Mwanafunzi na mzee wajinyonga Manyara

Mwanafunzi na mzee wajinyonga Manyara

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,273
Reaction score
25,296
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga akizungumza leo Alhamisi amesema matukio hayo ya vifo yametokea kwenye mazingira tofauti.

Simanjiro. Watu wawili wamefariki dunia wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kujinyonga akiwemo mwanafunzi wa darasa la saba wa shule msingi iliyopo mji mdogo wa Mirerani.

Kamanda Senga amesema tukio la kwanza lilitokea kwenye Kata ya Endiamtu mji mdogo wa Mirerani ambalo limemuhusu mwanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Songambele, Neema Achuu (15).

Amesema mwanafunzi huyo anayeishi na shangazi yake alijinyonga chumbani kwao jana Jumatano saa saba mchana kwa kutumia mtandao na kufariki dunia papo hapo.

Amesema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana na polisi bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.

Amesema kwenye tukio lingine mkata mkaa wa eneo la Kidawash, Tarafa ya Moipo, Isack Mlokole (60) alijinyonga na kamba kwenye mti.

Amesema polisi walipopata taarifa jana Jumatano saa 4 asubuhi walifika eneo la tukio na kukuta mfuko ukiwa pembeni ya mwili wake uliokuwa ukining'inia.

"Kwenye huo mfuko aliouacha marehemu tulikuta ujumbe kuwa ameamua kujiua mwenyewe na mtu yeyote asisumbuliwe wala kuulizwa juu ya kifo chake kwani ni uamuzi wake mwenyewe ukiwa na jina lake," alisema Kamanda Senga.

Mwananchi
 
RIP babu na mjukuu
Wachunguzwe DNA huenda wametokea eneo fulani Southern Highlands
 
Wameenda kula bata kwa sir.. God mda mwingn ukiona unachelewa kwenda unajipeleka Dadeek..
 
Ukifuatilia sana kwa undani utagundua chanzo cha kujinyonga kwa hao madogo ni MAPENZI
 
Back
Top Bottom