Mwanahalisi lilitabiri uchakachuaji october 6. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanahalisi lilitabiri uchakachuaji october 6.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by politiki, Nov 4, 2010.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  GAZETI LA MWANAHALISI LILITABIRI KILA KITU KINACHOTOKEA HIVI SASA SOMA HAPA CHINI. MWANAHALISI YA OCTOBER 6.2010.

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetwishwa tuhuma nzito za kuandaa mipango ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu ili kionekane kimeshinda, MwanaHALISI inaweza kuripoti.
  Taarifa zilizosambazwa kwa maandishi katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, zinadai kuwa CCM imefanikiwa kupenyeza wachakachuaji kura katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
  Maandishi hayo hayana saini na yamechapishwa kwenye karatasi za ukubwa wa A4.
   
Loading...