Mwanamke akiwezeshwa

Mwanamke akiwezeshwa

Valle jambo lolote mwanamke anaweza na mwqnaume anaweza pia

Hiyo siyo kweli kwa kila kitu.

Sijawahi kuona wala kusikia mwanamke ana au ka bench press 600 lbs.

Kama yupo, nitajie.

La sivyo kauli yako inahitaji qualification.

Unajua hata bench press ni nini?
 
Kuna kitu kinaitwa enabling environment sijui tunaweza sema mazingira wezeshi; hii inaanzia kwenye ngazi ya familia hadi jamii na taifa. Kama familia haiweki mazingira ya binti kuexprole dreams zake basi anaweza asifikie potential zake. Wakulima wengi waafrika wanalalamikia jinsi kusivyo na usawa maana wenzao wa ulaya 'wanawezeshwa'. Case ya viti maalumu imesaidia kwa kiwango fulani kupunguza ile mentality ya wanawake kutoweza na ndio maana baada ya kuonyesha uwezo wao baadhi ya wanawake wanaweza kuaminika hata kwenye majimbo yenye mila ngumu kama kanda ya ziwa hasa Mara. Sasa inategemea mtu ana maanisha nini kuhusu kuwezeshwa. Lakini kwangu mimi ingawa si neno ninalolitumia KABISA naelewa ni kutengeneza mazingira rafiki kwa wasichana na wanawake kuchangia katika uchumi, siasa na maendeleo kwa ujumla ya nchi na dunia. Kwa kuanzia juhudi za ziada zinahitajika maana hata Marekani ni miaka si zaidi ya 200 wanawake walikuwa hawapigi kura.
Nimekuelewa kwamba kwa mtazamo wako dhana "kuwezeshwa" ni kutengenezewa mazingira rafiki ili kurahisisha njia ya kufika hatua moja mbele...
 
Valle jambo lolote mwanamke anaweza na mwqnaume anaweza pia

Huu msemo ni kuwadidimiza wanawake tuu kwa maana hakuna hawezeshwa kokote suala LA maendeleo ya MTU ni yy mwenyew wapo wanawake waliofanikiwa zaid ya wanaume jiulize hao wamewezeshwa na nani ????huu msemo hauna maana kwa maisha halis tunayoishi kwa sasa.

Wanawake tukiamua tunaweza.suala LA kuweza ni ss wenyew tuwe tayar ndani ya akili zetu.tuamue kufanya jambo Fulani na kuwa na malengo juu ya hilo jambo.
Nimependa hapo "wanawake tukiamua tunaweza" na ninakubaliana na wewe kwamba tunaweza maana uwezo tunao ni kutia nia tu.

Wapo wanaume wenye mfume dume kwamba mwanamke ni mtu wa chini na mwisho wake ni majukumu ya nyumbani. Hao unawaambiaje?
 
Tunaposema mwanamke akiwezeshwa anaweza mimi kama everlenk ninachoelewa ni Kwamba siyo kwamba ni lazima abustiwe ili afanye mambo mazuri au aweze, Bali ni Kwamba mwanamke apewe Uhuru na aaminiwe katika ile nafasi anayokuwa nayo kwamba anaweza kufanya mambo kuwa Sawa.

Mwanamke asibanwe, dhana ya kwamba ni chombo dhaifu itoke ,mwanaume amuamini mwanamke kwamba hata naye ana akili na utashi Sawa km yeye alivyo,anaweza sababisha mambo kutokea,kwa kadri kila mmoja alivyopewa vipawa na mwenyezi Mungu in short ni Kwamba say no to mfumo dume. Huku ndo kuwezeshwa dunia inapokusema mwanamke apewe nafasi na aaminiwe tu mengine yote wamuachie apambane tu.
Nimekupata vema bibie,hivyo wale wanaodhani kuwezeshwa ni kushikwa mkono ama kubustiwa kwa namna yoyote waache dhana hiyo na badala yake watoe uhuru na nafasi ili kuonyesha ufanisi zaidi.
 
