Mwanafunzi aunda mabomu ya machozi nchini Uganda

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,276
Samuel Mugarula, Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda amevumbua njia ya kutengeneza mabomu ya kutoa machozi (Tear Gas) ambayo hutumika na vikosi vya polisi mara nyingi kuzima maandamano.
1476446940264.jpg
Mugarula 23, ambaye anayetarajiwa kuhitimu mwakani shahada ya kemia na utafiti wa mimea, alianza kutengeneza bomu la kutoa moshi wa machozi (Tear Gas) baada ya hapo Mugarula alifanya utafiti zaidi kutengeneza vilipuzi vingine, mfano bomu la moshi mkali na vibomu vidogo vidogo vya moto

"Imenichukua miaka mawili, nilianza mwaka 2014, na bomu la kutoa moshi wa machozi na nilipotoka na mafanikio ulikuwa ni mshangao mkubwa nilikuwa na furaha sana ndio maana niliendelea kufanya utafiti katika milipuko mingine"alisema

Mugarula anasema baadhi ya vifaa anavyotumia kutengeneza vilipuzi hivyo ni vifaa vya kawaida vinavyotumika majumbani, mfano sukari, hamira ya kuumua mikate, na vikorombozo vingine na sukari yenye sumu kali inayotengezwa maabara ambayo haitumiki majumbani.

Vikosi vya usalama nchini Uganda vimetaka kumkamata Mwanafunzi huyo anayemaliza kusoma mwaka huu kwa hofu ya kuhatalisha usalama wa Taifa.

Mugarula ana hofu kuwa huenda makundi ya kigaidi wakataka katumia ubunifu wake ndio maana aliweza kuwaandikia barua Waziri mkuu wa Uganda Dk. Ruhakana Rugunda, Waziri wa Elimu Janet Museveni na Mkuu wa polisi wa Uganda Jenerali Kale Kayihura akiwafamisha msimamo wake kutaka kushirikiana kwa pamoja na serikali ya Uganda katika utafiti wake

Mugarula kwa sasa habari zake zimefika kwa Rais wa Uganda na amealikwa rasmi kukutana na Rais Yoweri Kaguta Museveni

Chanzo : BBC
 
Aletwe Bongo haraka sana!!

Vijana kama hawa ndio nguvu ya taifa!!

Alichotengeneza ndio zana muhimu sana kwa uongozi Bongo!
 
Umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu.
Makerere siyo kama zamani lakini kwa hii hatau ya mwanafunzi wao wa mzima 23 kufanya kitu kikubwa hivyo inatia sana hamasa. Hapo kafungulia mlango wanafunzi wengine wataiga huo mfano .
 
Ndio mkuu.. kaamsha bongo zilizolala kuwa kila kitu kinawezekana
 
Napenda kumpongeza huyu ndugu kwa ubunifu wake (innovation) na si ugunduzi (invention) kama mwandishi anavyotaka kutuaminisha. Nashindwa kuelewa tafsiri ya neno ugunduzi. Unapogundua kitu ambacho ni technology artefact in maana kina unique design na pia kinaweza kuwa patented. Unaposema umegundua bomu la machozi napata ukakasi kwenye hii statement. Ni sawa na useme mtu amegundua helikopta wakati helikopta tayari zipo. Kwa kiingereza ugunduzi ni invention. Na maana ya Invention ni hii hapa "something that has never been made before, or the process of creating something that has never been made before:". Sasa maswali yangu ya msingi je ile bomu lina tofauti gani na hayo yanayo exist? Maana hapo ndo tunaweza kujua kama kuna invention au hakuna. Na pia kuna kitu kinaitwa innovation ambayo mara nyingi ni kuboresha existing ways na kuja na new ways ambazo ni better au unique. Je hilo bomu linafit kwenye category ya innovation au invention. Nawaomba kama great thinkers tujaribu kufikiria sambamba na maana za invention na innovation. Maana hawa waandishi wa habari wengi ni v.i.laza katika kureport ishu kama hizi.
 
Mkuu.. Lengo linaweza kuwa moja lakini kila mmoja ana njia yake ya kufikia katika lengo hilo

Kwahivyo kinachoongelewa hapa nadhani ni namna ya njia ya kutengeneza na vifaa vinavyotumika
 
Kwa hiyo mimi nafikiri ni innovation (ubunifu) maana amekuja na unique way kutengeneza bomu la machozi ambayo ina involve vifaa vya kawaida vinavyopatikana majumbani. Ingekuwa invention pale tu ambapo kusingekuwa na bomu la machozi kabisa kwa hiyo yeye ndo wa kwanza kuja nalo..Ndo maana utasikia kuna mtanzania amebuni gari au helikopta hawasemi amegunduaaa..
 
Huko jamaa kaunda bomu kaalikwa kukutana na rais....hapa bongo watu wanatengeneza magari na chopa, wanaambulia maonyo na vitisho vya kutosha.....Hivi unaweza kukataa kuwa hii nchi haina laana kweli???
 
Kwa hiyo mimi nafikiri ni innovation (ubunifu) maana amekuja na unique way kutengeneza bomu la machozi ambayo ina involve vifaa vya kawaida vinavyopatikana majumbani. Ingekuwa invention pale tu ambapo kusingekuwa na bomu la machozi kabisa kwa hiyo yeye ndo wa kwanza kuja nalo..Ndo maana utasikia kuna mtanzania amebuni gari au helikopta hawasemi amegunduaaa..
Yah.. huwezi sema nimegundua helicopter ama gari ilhali magari tayari yapo, hapo ni uundwaji kwa vifaa ni vya kawaida sana katika jamii yetu
 
Back
Top Bottom