Mwanamfalme wa Saudi Arabia afariki katika ajali ya ndege

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mwanamfalme mmoja nchini Saudi Arabia amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri pamoja na maafisa kadha wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, runinga ya Al-Ikhbariya imesema.

Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika.
Saudi Arabia ilisema ilitungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi.

Pia, wikendi, watu wengi wakiwemo wana wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.

Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi Mohammed bin Salman. Mwanamfalme Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanamfalme aliyekuwa wa kwanza katika urithi awali.

Babake, Muqrin bin Abdul Aziz, alitengwa na ndugu wa kambo wa Mfalme Salman miezi kadha baada yake kurithi ufalme mwaka 2015. Shirika la habari la Okaz limesema taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema hakukuwa na manusura kwenye ajali hiyo ya ndege.

BBC
 
karibu na mpaka wa Yemen ndege nyingi hukwepa mpaka wa Yemen imekuwaje wakakatiza pande hizo!!?
 
karibu na mpaka wa Yemen ndege nyingi hukwepa mpaka wa Yemen imekuwaje wakakatiza pande hizo!!?
Hata mimi nimeshangaa sana. Kwa mfano Etihad au Emirates ambazo zinafahamika ni za kiraia perse zikitoka Dar huambaa ambaa pwani kutokezea kwenye pembe ya Afrika (horn of Africa) then zinaikwepa kabisa Yemen kwa kujichimbia baharini zaidi then zinaingilia Oman and finally UAE. Yemen haziingizi pua kabisa sembuse hilo helikopta binafsi ambalo wasingeweza kujua lengo la kukatiza huko ni lipi na ukute hata HELLO message halikutuma au kujibu. Hata mimi ningekuwa ndiye kamanda wa kikosi wala nisingefikiria mara mbili; amri ni moja tu lawama baadaye no matter ndani kuna nani.
 
Labda mwana mfalme aliye mbioni kukaimu madaraka kaamua amrestishe in peace.
Maana kawakamata ndugu na viongozi wengi, katika kile kinachoonekana ni kupunguza nguvu zao na kujiimarisha.
Kawakata matajiri ambao wanapingana na sera zake.
Tumeshuhudia waziri mkuu wa Lebanon kujiuzuru, wachambuzi wanadai ni plan ya mwana mfalme maana Saudia ndiye mdhamini wa huyu waziri aliyejiuzuru.
Operation zake za vita huko yemen hazijazaa matunda na kila siku Saudia inaingia gharama kubwa kwasababu ya hiyo vita.
Hapa wanagombea madaraka hakuna kingine
 
Umeona nlipoona. Apo kachezewa mtu. Saudi saiv kunafutuka within the government
 
Houthi wamekataa hawausiki, na pia amna missile iliyokua detected na satellite za saudi
Hata wangehusika sitegemei wakubali, na nchi nyingi zikitunguliwa ndege zake huwa zinaficha na kutaka kusemani ajali ili kuondoa embarassement.

Pia, Wa Saudi wanavyofanyiziana wenyewe kwa wenyewe familia ya kifalme siwezi kushangaa kama wanalipuana wenyewe kwa wenyewe.

Just plausible theories.
 
na kwanini wakatae ujiko, juzi walirusha LRBM likadakwa mbona wakakubali kwamba ni wao, rumor has it, prince moh'd kafanya mchezo mchafu
 
na kwanini wakatae ujiko, juzi walirusha LRBM likadakwa mbona wakakubali kwamba ni wao, rumor has it, prince moh'd kafanya mchezo mchafu
Inawezekana mtu akakataa ujiko kwa sababu kushambulia ndege ya kiraia unaweza kufunguliwa mashataka ICC, kupiga targets za kijeshi unaweza kusema ni vita.

Kama nilivyosema awali, inawezekana pia Princes wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe, sasa hivi habari kubwa ni kwamba Crown Prince kawafunga wenzake kibao kwa tuhuma za rushwa,while habari za rushwa hazijulikani vizuri,inajulikana hawa wana wafalme wa Saudi wana beef zao za kugombea madaraka.

Anayevuma kuua ndugu zake Kim Jong Un, kumbe wa Saudi nao inawezekana wamo.

Saudi Crown Prince’s Mass Purge Upends a Longstanding System
 
Wamemtoa wenyewe wasaudi,hujui kunafukuta moto kwenye utawala wa kifalme.Dogo akijua humpendi tu anakutoa.
 
Back
Top Bottom