Tatizo fikra,ukibadili fikra na mtazamo kila kitu kinawezekana
Nakubaliana nawe kila kitu kinaanzia kwenye fikra hivyo nanyi mkituamini na kutupa nafasi na uhuru tunaweza kusababisha maendeleo makubwa tu....

Heri ya mwaka mpya,nafurahi kukuona umetoka huko pangoni
 
Si kweli kwmaba mwanamke asipowezeshwa hawezi. Ni ile dhana tu ya utegemezi na kuwezeshwa ambayo tumejiwekea hasa sisi wa Afrika ndio inayotufanya tuone kuwa mwanamke bila ya kuwezeshwa hawezi.
Inabidi hiyo dhana tuachane nayo,tuone tunaweza kufanya mambo kwa uhuru na utashi sahihi
 
Inawezekana unaingalia kauli hiyo kutoka angle ipi...Mwanzo wa kauli hiyo haikuwa na maana ya kuwadhalilisha kina mama ilikuwa ni kampeni dhidi ya wanawake....Kwa maana ya mwanamke akiwezeshwa anaweza hasa katika nyanja za kisiasa zamani kulikuwa hamna uwiano kati ya wanawake na wanaume katika nafasi mbalimbali na hao wachache waliojaribiwa kupewa nafasi hizo walifanya vizur ndo ukaja huo usemi wa mwanamke akiwezeshwa atawezana yakajitokeza mashirika kama women empowerment.....Ila nadhani mmewezeshwa hadi mnakaribia kutupita wanaume nadhani inahitajika jitihada za makusudi za kuwarudisha nyuma...Hakika.
Ha haa kuturudisha nyuma tena jamani! Tunaweza na hakika tunaweza
 
Kama ni demu sikilizaa...

Kama una swali ulizaa...

Hata kama sijamalizaa aaaaaa sikilizaaa...
 
Nyie hamjaelewa maana ya mwanamke akiwezeshwa. Nadhani mmeelewa vibaya ,
 
Katika slogan mbaya kuwahi kutumika, basi hii ni mojawapo. "Mwanamke akiwezeshwa anaweza", maana nyingine ni kuwa, "Mwanamke asipowezeshwa hawezi"

Ni kweli akiwezeshwa anaweza.
Kuna jamii ziliamini mwanamke hawezi ndio maana hata hakupelekwa shule.

Lakini imethibitisha kua wakiwezeshwa wanaweza. Kwa maana akipewa nafasi ya kusoma anaweza kufanya vizuri (utajuaje uwezo wake darasani na atatokaje kitaaluma bila 'kupelekwa ' shule?

Kwenye nafasi za uongozi akiwezeshwa pia anaweza. Kama msipompa nafasi mtaonaje uwezo wake?

Kupewa nafasi ndio kuwezeshwa. Ina maana walikua wanawezeshwa wanaume tu, wanawake hawakupewa nafasi.

Sasahivi kwenye elimu tunaenda vizuri bado kwenye uongozi na tatizo na fikra mgando.

Narudia... KUWEZESHWA NI KUPEWA NAFASI/FURSA.
 
anzisheni kampeni ya kupinga ''mkiwezeshwa mnaweza'' mje na mwanamke anaweza.....na muache kuomba omba vocha...

Atawezaje bila kuwezeshwa?
Hata mwanaume akiwezeshwa ndio ataweza, kumbuka kampeni za Urais hao wanaume wenyewe walikua na wawezeshaji ili kufanikisha.

Kuweshwa ni kujengewa uwezo ili kufikia malengo.
 
Nakubaliana nawe kila kitu kinaanzia kwenye fikra hivyo nanyi mkituamini na kutupa nafasi na uhuru tunaweza kusababisha maendeleo makubwa tu....

