Njama za kuiba kura jamani hizi hapa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njama za kuiba kura jamani hizi hapa.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by URASSA THE DON, Oct 15, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. URASSA THE DON

  URASSA THE DON Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [​IMG]


  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetwishwa tuhuma nzito za kuandaa mipango ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu ili kionekane kimeshinda, MwanaHALISI inaweza kuripoti.
  Taarifa zilizosambazwa kwa maandishi katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, zinadai kuwa CCM imefanikiwa kupenyeza wachakachuaji kura katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
  Maandishi hayo hayana saini na yamechapishwa kwenye karatasi za ukubwa wa A4.
  Madai hayo yanaihusisha pia serikali na idara ya usalama wa taifa kwa kupeleka NEC watumishi kadhaa wenye ujuzi katika mawasiliano ya kompyuta (IT) ili kufanya maandalizi ya uchakachuaji matokeo ya uchaguzi.
  Hata hivyo, Mkurugenzi wa NEC, Rajab Kiravu ameliambia gazeti hili kuwa hawezi kutolea tamko hoja hii kwa madai kuwa alikuwa mkutanoni.
  Gazeti lilikuwa limemuuliza iwapo anajua kuwa kuna maofisa wenye utaalam wa IT waliopelekwa NEC kwa lengo la kuchakachua matokeo ya uchaguzi kwa niaba ya CCM.
  Alisema, “Niko kwenye kikao. Nikitoka hapa nakwenda Airport (Uwanja wa Ndege). Nakwenda Zanzibar. Nitafute Jumatano (leo) nikitoka Zanzibar.”
  Nacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekiri kupelekewa makaratasi hayo, mbali na nyaraka kutoka serikalini, NEC na idara ya usalama wa taifa zinazoonyesha kuwapo kwa mpango huo.
  Akiongea na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka Mwanza, mwanasheria wa CHADEMA na wakili wa mahakama kuu, Mabere Marando, alisema chama chake kinafahamu njama hizo na kwamba kimepanga kuchukua hatua za haraka kuhakikisha hakuna kura inayoibwa.
  Aidha, taarifa hizi pia zinakuja siku tano tangu Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JW), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo atangaze kuwa jeshi linaingia rasmi katika mchako wa uchaguzi mwaka huu.
  Alisema vyombo vya ulinzi vitashirikiana na NEC katika kipindi chote ili kuhakikisha kuwa wadau wote wanaheshimu matokeo.


  MJUE NDUGU ZANGU NI RAHISI SANA KWA MTOTO(CCM) KUCHEZEA MATITI YA MAMA YAKE,ILA SI RAHISI KUCHEZEA KORODANI(CHADEMA) YA BABA YAKE KWA HIYO CHA MSINGI SASA NI KUPIGA KURA YA NDIO KWA DR SLAA (PHD),KWA MFANO AHH SIO MFANO KI UKWELI SLAA (PHD) AKIPATA KURA MILLION 11 NA KIKWETE (BA) AKIPATA KURA MILLION 3 NI VIGUMU SANA KUCHAKACHUA MATOKEO ILA DR SLAA AKIPATA KURA MILLION 8 NA MKWERE AKIPATA MILLION 7 HAPO NI RAHISI SANA KUCHAKACHUA KWA HIYO POINT NI KUJITOKEZA KWA WING KWELI
   
 2. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  eeh mola tuepushe na huu wizi wa ccm
   
 3. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  mmh aisee!
   
 4. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wamekwisha ......
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...