Mwanablogu auawa kinyama Bangladesh

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
16,654
Reaction score
18,804
Mwanablogu mmoja mwenye asili ya Marekani na ile ya Bangladeshi- maarufu kwa maoni ya kumkana Mungu ameuawa kinyama alipozuru mji wa Dhaka.

Avijit Roy ambaye alikuwa akiishi Marekani alikuwa amezuru mji huo mkuu wa Bangladeshi na mkewe kuhudhuria dhifa ya uzinduzi wa kitabu.

Alikuwa amepokea vitisho baada ya kuchapisha makala ya kupigia debe maoni huru, sayansi na maswala ya jamii, ambayo yamekuwa yakikosolewa na kutajwa kuwa ni kinyume cha dini ya Uislamu.

Polisi wanasema wanachunguza kuuwawa kwake lakini kufikia sasa hakuna aliyetiwa mbaroni.
 
kwanza siungi mkono kuuawa kwa huyu jamaa., ila wakati mwingine napata kigugumizi, wiki iliyopita watu wa 3 raiya wa U S waliuwawa kwa kupigwa risasi na mtu anayesemekana anachuki dhidi ya uislam.., hadi Leo hakuna aliyejitokeza kuzungumzia mauaji Yale hasa wale wanaojiita ni watetezi wa haki za binadam, vyombo vya Habari vya u s na kwengineko wamelichukulia ni tukio la kawaida tu, .kumbe akiuwawa asiyekua muislam ni ugaidi ila akiuwawa muislam ni kawaida tu!!!?.ufaransa waliuwawa watu 12 ambapo hadi sasa tukio lile linaonekana ni la kisanii tu lakin viongozi wakubwa dunian waliandamana., mbona hata tamko halitolewi kwa huyu ambaye kaua hadharani!? mbona hapasemwi ni mauwaji ya kigaidi? ...think twice.!
 
Jambazi

Its shameful how humans act like wild animals in the name of religion. What a brave soul the world has lost to those good for nothings!
 
Last edited by a moderator:
extremists think ''communication'' means agreeing with them
 
Sasa kama wanaoamini mungu wanaua wasioamini mungu kinyama hivi, kuamini mungu kuna moral value gani?
 
Kajipange upya urudi
 
bado kiranga

Hata ukimuua Kiranga, hill halibadilishi ukweli.

Litadhihirisha tu kwamba mungu unayemuamini hawezi kukupa muongozo wa maadili ya kutoua binadamu mwenzako.

Kitu ambacho hata Mimi nisiyeamini kuwepo kwa mungu nakijua.

Kam wanaoamini mungu wanaua watu, na mimi natakiwa kuangalia mifano, je kuna haja kwangu kuamini mungu?
 
Bado msimamo wangu uko pale pale, kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya Mungu anaetajwa na Waislam, na Mungu anaetajwa na Wakiristo???
 
wapi umesema huogopi ?

Kutosema siogopi ni kusema naogopa?

Wapi palipokupa wazo la kwamba naogopa mpaka ukaona haja ya kuniambia nisiogope?

Umejiridhisha vipi kwamba naogopa?
 
Kutosema siogopi ni kusema naogopa?

Wapi palipokupa wazo la kwamba naogopa mpaka ukaona haja ya kuniambia nisiogope?

Umejiridhisha vipi kwamba naogopa?

swali linapoulizwa mtu ananyamaza kimya ana maana gani ?

Najua mioyo yetu hujawa na hofu kwa hiyo unatakiwa umpe mtu matumaini

usijali akina sisi hatuui ila wale akina naniliu wanaua kishenzi usitufananishe na wale

be strong hakuui mtu
 
swali linapoulizwa mtu ananyamaza kimya ana maana gani ?

Najua mioyo yetu hujawa na hofu kwa hiyo unatakiwa umpe mtu matumaini

usijali akina sisi hatuui ila wale akina naniliu wanaua kishenzi usitufananishe na wale

be strong hakuui mtu

Hujajibu swali.

Ananyamaza kimya nani? Wapi? Umejuaje kwamba kanyamaza kimya? Kimya hicho kwa swali gani?
 
Ni kukosa utu na uadilifu tu kufikia hatua ya kuua kwa sababu ya kukinzana kiimani.Kama uchawi upo sasa hao wauaji wana tofauti gani na wachawi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…