Heri ya mwaka mpya,nafurahi kukuona umetoka huko pangoni


Nawe pia hero ya mwaka mpya my long time mchepuko,the issue is siyo sisi wa kuwapa nafasi but ni nyie wenyewe kuwa kufanya uamuzi wa kuweza.asilimia kubwa ya wadada wana ile mentality kwamba kuna mtu lazima awafanyie kitu flani.mfano mdada hajishughulishi kutafuta pesa but anawaza lazima apewe na boyfriend.mfano mzuri ni hawa dada zako masupa star wa bongo,wanaishi cosmetic life,yaani kila mmoja anajiona yuko juu but in real sense she got nothing.hatafuti anasubiri leo ahongwe hiki,kesho ananyang'anywa etc,hachukui step kutafuta vyake,mawazo yake ni lini ampate kozo okamoto ili amuweke mjini,afikirii age inaenda na after 10yrs atakuwa 35 or beyond sasa nani atamtaka tena wakati hapa mujini vidada vinachepukia kila leo.where will they stand after 20yrs?vingine vidogo hata 25yrs havina hata form 2 havikufika sasa una imagine vitakuwa na future ua aina gani?

N'way you guys,you ladies have to free your mentality otherwise ever mtasubiri na hizo fikra za mtu aje kuwawezesha ndo muweze
 
Nini tafsiri ya neno kuwezeshwa kwako?
Binti yako usipompeleka shule unadhani ataonesha wapi uwezo wake kielimu (kwa wanaoamini elimu ya darasani)

Hukumuwezesha mwanao kwenda shule ataonesha wapi uwezo wake kitaalam?

Binti yako hukumjengea uwezo wa kujiamini kua anaweza tangu nyumbani utawezaje kusema mwanangu ni kiongozi mzuri?

Hata kumpa mtaji au kumshirikisha kwenye biashara zako huwezi, atawezaje?

Hata watoto wa kiume wazibie fursa uone kama kuna watakachoweza.

Hiyo kauli ilikua kwa ajili ya kuwahamasisha wazazi na jamii kuwapa fursa mabinti.


kuwezeshwa kimsingi wa familia kunafanyika kwa wote,wakiume na like.kama ni elimu,biashara etc but why you guys think need special antention?
 
Bila shaka mko vema na mwaendelea vema na majukumu yenu ya hapa na pale. Kwa wagonjwa ama mafadhaiko mbalimbali tunawaombea hali zirudi kua sawa....

Nisiandike mengi sana ya kuwachosha niende moja kwa moja kwenye swali langu ambalo leo nimekua interesting nalo japo hua nalisikia na limezungumzwa sana ila kwaleo nimependa kusikia kwa undani wake zaidi...

Kuna ule msemo kwamba "mwanamke akiwezeshwa anaweza"

Swali langu hapo ni kuwezeshwa kwa namna gani huko kunakozungumziwa? Ina maana pasipo kuwezeshwa ndio hatuwezi kabisa au mambo yataenda taratibu ama tutabweteka? Mimi sijui zaidi ila naomba mnifafanulie hapo.

Wanawake wenzangu hebu njooni tusemezane hili,ni kweli pasipo kuwezeshwa hatuwezi? Hatuwezi kusimama hata kidogo peke yetu bila upande wa pili kuwepo kutushika mkono?

Munkari, ICHANA, Apologise lady, Everline lank, Madame B, Blue G, sweet lady, Heaven Sent,na wengineo

Wanaume nanyi karibuni mtuambie nini mtazamo wenu katika hili?
Kataeni viti maalum... hakika hii kauli itatokomea.

Swali ni kwamba.... mtakubal;i??

Kitu kingine.... mwanamke asipowezeshwa atapata mimba??
 
Kataeni viti maalum... hakika hii kauli itatokomea.

Swali ni kwamba.... mtakubal;i??

Kitu kingine.... mwanamke asipowezeshwa atapata mimba??
Hahahahhaah shemeji langu hiloooo ........duhhh na mwanaume asipowezesha atampa nani mimba???????
 
Back
Top Bottom