Mwanahistoria Francis Daud Alipotembelea Nyumba ya Ali Msham Magomeni Mapipa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
MWANAHISTORIA FRANCIS DAUD ALIPOTEMBELEA NYUMBA YA ALI MSHAM MAGOMENI MAPIPA DAR ES SALAAM

Historia ya Ali Msham ni katika historia zinazosisimua za wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa hali na mali zao lakini historia imewasahau.

Lau kama si picha alizoacha Ali Msham baada ya kifo chake leo hii ingekuwa tabu watu kuamini kuwa Ali Msham alikuwa moja ya nguzo za Mwalimu Nyerere katika kukipa msukumo chama cha TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Watu wangepata tabu kuamini kuwa Ali Mshama alipata kufahamiana kwa karibu sana na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mkewe Mama Maria Nyerere.

Leo nilitembelewa na mhadhiri wa historia Francis Daud ambae hivi sasa anakamilisha Ph D yake Uswisi na tulizungumza mengi.

Mwisho wa mazungumzo yetu aliniomba nimpeleke kwenye nyumba ya Ali Masham ambako palikuwa na tawi la TANU, duka la mafuta ya taa la Mama Maria Nyerere, shule ya watoto wadogo na ua wa nyumba hiyo ndiyo ulikuwa ukumbi wa mikutano ya ndani ya TANU.

Francis Daud anazungumza na mtoto wa Ali Msham, Mfaume Ali Msham.

Sisi kama walivyo watoto wa Ali Msham hatutoacha kumkumbuka na kumuenzi mzalendo huyu aliyeisabili nyumba yake kwa TANU ili Tanganyika iwe huru.

 
Back
Top Bottom