Mwanahalisi imepotosha kauli ya Mbunge wa Tanga (Viti Maalum)

AMOSIRICHARD

Member
Apr 25, 2020
50
40
JE, MWANAHALISI WAMEHONGWA KUPOTOSHA KAULI YA MHE. MWANAISHA?

The Diplomat
Vita dhidi ya ufisadi ni ngumu sana kwa sababu baadhi ya vyombo vya habari vinamilikiwa na mafisadi ama vinajiendesha kwa kutumia fedha za mafisadi zinazotolewa kwa ajili ya kuzuia hoja zenye maslahi makubwa kwa Taifa.

Mwanahalisi imepotosha kauli ya Mbunge wa Tanga (Viti Maalum) Mhe. Mwanaisha Mlenge ambaye ameishauri Serikali iwe na Ofisi moja tu ya tathmini na ufuatiliaji kuliko kuwa na viofisi vidogo sita ambavyo havina nguvu kwa sababu vipo chini ya Wizara mbalimbali ikiwemo Utumishi, TAMISEMI na Wizara ya Fedha.

Mwanahalisi ilidai eti ushauri huo adhimu unakusudia kuundwa kwa chombo kitakachoiweka Serikali mfukoni likidai eti chombo hicho kitapunguza mamlaka ya Serikali.

"Mhe. Spika naomba kuishauri Serikali, ili mikakati yetu bora, mipango yetu mizuri na miradi yetu mizuri iende kufanya kazi na kuleta matunda yanayotarajiwa ni lazima tujipange vizuri katika ufuatiliaji na tathmini.

“Ukiangalia Afrika Kusini ina taasisi malumu ya tathmini na ufuatiliaji ndani ya Ofisi ya Rais, Uganda wana taasisi maalum ya ufuatiliaji ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ghana ina Wizara maalumu ya ufuatiliaji lakini Tanzania tathmini na ufuatiliaji umepewa sekta ndogo katika Wizara sita tofauti,”_ amesema Mhe. Mwanaisha.

Ukweli ni kwamba, kauli ya Mhe. Mwanaisha ina faida nyingi ikiwamo kuweka umakini kwenye ufuatiliaji na tathmini ili kujua utekelezwaji wa miradi mbalimbali na changamoto katika utekelezaji wake; na kukomesha matumizi mabaya ya fedha za umma, ubadhirifu na ufisadi.

Mwanahalisi jitahidini kuwatumikia maslahi ya umma. Tamaa za kujaza matumbo yenu zisiwafanye mkazuia ushauri unaolenga kulisaidia Taifa. Pingeni kwa haki! Msiipinge haki!
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
6,390
8,951

Kwani huyo mbunge ni wa Jimbo gani?
Masalia ya mwendazake yana luka na kukanyagana
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom