Mwanaharakati wa Haki za watu weusi nchini Marekani Mutulu Shakur afariki Dunia

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,110
37,645
Tanzia.

Mutulu Shakur, Mwanaharakati wa haki za Weusi wa Marekani, Mfungwa alietumikia Miaka 35 Jela Kati ya 60 aliohukumiwa, Baba wa kufikia wa Mkali asiyechuja Tupac Shakur amefariki!

Amefariki nyumbani akiwa na familia yake. Enzi za uhai wake alikuwa Mwanachama wa New Afrikan Movement na pia ni Legendary wa Black Liberation Army.

Mwaka jana May 2022, mwanasheria wake Brad Thomson, aliweka wazi kuwa Madaktari wa Shirikisho la Magereza la Marekani wamemfahamisha kuwa Mutulu amebakisha miezi 6 tu ya kuishi.

Amefariki usiku wa jana akiwa na miaka 72. Anaenda kuungana tena na Mama Afen Shakur pamoja na Mwanae wa kufikia Legendary Tupac.

IMG_7938.jpeg
 
mwanaharakati aliyeingia jela uwa namuheshimu sana.amekubali kupoteza muda wake kwa ajili ya watu wengine.
Ni kweli. Na Wanaharakati wa hivo huwa wanaamini Jela ni another platform ya harakati zao!
 
Uwana harakati wa kweli unaweza kumpotezea mtu muda ila sio heshima yake. Sio kama hawa wetu wa bandari kesho utawakuta wakigonga glass.

Ni hayo tu.
Kwa akili yako, ulitaka watu wasihoji vifungu tata kwenye mkataba wa bandari ?!

Hufai kuwazungumzia wanaharakati.
 
Familia yao wana majina ya kiafrika.
Rip Mutulu Shakur
From Jomo Kenyatta; Mohammed Ali; Malcom X na hata huyu jamaa Born. Jeral Wayne Williams; Majina waliyopewa na waliyoamua kuyachukua hapo baadae ni tofauti...

Sababu ni tofauti tofauti ila nyingine ni ku-indentify na the roots; Kuachana na majina waliyopewa na wanaowa-marginalize kwamba ni kama utumwa - au mwingine kwa X aliweka hio X sababu Surname yake hai-kudepict ancistors wake na hilo jina lilipatikana utumwani...

At least watu hawa wa zamani walijua wanataka nini na waliishi katika kutafuta wanachotaka - sasa hivi watu wanahisi wanachotaka na mara nyingi kinaendana na illusion fulani ambayo unakuta inabadilika badilika; Anyway to each their own...
 
Dogo Tupac akiwa na Babake wa Kufikia - Mutulu Shakur. Mutul Shakur ni Baba Mzazi wa Sekyiwa Shakur.

Sekyiwa Shakur ndiye aliepokea tuzo ya Tupac mwezi ulopita ya "Hollywood Walk of Fame Star" iliyopo 6212 Hollywood Blvd.

Tupac amemzungumza Sekyiwa Shakur ktk Ngoma yake kali ya DEAR MAMA....

"I shed tears with my baby sister, over the years
We was poorer than the other little kids
And even though we had different daddies, the same drama
When things went wrong we'd blame Mama"
Screenshot_20230708-091042_Instagram.jpg
 
Tanzia.

Mutulu Shakur, Mwanaharakati wa haki za Weusi wa Marekani, Mfungwa alietumikia Miaka 35 Jela Kati ya 60 aliohukumiwa, Baba wa kufikia wa Mkali asiyechuja Tupac Shakur amefariki!

Amefariki nyumbani akiwa na familia yake. Enzi za uhai wake alikuwa Mwanachama wa New Afrikan Movement na pia ni Legendary wa Black Liberation Army.

Mwaka jana May 2022, mwanasheria wake Brad Thomson, aliweka wazi kuwa Madaktari wa Shirikisho la Magereza la Marekani wamemfahamisha kuwa Mutulu amebakisha miezi 6 tu ya kuishi.

Amefariki usiku wa jana akiwa na miaka 72. Anaenda kuungana tena na Mama Afen Shakur pamoja na Mwanae wa kufikia Legendary Tupac.

View attachment 2681676
RIP roommate
 
Back
Top Bottom