahiri kuwa huyo mwana mama amechepuka......labda wawe wale wanasayansi wetu wanapasua watu miguu badala ya vichwa na vichwa badala ya miguu.........
 
akina Lizaboni
 
Last edited by a moderator:
Nina mashaka na hao wanasayansi waliomizwa vichwa na hili suala kwani naona kama lipo simpo sana kwani inaonyesha dhahiri kuwa huyo mwana mama amechepuka......labda wawe wale wanasayansi wetu wanapasua watu miguu badala ya vichwa na vichwa badala ya miguu.........

Mara nyingi kwa wenzetu hasa wanawake ukiwa kwenye ndoa kuchepuka ni marachache sana, kama mapenzi yamekwisha mnaelezana ukweli.
 
Unapima. Na dna test haifanyikii bongo. Sampuli zinatumwa marekani baada ya kuwa collected hapo hapo kwenye ubalozi. Tanzania inaheshimika mno kwa kufoji, lol
Ukiomba VISA unapima DNA?
kila anaeenda Marekani anakutanishwa na scientists? au sijaelewa?

Sio kwa ajili ya ukimbizi tu. Ukipata uraia kwa sababu yoyote ile na ukataka kuchukua wanao ambao haukuwazaa marekani ni lazma uthibitishwe kama kweli ni wanao.
Kwasababu alisema ni mkimbizi wa nchi nyingine, na familia yake aliiacha Tanzania alipokimbia kwao.
 
Unapima. Na dna test haifanyikii bongo. Sampuli zinatumwa marekani baada ya kuwa collected hapo hapo kwenye ubalozi. Tanzania inaheshimika mno kwa kufoji, lol

Sio kwa ajili ya ukimbizi tu. Ukipata uraia kwa sababu yoyote ile na ukataka kuchukua wanao ambao haukuwazaa marekani ni lazma uthibitishwe kama kweli ni wanao.

Duh mie nilijua wewe ukipewa uraia huko tuta foji nijifanye brother wako kumbe dah
 
Kufoji wabongo tunayaweza mno tu. Isingekuwa haya ya dna mbona ungekuwa mtoto wangu kabisa, sitti mtemvu angekupa cheti cha 15 yrs old... Huna jinsi itabidi uniwowe. Halafu nahamia pm zako kunyorosha wadada wote humu jf. Hehehehe hakuna lisilowezekana bongo.
Duh mie nilijua wewe ukipewa uraia huko tuta foji nijifanye brother wako kumbe dah
 
Hao wanasayansi walioumiza kichwa basi watakua ni wale wataalam wa miamba ya baharini.....wanafanania sana na Leprofesari mu.....go!
 
Kufoji wabongo tunayaweza mno tu. Isingekuwa haya ya dna mbona ungekuwa mtoto wangu kabisa, sitti mtemvu angekupa cheti cha 15 yrs old... Huna jinsi itabidi uniwowe. Halafu nahamia pm zako kunyorosha wadada wote humu jf. Hehehehe hakuna lisilowezekana bongo.

sounds scary lol
 
Back
Top Bottom