Mwanafunzi avaa mabango na kukaa barabarani akipinga kuchaguliwa masomo ya ECA ambayo hajayasomea

Si mchezo, mie dogo kapangiwa Shybush HGL "CCA" ana 1 ya 15, kasheshe ni kwamba yeye alijaza vyuo vya Tech DIT,MUST & AIT na PCM ana "BCD" je wakuu anaweza pata transfer ya kwenda kwa hizo college? Kama ndio taratibu za sasa zikoje?
Ndio makosa yenyewe hayo tamisemi wafanye majukumu yao kwa weledi wasiwaharibie watoto future zao.by the way anaweza kubadili maana sifa Anazo cha kufanya ni kwenda moja kwa moja chuoni husika watampikea.
 
Huyo dogo dishi lake naliona kwa mbaaali limeyumba.Masuala ya kubadilisha Combination (Tahasusi) huwa yapo rahisi tu.Yeye angeenda ktk shule yake ya awali alikomaliza kidato cha nne na kumuona mkuu wa shule, kisha amueleze shida yake na mkuu angemhudumia vizuri tu hadi akafanikiwa.Hicho alichofanya ni ujinga na amejiweka ktk mazingira magumu ya kupokelewa ktk shule atakayokwenda kuanza kidato cha 5.
Ndio inawezekana kubadili izo tahasusi lkn Incase should ambayo amepangwa haina tahasusi anayopenda itakuwaje mama sio kupotezwa uko...
 
Tamisemi wameshatoa ufafanuzi kuhusu hili kuna uzi unazungumzia hili. Tafuteni huo uzi.
 
Ndio inawezekana kubadili izo tahasusi lkn Incase should ambayo amepangwa haina tahasusi anayopenda itakuwaje mama sio kupotezwa uko...
Mkuu kama shule aliyopangwa haina hiyo tahasusi anayopenda kusoma ataomba uhamisho na kwenda kwenye shule ambayo inayo hiyo Tahasusi.
 
Mwanafunzi Josephat John hakuchaguliwa ECA na hakuwa na sifa za kuchaguliwa PCB

OR-TAMISEMI,DODOMA

Mwanafunzi Josephat John aliyekuwa anasoma kidato cha nne shule ya Sekondari Kom iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga alizua taharuki baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya biashara (ECA) ambayo anadai hajawahi kusomea kwani yeye amesoma masomo ya Sayansi(PCB)

Mwanafunzi huyu amepata Div II:21 na masomo ya sayansi anayodai amesomea amepata DCC yenye jumla ya pointi 10. Mwisho wa pointi za wanafunzi waliopangiwa Tahasusi hii ni 8 sawa na BCC, hivyo mwanafunzi huyu hajakidhi vigezo vya kuchaguliwa katika Tahasusi hii ya PCB kulingana na idadi ya nafasi zilizopo mwaka huu.

Hata hivyo Mwanafunzi huyu hajapangiwa Tahasusi ya Biashara (ECA) kama anavyodai, bali amepangiwa kusoma Stashahada Maalumu ya Ualimu kwa Masomo ya Physicis na Hesabu katika chuo cha Ualimu Songea ambapo ni miongoni mwa Maeneo aliyochagua katika machaguo ya vyuo alianza na Ufundi, Afya kisha Elimu.

OR TAMISEMI inaendelea kumtafuta mwanafunzi huyu ili iweze kufahamu nia na shida ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia kufanya kitendo hiki.

OR TAMISEMI inaendelea kusisitiza kama kuna mzazi au mlezi yoyote anahitaji ufafanuzi wowote awasiliane na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu namba 0735-160201 na 0262-160201 kuandika barua pepe kwenye anwani yetu huduma@tamisemi.go.tz
Sawa
 
Dogo home apa ana three ya 23, kapangiwa chuo Tanga tena course ya u secretary ajabu ji wa kiume. Na hakuchagua
 
This country has gone to the dogs! PCB na ECA wapi na wapi? Apewe anachotaka kama kashinda. Na angekuwa hajashinda asingehangaika!
 
Si mchezo, mie dogo kapangiwa Shybush HGL "CCA" ana 1 ya 15, kasheshe ni kwamba yeye alijaza vyuo vya Tech DIT,MUST & AIT na PCM ana "BCD" je wakuu anaweza pata transfer ya kwenda kwa hizo college? Kama ndio taratibu za sasa zikoje?
Hili tatizo naona wamepatacwengi, waliochagua vyuo wamepangiwa advance. Waliochagua advance kama chaguo lao wamepangiwa vyuo
 
Kwa
View attachment 1808793

Mwanafunzi Josephat John, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo Manispaa ya Shinyanga, amezua taharuki ya aina yake leo mchana Ijumaa Juni 4,2021 mjini Shinyanga mara baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango na kujifunika maboksi yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya Economics, Commerce , Accounts (ECA) ambayo amedai hawajawahi kuyasomea kwani yeye amesomea masomo ya Physics, Chemistry, Biology (PCB).

Ametumia mbinu hiyo ya kuvaa mabango kuiomba Wizara husika ifanye uchaguzi upya wa michepuo ili akasomee masomo ambayo ameshayasoma.

Tukio hili limekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu atangaze matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda vyuo vya ufundi na vyuo vya kati na kidato cha Tano mwaka 2021.

Kwa kwandiko huo ni bahati hiyo kuchaguliwa ashukuru tu
 
Kuna masomo kama umeyafaulu inamaanisha na ya aina nyingine utayaweza. Waliompangia hawajakosea.

Huyu dogo ni miyeyusho.

Hajawahi kusikia kama kuna kuhama? Tena huu muda anaopoteza kukaa juani akichanga karata vizuri atajikuta hata huko alikopangiwa hafikii kuripoti ataenda zake shule aliyotaka kuhamia.

Hiki alichofanya kinaingia kwenye rekodi. Anaweza akatemwa na baadhi ya shule/ taasisi kwa kuonekana ni rebel hata kwa vitu vya kutumia akili ya kawaida tu.
Sikuungi mkono, kila mmoja anakitu amambocho yeye akisomea na kukifanya anakuwa comfortable na anafanya kwa moyoo wote, huwezi mchagulia mtu nini cha kufanya na kusoma, hayoo mambo yalishapitwa na wakati, umeshawahi pita kwenye taasisi mbalimbali mtu anakwambia hatasijuii kwanini nilisoma hii field, waza sasa ni daktari au nesi, anatakiwa kuhudumia watu ndio maana inafika mahala dk wa kusomea anashauri tupige nyungu. Naungana na kijana.
 
Amesema hajasoma masomo ya taasusi ya ECA
 
Mimi nimeongelea pande zote mbili.

Waliomchagua hawajakosea. Hii ni kwa upande wa waliomchagua.

Aliyechaguliwa anaweza kuhama siyo lazima kwenda alipochaguliwa. Hii ni kwa aliyechaguliwa.

Halafu humu humu kuna update kutoka Tamisemi ikisema hana marks za kwenda sayansi so waliomchagua wamejiongeza. Na yeye badala ya kujiongeza kuhama kaenda barabarani.
 
1622898671733.png
 
Back
Top Bottom