MwanaJF mwenzetu kavamiwa na wezi na kukatwa katwa Mapanga

Pole mkuu MOTOCHINI Nimevutiwa na ujasiri wa kupanga na na hao wezi hadi kufanikiwa kuua mmoja. Hongera na pole nyingi sana.
 
Last edited by a moderator:
Binafsi naona sahihi kabisa ulivyomuua huyo mshenzi. Naapa hata ningelikuwa mimi ningewaua wote kama ningekuwa na fursa (I mean this).

Kiukweli mtu ambae yupo tayari kudhuru mtu mwingine kwa sababu ya kupata mali kwangu mimi simuchukulii kama ni binadamu...namuona ni zaidi ya shetani na ndio maana uwa natamani sana kuwaua watu wa aina hii.
 
Mkuu hivi unadhani kuua ni jambo rahisi rahisi tu ?? hasa unapopigwa counter attack??

Btw, tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumnusuru huyu ndugu yetu.

Mimi ndugu zangu walishawahi kutembezewa nondo na vibaka zaidi ya 10 usiku wa saa nane wakiwa kati kati ya usingizi mzito!

Kuna umuhimu angalau wa kulala na silaha za jadi ndani kama hatuwezi kumiliki silaha. Hapa angalau tutaweza kujisaidia kwa kiasi fulani.

Pole sana mkuu Moto chini kwa matatizo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu pole sana kwa tukio lililokukuta pia nitumie nafasi hii kukupongeza kwa kuondoa uhai wa hilo LIIBILISI lililotaka kukudhuru....kwenye hili nakupa pongezi sana! Maana usingeliua nani anajua huenda angefanya madhambi ya kudhuru wanadamu wengine.

Pamoja na yote haya nafahamu kwa kiasi fulani tukio hili litakuwa limekurudisha nyuma. Hivyo kama member wa JF napenda ufahamu tupo pamoja kwenye hili na kama utahitaji msaada wowote tafadhali usisite kuniarifu.

Nakutakia upone haraka mkuu.
 
very sad, ikiwa kuna hitajika msaada zaidi ni vyema tujuzwe lkn pia akirudi abadili ID maaana tumeshamjua
 
Aisee...!!!
Pole sana, inatisha na inasikitisha.
Mungu anajua, akusamehe na akusaidie upone haraka.
 
Pole sana MOTOCHINI. Ni kweli Don't Trust the Society to Protect you and your Family. Police wanakuja baada ya Wahalifu kukimbia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom