anjnr
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 539
- 208
Gazeti la mwanahalisi limeshinda kesi yake na mlalamikaji ameamriwa na mahakama kulipa gharama za kesi.
Chanzo: Tanzania Daima toleo la leo.
Habari yenyewe hii hapa: By Buchanan,
KESI ya kukashifu, iliyokuwa ikilikabili gazeti la MwanaHALISI, imetupiliwa mbali na mdai ametakiwa kulipa gharama zote za kesi. Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Warialwande Lema, katika hukumu yake Jumatano, alisema ili maneno yawe, au yaonekane kuwa ya kashfa, sharti yawe ama si ya kweli au yawe ya uongo. Alisema kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakama haikuona chochote kile kilichothibitisha madai ya kashfa. Juma Jaffari Nyaigesha, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msewe, jijini Dar es Salaam ndiye alilishtaki gazeti akidai kuwa kwa habari na makala zilizochapishwa katika matoleo yake matano, alikashifiwa na kuvunjiwa heshima mbele ya jamii. Mdai alimshtaki mhariri wa gazeti, Jabir Idrisa, mshauri wa gazeti, Ndimara Tegambwage, Stella Kajuna mkazi wa Msewe, mhariri mkuu, kampuni inayochapisha gazeti, Hali Halisi Publishers Limited, kampuni ya uchapaji ya Printech na kampuni nyingine ya uchapaji, Tanzania Standard Printers Limited. Nyaigesha alidai kuwa matoleo matano ya MwanaHALISI yalikuwa na taarifa zilizomkashifu na kumwondolea hadhi mbele ya jamii. Aliyataja matoleo hayo kuwa yale ya 10, 12, 24, 31 Oktoba 2007 na 14 Oktoba 2008. Katika matoleo hayo kulikuwa na habari na makala juu ya madai ya kuwepo vitendo vya uhalifu Msewe, ukosefu wa amani na matumizi mabaya ya madaraka ambavyo Nyaigesha alidai vilikuwa vinaelekezwa kwake. Katika hukumu yake, hakimu Lema alisema kwanza mdai hakuleta hata shahidi mmoja kuthibitisha madai yake na kwamba yeye mwenyewe hakuweza kuthibitisha kuwa amekashifiwa. Hata takwimu za kura za uchaguzi alizopeleka mahakamani, zilionyesha kuwa hata baada ya kuandika yaliyokuwa yakitokea Msewe, katika uchaguzi uliofuata alipata kura nyingi, jambo ambalo lilikinzana na madai ya kukashfiwa. Hakimu alisema Jaffari ni kiongozi na kile walichofanya waandishi kilikuwa ni mjalizo halali na wa haki juu ya kiongozi na uongozi wa umma na siyo kashfa. Alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa na walalamikiwa, ushahidi wa maandishi kutoka kwenye kata na hata kauli ya mdai kuwa mmoja wa walalamikiwa alipigwa na kwamba yote hayo yalidhihirisha umuhimu wa kilichoandikwa. MwanaHALISI ilikuwa ikitetewa na wakili maarufu, Mabere Marando, wakati Tanzania Standard Printers Ltd, iliwakilishwa na wakili Audax Kahendaguza Vedasto wote wa Dar es Salaam. Kuhusu wachapaji wa gazeti, hakimu alisema hawakuwa na hatia kwa kuwa hawakutenda kashfa yoyote, kwa vile hakuna kashfa iliyothibitishwa. Aidha hakimu alikubaliana na hoja kwamba mchapaji anayefanya kazi aliyopewa na kuirejesha kwa mhusika, hawezi kuwa ametenda kashfa. Alipoulizwa Mkurugenzi Mtendaji wa HaliHalisi Publishers, Saeed Kubenea, juu ya hatua anayojiandaa kuchukua, alisema hajakaa na wakili wake kupanga hatua inayofuata.
Source: Tz Daima.

Last edited by a moderator: