Mwanamke akiwezeshwa

Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
24,685
28,769
Bila shaka mko vema na mwaendelea vema na majukumu yenu ya hapa na pale. Kwa wagonjwa ama mafadhaiko mbalimbali tunawaombea hali zirudi kua sawa....

Nisiandike mengi sana ya kuwachosha niende moja kwa moja kwenye swali langu ambalo leo nimekua interesting nalo japo hua nalisikia na limezungumzwa sana ila kwaleo nimependa kusikia kwa undani wake zaidi...

Kuna ule msemo kwamba "mwanamke akiwezeshwa anaweza"

Swali langu hapo ni kuwezeshwa kwa namna gani huko kunakozungumziwa? Ina maana pasipo kuwezeshwa ndio hatuwezi kabisa au mambo yataenda taratibu ama tutabweteka? Mimi sijui zaidi ila naomba mnifafanulie hapo.

Wanawake wenzangu hebu njooni tusemezane hili,ni kweli pasipo kuwezeshwa hatuwezi? Hatuwezi kusimama hata kidogo peke yetu bila upande wa pili kuwepo kutushika mkono?

Munkari, ICHANA, Apologise lady, Everline lank, Madame B, Blue G, sweet lady, Heaven Sent,na wengineo

Wanaume nanyi karibuni mtuambie nini mtazamo wenu katika hili?
 
Valentina asante, umefanikiwa kunitoa machimboni.

Hakuna suala la kuwezeshwa kwa mwanamke, mwanamke kama mwanamke anao utashi sawa na mwanaume kiasi kwamba anao uwezo wakusimamia mambo yake hata zaidi ya wanaume, suala la kusema hadi tuwezeshwe ndio tuna weza ni hoja dhaifu na haina mashiko katika katika dunia hii ya sasa kwasababu, wanawake tunauwezo na nguvu, maarifa nk. Angalia katika elimu je ni mabinti wangapi wanafanya vizuri je wameweze na nani ili hali masomo, walimu na mitihan vyote wanashiriki pamoja??

Pia hata maofisin kuna wanaume wangapi ni mizigo ili hali akina mama wanasimamia ofisi kwa ustadi mkubwa, je wamewezeshwa na nani???

Pia kuna wanawake wangapi wanaendesha maisha na kutafuta maisha na wameweza kuliko hata wanaume, je wamewezeshwa na nani???

ifahamike wazi dhana ya ufemisti ndio iliyomfungua mwanamke na kumfanya ajitambue kuwa anauwezo sawa sawa na binadamu mwingine. Na ni kweli mwanamke anaweza yeye kama yeye hakuna suala la kuwezeshwa, ikiwa mtu anasema lazima tuwezeshwe anapaswa kutoa ushahdi yeye amewazesha wangapi katika nyanja ipi.
 
Wako wanaoamini kwamba mwanamke akifanikiwa kufika juu/kuweza/kuwezeshwa basi anaota mapembe kwakuonyesha dharau za wazi kwa wanaume. Hili unalionaje kwa upande wako?
 
Katika slogan mbaya kuwahi kutumika, basi hii ni mojawapo. "Mwanamke akiwezeshwa anaweza", maana nyingine ni kuwa, "Mwanamke asipowezeshwa hawezi"
 
Huwa naita inferiority complex, kuna wakati binadamu kaumbwa kuhamaki bila sababu hasa anapoona kazidiwa jambo fulan na mwanamke, hawezi kukubali matokeo atatafuta sababu ili tu kutaka kujaribu kumshusha katika level aliyokuwepo. wengi wao hudai mwanamke akifanikiwa anakuwa jeuri, hataki kushindwa nk, huwa najiuliza je hawa watu katika familia zao jinsi ya kike wote hawajafanikiwa au?? Maana wapo ambao wakiona mwanamke kafanikiwa hawaishi kusema, anajiuza, anategemea kuhongwa nk muulize ushawah kumuhonga? Au ashawah kukuuzia anabaki anajikanyaga.

Suala kubwa hapo ni inferiority complex na hakuna jambo lingine.

Lakin wapo wengine wanachukulia kawaida mafanikio ya mwanamke na wanasupport kubwa sana hasa ya mawazo ambazo huweza kumsaidia mwanamke kufikia malengo yao, "hao ni wanaume wa kweli"
 
Kuna kitu kinaitwa enabling environment sijui tunaweza sema mazingira wezeshi; hii inaanzia kwenye ngazi ya familia hadi jamii na taifa. Kama familia haiweki mazingira ya binti kuexprole dreams zake basi anaweza asifikie potential zake. Wakulima wengi waafrika wanalalamikia jinsi kusivyo na usawa maana wenzao wa ulaya 'wanawezeshwa'. Case ya viti maalumu imesaidia kwa kiwango fulani kupunguza ile mentality ya wanawake kutoweza na ndio maana baada ya kuonyesha uwezo wao baadhi ya wanawake wanaweza kuaminika hata kwenye majimbo yenye mila ngumu kama kanda ya ziwa hasa Mara. Sasa inategemea mtu ana maanisha nini kuhusu kuwezeshwa. Lakini kwangu mimi ingawa si neno ninalolitumia KABISA naelewa ni kutengeneza mazingira rafiki kwa wasichana na wanawake kuchangia katika uchumi, siasa na maendeleo kwa ujumla ya nchi na dunia. Kwa kuanzia juhudi za ziada zinahitajika maana hata Marekani ni miaka si zaidi ya 200 wanawake walikuwa hawapigi kura.
 
Valle jambo lolote mwanamke anaweza na mwqnaume anaweza pia

Huu msemo ni kuwadidimiza wanawake tuu kwa maana hakuna hawezeshwa kokote suala LA maendeleo ya MTU ni yy mwenyew wapo wanawake waliofanikiwa zaid ya wanaume jiulize hao wamewezeshwa na nani ????huu msemo hauna maana kwa maisha halis tunayoishi kwa sasa.

