Mwanafunzi mpya Chuo Kikuu ajinyonga(1st yr)

Sine r Winters

Senior Member
Jul 10, 2012
110
15
MWANAFUNZI aliyemaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari Saronge, iliyoko mkoani Kigoma na kuchaguliwa kwenda chuo kikuu kwa ajili ya kuanza masomo ya mwaka wa kwanza katika kipindi cha mwaka 2012/2013, amekufa akidaiwa kujinyonga wilayani Bunda mkoani Mara. Tukio hilo lilitokea juzi katika kitongoji cha Kimanitwentemi, kilichoko katika kijiji cha Kabasa wilayani hapa na Mwenyekiti wa kitongoji hicho Donard Kalemela, alisema mwanafunzi huyo anatambuliwa kwa jina la Majinge Mafuru, mkazi wa kijiji hicho. Baba wa mwanafunzi huyo, Samson Musimu, alisema mwili wa mwanafunzi huyo uligunduliwa na mdogo wake baada ya kutoka shuleni na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Alisema mfukoni mwake walikuta ujumbe wa maandishi ukisomeka, “Naomba mniandalie mahali pa kulala, nimeamua mwenyewe, baada ya kuwa nimeghafirika, msimshuku mtu yeyote, ni maamuzi yangu mwenyewe, ahsante.”
 
kwa tulio hai hakuna tatizo lisilo na suluhisho na hasa ukiamua kulitafuta suluhisho kwa dhati kabisa!
pumzika kijana lala pema peponi!
 
lakini pia lipo tatizo la udhaifu wa elimu itolewayo mashuleni,tunapoelimishwa vyema wakati wote tufanya juhudi za kukiepuka kifo mpaka pale kitakapokuja kwa wakati wake na kwa namna yake.
Bado tuna ulazima wa taaluma ya ualimu kuboreshwa zaidi ili walimu warudi kwenye sifa yao ya ualimu na malezi ili vijana wengi walio na msongo na sonono wapate pa kukimbilia na kueleza yanayowasibu, na hakika mwalimu bora lingekuwa kimbilio sahihi kwao!
 
MWANAFUNZI aliyemaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari Saronge, iliyoko mkoani Kigoma na kuchaguliwa kwenda chuo kikuu kwa ajili ya kuanza masomo ya mwaka wa kwanza katika kipindi cha mwaka 2012/2013, amekufa akidaiwa kujinyonga wilayani Bunda mkoani Mara. Tukio hilo lilitokea juzi katika kitongoji cha Kimanitwentemi, kilichoko katika kijiji cha Kabasa wilayani hapa na Mwenyekiti wa kitongoji hicho Donard Kalemela, alisema mwanafunzi huyo anatambuliwa kwa jina la Majinge Mafuru, mkazi wa kijiji hicho. Baba wa mwanafunzi huyo, Samson Musimu, alisema mwili wa mwanafunzi huyo uligunduliwa na mdogo wake baada ya kutoka shuleni na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Alisema mfukoni mwake walikuta ujumbe wa maandishi ukisomeka, “Naomba mniandalie mahali pa kulala, nimeamua mwenyewe, baada ya kuwa nimeghafirika, msimshuku mtu yeyote, ni maamuzi yangu mwenyewe, ahsante.”

uyo n dem au n dude.
 
alighafirika nini hadi akajinyonga? kuna sababu. alale mbele ya shetani peponi
 
Wote tutakwenda huko huko tu tatizo sisi wengine hatutaki kijipeleka mpaka tupelekwe wakati wetu ukifika.Kaamua kujiwahi ingawa katika hali ya kawaida inasikitisha kujiwahisha huko.
 
Huo ujumbe kauandika mwenyewe? maana sikuhizi kuna style ya kuuwa watu na kuwawekea ujumbe mfukoni! panahitajika uchunguzi hapo!
 
MWANAFUNZI aliyemaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari Saronge, iliyoko mkoani Kigoma na kuchaguliwa kwenda chuo kikuu kwa ajili ya kuanza masomo ya mwaka wa kwanza katika kipindi cha mwaka 2012/2013, amekufa akidaiwa kujinyonga wilayani Bunda mkoani Mara. Tukio hilo lilitokea juzi katika kitongoji cha Kimanitwentemi, kilichoko katika kijiji cha Kabasa wilayani hapa na Mwenyekiti wa kitongoji hicho Donard Kalemela, alisema mwanafunzi huyo anatambuliwa kwa jina la Majinge Mafuru, mkazi wa kijiji hicho. Baba wa mwanafunzi huyo, Samson Musimu, alisema mwili wa mwanafunzi huyo uligunduliwa na mdogo wake baada ya kutoka shuleni na kuingia ndani ya nyumba hiyo. Alisema mfukoni mwake walikuta ujumbe wa maandishi ukisomeka, "Naomba mniandalie mahali pa kulala, nimeamua mwenyewe, baada ya kuwa nimeghafirika, msimshuku mtu yeyote, ni maamuzi yangu mwenyewe, ahsante."

Nature has a way of eliminating bad genes from a generation, that is one way. Why would someone take his own life for whatever reason?
 
anadhani yeye ndiye mwenye matatizo, wote tunayo. Its not a right idea and he was lacking self confidence. njia nyeupe kwa moto
 
kama kweli ni maamuzi yake mwenyewe nasikitika sna kwani alikuwa yu bado kijana mdogo angeweza kuleta chachu kubwa sana katika maendeleo ya taifa letu mungu akupumzishe mahali pema peponi.
 
Hamna kitu kibaya kama unapokua na tatizo then hutaki kulitiririsha watu wakusaidie. Hii kitu ni mbaya sana. Inapendeza hata kumwambia mzazi au mtu wako wa karibu ili akusaidie mawazo. YAN NAUHAKIKA HILO TATIZO ANGELITAJA HAPA JF ANGEPEWA MAJIBU YA KUTOSHA THEN ANGEFURAHI MWENYEWE.
 
kama unaona maisha magumu, achana nayo ufanye kitu kingine
 
Dah!
Msongo wa mawazo mbaya sana!

Ni kweli msongo wa mawazo unasababisha kitu kinaitwa ''sonona''(Depression) na kupelekea mtu kufikia maamuzi kama hayo. Binadamu tunatofautiana jinsi ya kupambana na sonona, wengine hufikia maamuzi kama hayo lakini moja ya sababu kubwa ni kukosekana kwa watu wa karibu ambao angeweza ku-share nao yale yanayomsibu.
 
Back
Top Bottom