Mzee makoti

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
3,146
4,007
Hali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti ya Nandi Nchini Kenya baada ya Mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Kenya (KDF) kumkata sehemu za siri kisha kumuua Kasisi wa Kanisa la ACK baada ya kumfumania akifanya mapenzi na Mkewe juu ya kitanda cha Mwanajeshi huyo.

Askari huyo alipewa taarifa za siri na Wasamaria wema kuhusu Mkewe ambaye ni Mama Mshirika na pia ni Kiongozi wa Kanisa hilo kuchepuka na Kasisi huyo aliyetambulishwa kwa jina Rev Kime ndipo alipoamua kumvizia nyumbani kwake ambapo alirejea nyumbani kimyakimya usiku bila kumpa taarifa Mkewe na akaingia katika chumba kimoja bila ya Mkewe kujua ili kuthibitisha taarifa hizo.

Baada ya muda kidogo akaingia chumbani kwake na kumfumania Mtumishi huyo wa Mungu mwenye umri wa miaka 43 katika kitanda chake na Mke wake ndipo alipochukua uamuzi wa kumchoma na kitu chenye ncha kali mgongoni na kumkata sehemu zake za siri na kisha Askari huyo akatoweka kusikojulikana na Mkewe ambaye amejeruhiwa hajulikani alipo.

Majirani wameuambia mtandao wa The Star kuwa kabla ya kumuua Mchepuko wa Mkewe, Askari huyo alimfunga Mkewe kwenye kona ya nyumba ili amshuhudie wakati akimuua Mchepuko wake huyo ambapo ripoti zinasema Kasisi huyo alikuwa akisafiri KM 30 hadi kwa Mwanamke huyo na kufanya nae ngono pale Mumewe anapokuwa kwenye kazi zake za ulinzi wa Nchi.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nandi Dickens Njogu amesema “Ilikuwa tu asubuhi ya leo wakati Mkuu wa Kanisa kuu la St. Barnabas Mchungaji Nillah Bassy alipotoa ripoti rasmi ya tukio hilo la kusikitisha sana ambalo Maafisa wa Polisi walikwenda kushuhudia”

Ripoti zimesema baada ya tukio hilo Majirani walimpeleka Mchungaji huyo Rev Kemei katika Hospitali ya Kapsabet Level 5 akiwa katika hali ya umahututi na baadaye alipelekwa Eldoret na kisha akapelekwa Hospitali ya Top Hill ambako alifia akiendelea na matibabu.

Millard Ayo
 
Ipitishwe sheria kuwa kila mwanamume anayemfumania mkewe akiwa katika chumba chake basi adhibitiwe tu lakini asiadhibiwe. Hiyo ni iwapo atamjeruhi vibaya huyo mgoni wake au hata akiweza kumuua.

Sheria hii itafanya kazi kubwa kuwazuia wanaume kuwanyemelea wake za watu.Itafanya kazi kuliko ile sheria ya miaka 30 jela.
 
Kwa mwanaume mwenye akili, tatizo sio huyo mwanaume, ni mwanamke.

Kama anapata ujasiri wa kuleta mwanaume hadi kwenye kitanda chako basi mwanamke amekudharau sana.

Ila na huyo mshikaji ana kosa moja la ujinga uliopitiliza, hata kama mwanamke atakuhakikishia vipi kwamba amemshika mumewe usiende kwake kumtafunia kwake.
 
Ipitishwe sheria kuwa kila mwanamume anayemfumania mkewe akiwa katika chumba chake basi adhibitiwe tu lakini asiadhibiwe.Hiyo ni iwapo atamjeruhi vibaya huyo mgoni wake au hata akiweza kumuua.
Sheria hii itafanya kazi kubwa kuwazuia wanaume kuwanyemelea wake za watu.Itafanya kazi kuliko ile sheria ya miaka 30 jela.
Kabisa.

Huyo mgoni ahesabiwe kama jambazi aliyevamia na kushirikiana na jambazi la ndani kuidhuru familia. Mvamiwa anapojihami na kuua (ma)jambazi asihesabiwe hatia.

Yaani mwanamke anayethubutu kuleta bwana kitandani kwako hata kukuua ni suala la muda tu na maamuzi ya mume mwenzio. Mwamba akiagiza uuawe ni chap sana unakula sumu.
 
K
Hali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti ya Nandi Nchini Kenya baada ya Mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Kenya (KDF) kumkata sehemu za siri kisha kumuua Kasisi wa Kanisa la ACK baada ya kumfumania akifanya mapenzi na Mkewe juu ya kitanda cha Mwanajeshi huyo.

Askari huyo alipewa taarifa za siri na Wasamaria wema kuhusu Mkewe ambaye ni Mama Mshirika na pia ni Kiongozi wa Kanisa hilo kuchepuka na Kasisi huyo aliyetambulishwa kwa jina Rev Kime ndipo alipoamua kumvizia nyumbani kwake ambapo alirejea nyumbani kimyakimya usiku bila kumpa taarifa Mkewe na akaingia katika chumba kimoja bila ya Mkewe kujua ili kuthibitisha taarifa hizo.

Baada ya muda kidogo akaingia chumbani kwake na kumfumania Mtumishi huyo wa Mungu mwenye umri wa miaka 43 katika kitanda chake na Mke wake ndipo alipochukua uamuzi wa kumchoma na kitu chenye ncha kali mgongoni na kumkata sehemu zake za siri na kisha Askari huyo akatoweka kusikojulikana na Mkewe ambaye amejeruhiwa hajulikani alipo.

Majirani wameuambia mtandao wa The Star kuwa kabla ya kumuua Mchepuko wa Mkewe, Askari huyo alimfunga Mkewe kwenye kona ya nyumba ili amshuhudie wakati akimuua Mchepuko wake huyo ambapo ripoti zinasema Kasisi huyo alikuwa akisafiri KM 30 hadi kwa Mwanamke huyo na kufanya nae ngono pale Mumewe anapokuwa kwenye kazi zake za ulinzi wa Nchi.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nandi Dickens Njogu amesema “Ilikuwa tu asubuhi ya leo wakati Mkuu wa Kanisa kuu la St. Barnabas Mchungaji Nillah Bassy alipotoa ripoti rasmi ya tukio hilo la kusikitisha sana ambalo Maafisa wa Polisi walikwenda kushuhudia”

Ripoti zimesema baada ya tukio hilo Majirani walimpeleka Mchungaji huyo Rev Kemei katika Hospitali ya Kapsabet Level 5 akiwa katika hali ya umahututi na baadaye alipelekwa Eldoret na kisha akapelekwa Hospitali ya Top Hill ambako alifia akiendelea na matibabu.
#MillardAyoUPDATES
Kumkata tu amemuhurumia sana, ningemfunga kwenye gari na kumburuza nchi nzima akiwa uchi, sheenzi kiongozi wa dininunaendekeza uzinzi tu
 
Back
Top Bottom