Wanawake tukiamua tunaweza.suala LA kuweza ni ss wenyew tuwe tayar ndani ya akili zetu.tuamue kufanya jambo Fulani na kuwa na malengo juu ya hilo jambo.
 
Tunaposema mwanamke akiwezeshwa anaweza mimi kama everlenk ninachoelewa ni Kwamba siyo kwamba ni lazima abustiwe ili afanye mambo mazuri au aweze, Bali ni Kwamba mwanamke apewe Uhuru na aaminiwe katika ile nafasi anayokuwa nayo kwamba anaweza kufanya mambo kuwa Sawa.

Mwanamke asibanwe, dhana ya kwamba ni chombo dhaifu itoke ,mwanaume amuamini mwanamke kwamba hata naye ana akili na utashi Sawa km yeye alivyo,anaweza sababisha mambo kutokea,kwa kadri kila mmoja alivyopewa vipawa na mwenyezi Mungu in short ni Kwamba say no to mfumo dume. Huku ndo kuwezeshwa dunia inapokusema mwanamke apewe nafasi na aaminiwe tu mengine yote wamuachie apambane tu.
 
Last edited:
Bila shaka mko vema na mwaendelea vema na majukumu yenu ya hapa na pale. Kwa wagonjwa ama mafadhaiko mbalimbali tunawaombea hali zirudi kua sawa....

Nisiandike mengi sana ya kuwachosha niende moja kwa moja kwenye swali langu ambalo leo nimekua interesting nalo japo hua nalisikia na limezungumzwa sana ila kwaleo nimependa kusikia kwa undani wake zaidi...

Kuna ule msemo kwamba "mwanamke akiwezeshwa anaweza"

Swali langu hapo ni kuwezeshwa kwa namna gani huko kunakozungumziwa? Ina maana pasipo kuwezeshwa ndio hatuwezi kabisa au mambo yataenda taratibu ama tutabweteka? Mimi sijui zaidi ila naomba mnifafanulie hapo.

Wanawake wenzangu hebu njooni tusemezane hili,ni kweli pasipo kuwezeshwa hatuwezi? Hatuwezi kusimama hata kidogo peke yetu bila upande wa pili kuwepo kutushika mkono?

Munkari, ICHANA, Apologise lady, Everline lank, Madame B, Blue G, sweet lady, Heaven Sent,na wengineo

Wanaume nanyi karibuni mtuambie nini mtazamo wenu katika hili?

Si kweli kwmaba mwanamke asipowezeshwa hawezi. Ni ile dhana tu ya utegemezi na kuwezeshwa ambayo tumejiwekea hasa sisi wa Afrika ndio inayotufanya tuone kuwa mwanamke bila ya kuwezeshwa hawezi.
 
Inawezekana unaingalia kauli hiyo kutoka angle ipi...Mwanzo wa kauli hiyo haikuwa na maana ya kuwadhalilisha kina mama ilikuwa ni kampeni dhidi ya wanawake....Kwa maana ya mwanamke akiwezeshwa anaweza hasa katika nyanja za kisiasa zamani kulikuwa hamna uwiano kati ya wanawake na wanaume katika nafasi mbalimbali na hao wachache waliojaribiwa kupewa nafasi hizo walifanya vizur ndo ukaja huo usemi wa mwanamke akiwezeshwa atawezana yakajitokeza mashirika kama women empowerment.....Ila nadhani mmewezeshwa hadi mnakaribia kutupita wanaume nadhani inahitajika jitihada za makusudi za kuwarudisha nyuma...Hakika.
 
walitaka kuwezeshwa wakawezeshwa wakawezesheka sasa viburi juu
 
Mbona liko wazi kabisa.. "mwanamke akiwezeshwa anaweza".
 
Kiuhalisia wanawake wengi wa kiafrika ni mpaka wawezeshwe hii inatokana na kutokujiamini(fikra),mila...nk
Lakini pia kuna wanawake wa shoka ambao hawaitaji support wala escort wanajituma na kujiamini pia
 
anzisheni kampeni ya kupinga ''mkiwezeshwa mnaweza'' mje na mwanamke anaweza.....na muache kuomba omba vocha...
 
Katika slogan mbaya kuwahi kutumika, basi hii ni mojawapo. "Mwanamke akiwezeshwa anaweza", maana nyingine ni kuwa, "Mwanamke asipowezeshwa hawezi"
Unakubali kwamba wanawake tunaweza hata pasipo ninyi?
 
Huwa naita inferiority complex, kuna wakati binadamu kaumbwa kuhamaki bila sababu hasa anapoona kazidiwa jambo fulan na mwanamke, hawezi kukubali matokeo atatafuta sababu ili tu kutaka kujaribu kumshusha katika level aliyokuwepo. wengi wao hudai mwanamke akifanikiwa anakuwa jeuri, hataki kushindwa nk, huwa najiuliza je hawa watu katika familia zao jinsi ya kike wote hawajafanikiwa au?? Maana wapo ambao wakiona mwanamke kafanikiwa hawaishi kusema, anajiuza, anategemea kuhongwa nk muulize ushawah kumuhonga? Au ashawah kukuuzia anabaki anajikanyaga.

Suala kubwa hapo ni inferiority complex na hakuna jambo lingine.

Lakin wapo wengine wanachukulia kawaida mafanikio ya mwanamke na wanasupport kubwa sana hasa ya mawazo ambazo huweza kumsaidia mwanamke kufikia malengo yao, "hao ni wanaume wa kweli"
Umenena vema kabisa bibie natamani wote wenye mawazo hasi wabadili fikra zao....
 
Back
Top Bottom