Mwanamke akiwezeshwa

Mwanamke akiwezeshwa

Hahahahhaah shemeji langu hiloooo ........duhhh na mwanaume asipowezesha atampa nani mimba???????
Mwanaume anajiwezesha kwa kulipa mahari...

Afu shem nasikia juzi ulinigeuka..... sio vizuri hivo...
 
Mwanaume anajiwezesha kwa kulipa mahari...

Afu shem nasikia juzi ulinigeuka..... sio vizuri hivo...
Siku hizi mahari tunawalipia....

Shem sijakugeuka bana nilikuwa nachangamsha wadau tu........
 
Mwanamke ni kiumbe mwenye akili na ufahamu wa hali ya juu sana....na ana misimamo mikali sana kwa kile anachokiamini kuwa ni sahihi kwake.....

Kitu pekee alichokikosa mwanamke katika neema hizo ni maarifa na utashi wa kusimamia vile ambavyo ni sahihi....mara nyingi sana wanawake huwekeza misimamo ,utashi na ufahamu wao katika mambo yasiyo na faida kwao....

Na ndio sababu kubwa mwanamke anatakiwa apate kiongozi kwa ajili ya kumsimamia katika mambo au mstari ulionyooka......

Kitu kikubwa kinachowafanya wanawake wasione umuhimu wa kuwa na viongozi wao ambao ni wanaime ni kwamba wengi wao wanaangukia katika mikono ya wavulana au vijana wa kiume waliokiwa katika kipindi cha balehe ambao mara nyingi wanaume hao au wavulana wao wenyewe hawawezi kujiongoza...hivyo wanakosa uhalali wa kumuongoza kiumbe mwingine......

Kuna namna nyingi sana za kumuwezesha mwanamke lakini kwa nyakati hizi ambazo wanawake wamepiga hatua ni jambo dogo tu la kumuwezesha kimawazo na kumjaza mitazamo chanya juu ya hali mbali za kimaisha.....
 
Mfumo wa maisha kwa muda mrefu umemnyima mwanamke fursa nyingi. mojawapo umiliki wa mali na mamlaka. pia uwezo wa kuamua au hata ushiriki. kumwezesha mwanamke maana yake ni kumpanafasi katika hayo na mengine.
 
mfano mwanamke anatendwa na mwanamume anamtenda. mfano mwanamume anaoa mwanamke anaolewa. mwanamke anaamuliwa huku mwamuzi ni mwanamume. mwanamke hakuhitaji hata elimu bali mwanamume kwa sababu hapangi bali kupangiwa. kwa hiyo kumwezesha mwanamke ni kuondoa vikwazo hivyo.
 
Mimi naona ni kauli mbiu ambayo ni tata. Hao walioitunga ndio wenye majibu kamili ya nini walikusudia au kumaanisha.
 
Umenena vema kabisa bibie natamani wote wenye mawazo hasi wabadili fikra zao....
mwanamke hashindwi kitu, hata bila kuwezeshwa mwanamke anaweza. waangalieni wanavyoteseka kwa malezi ya watoto huku wakiwa wametopea kwenye dimbwi la umasikini tena wakiwa hawana wanaume. Ukiliangalia hilo tu nikubwa kuliko haya mengine tunayoongelea. ni wangapi wamelelewa na mwanamke katika mazingira magumu tena bila msaada wa baba na ndugu...mbona alisimama mpaka ww ukakua na kusoma? Hilo tu linaweza kutupa majibu ya Swali lako mpendwa valentine
 
mwanamke hashindwi kitu, hata bila kuwezeshwa mwanamke anaweza. waangalieni wanavyoteseka kwa malezi ya watoto huku wakiwa wametopea kwenye dimbwi la umasikini tena wakiwa hawana wanaume. Ukiliangalia hilo tu nikubwa kuliko haya mengine tunayoongelea. ni wangapi wamelelewa na mwanamke katika mazingira magumu tena bila msaada wa baba na ndugu...mbona alisimama mpaka ww ukakua na kusoma? Hilo tu linaweza kutupa majibu ya Swali lako mpendwa valentine
Dah.. Na hili hasa ndiyo jambo kuu kwa mwanamke.. Ameumbwa kwa ajili hii
 
kuwezeshwa ni fikra mgando! binadamu yoyote akichapa kazi akaahirikisha ubongo wake vilivyo na anakuwa super bila kujali jinsia.

wanawake wako makini sana naturally wakiamua kufanya jambo la kiuchumi nashangaaa wanaojiinamia kama kobe kusubir wapewe na nani cjui umasikin na utegemezi wakujitakia huo
 
Unakubali kwamba wanawake tunaweza hata pasipo ninyi?
Ingawa umemwuliza mwingine, ngoja mimi nikujibu, 'NDIYO'. Nimefuatilia mjadala, wachangiaji wengi ambao ni akina mama, wameeleza vizuri tu, kumuwezesha mama sio kumjaza mapesa mifukoni bali ni kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili mwanamke atumie fursa zilizopo. Katika maisha ya kila siku mazingira wezeshi hata yakiwekwa yanawanufaisha wanawake wa hali za juu (high class) na si akina mama wa wakawaida. Hata hivyo, ingawa akina mama wa hali za chini hawanufaiki moja kwa moja na mazingira wezeshi wanayopewa wanawake bado akina mama hao kwa ubunifu wao, uthubutu na bidii zao binafsi bila kutoka kwa wanaume wameweza kumudu maisha kwa kiwango chao na kutunza familia akiwemo baba mweneyewe. Utaona kuna biashara za kufunga maji na kuuza, kupika maandazi, mamalishe,kilimo cha mboga mboga, ufugaji kuku, kupika pombe za kienyeji n.k. Niseme tunapojadili akina mama kuweza si lazima wawe ni wale wa level ya juu, tukumbuke waliopo pia level ya chini ambao ndio wengi.
 
Back
Top Bottom