Mwanamke akiri kujihusisha na ushirikina.

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
*Adai kuangusha magari 15, auwa watu 15 mpaka sasa.
*Aonesha ngozi ya mtoto wa miaka miwili.

Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Belikumana Lugome(48), Mkazi wa Kijiji cha Parangu Songea Mkoani Ruvuma amekiri kujihusisha na imani za kishirikina na kukabidhi sehemu ya madawa aliyokuwa akiyatumia kwa Mganga wa Jadi aliyefahamika kwa jina la Jesca Ndembo Mkazi wa Iyunga Mkoani Mbeya. Mwanamke huyo alifika kwa Mganga huyo wa jadi Oktoba 12 mwaka huu, majira ya saa 8 mchana alipokwenda hapo kwa nia ya kumwangalia shangazi yake aliyekuwa akitibiwa na Mganga huyo. Aidha imedaiwa kuwa shangazi yake huyo alirogwa na nduguye na mshirikina huyo kukiri kwamba ndiye alisababisha upasuaji wa tumbo lake mara mbili na kutakiwa apasuliwe tena na kama asingewahi angeuawa kwa siku za hivi karibuni. Bi. Lugome amekiri kujihusisha na matukio ya ajali 15 mkoani Ruvuma na kusababisha vifo vya watu 15 katika ajali hizo. Aidha alionesha sehemu ya vifaa ambavyo alikuwa akivitumia katika ushirikina ikiwemo ngozi ya mtoto wa miaka miwili. Hata hivyo amesema kuwa yeye aliupata uchawi huo kutoka kwa Waganga mbalimbali Mkoani Ruvuma na kwamba hapendi hali hiyo kwani haina faida yoyote.
 
akamatwe na kufunguliwa kosa la mauaji ya watoto aliokutwa na ngozi zao.
 
Kama wabunge, mawaziri n.k. nao ni watu wa ndumba itakuwaje kwa watanzania hawa masikini? Tuna safari ndefu sana kujikomboa.
 
Wangoni kwa ushirikina Songea si ndiko wakoenda kumloga hata yule waziri wa mawasiliano a.k.a mtaalam wa Richmond
 
Uongo mtupu. Huyu anataka kummsadia huyo mganga apate biashara kwa kuaminiwa kuwa anaweza kuwabaini wachawi na wakatupa uchawi. Unaweza kukuta hiyo ngozi si ya mtoto, bali ni ya nyani au mnyama wa aina yoyote. Mbinu za hawa waganga ni nyingi. Mmesahau wale waliokuwa wanapandishana kwenye mapaa ya nyumba na kujifanya eti wamenaswa na "antena" za waganga? Utapeli tu huu. Tuache ujinga!
 
Kama wabunge, mawaziri n.k. nao ni watu wa ndumba itakuwaje kwa watanzania hawa masikini? Tuna safari ndefu sana kujikomboa.

Umeona eeenh! Wanaounda serikali ni washirikina lakini serikali haitambui huo ushirikina. So strange! Bora wamhukumu kwa mauaji na si huo ushirikina
 
Gari 15 watu 15 uongo tena mkubwa hebu atueleze alikuwa anadondosha aje

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
kweli ufalme wa shetani ni fitna.....eti shetani (mchawi) akijiumbue kwa shetani (mganga) na kujifanya eti hataki tena.....!! hataki tena maneno haya anayasema kwa mganga??????? non sense

mix with yours
 
Shtaka analoweza kushtakiwa nalo ni kupatikana na viungo vya binadamu maana itakuwa ngumu kuthibitisha kosa la mauaji ya mtoto, standard ya proof iko juu sana. Wapelelezi mkamateni na ashughulikiwe ipasavyo.
 
Back
Top Bottom