Mwana Usalama wa Kitaa

Mwana Usalama wa Kitaa

Mkuu waliosoma Cuba hizi mambo wanazielewa wanacheza na code Tu!
Hadithi za vijiweni ambako hawajielewi hizi. Mnadhani rais anafakamia vitu hovyo hovyo bila utaratibu maalum? Kile unachoona kwenye hadhara ni sehemu ndogo sana ya mambo mengi yanayoendelea background.
 
Jioni ya Jana nikaamua niende zangu uwanjani nikacheki vijana wakifanya mazoezi,,,Kwa kawaida mi si mtu wa vijiweni kabisa kwahiyo nikiwa kitaa kama nikiamua kunyoosha miguu Sana Sana ntaenda uwanjani. Sasa hapo ndo tunaweza kutana na wadau tukabadilishana mawili matatu.

Nikiwa pale nikachukua Simu yangu na kufungua app moja ya burudani,Mimi ni mpenzi Sana WA miziki Ile ya taratibu ikiwa endapo nimejisikia kusikiliza mziki,Ile miziki ya kubembeleza na kutuliza akili/slow jam,ndo naanza kusikiliza Ngoma ya Kwanza ya Luther Vandrose inaitwa "Dance with my Father" mara paap mwamba mmoja kafika kanipa salam nami nikatoa ear phone na kumuitikia. Nikiwa katika process za kurudisha ear phone na kusikiliza Ngoma, mwamba akaanzisha story so nikasitisha zoezi la kupata vitu laini na kumsikiliza mshikaji.

Kwa namna alivyokuwa anaongea na kuchambua mambo nikajua huyu atakuwa miongoni mwa wale jamaa waliosomea Cuba Kwa Mzee Fider Castro,,,,mwamba akaniambia Ile ishu ya Mama Samia kumnywesha Raisi wa Malawi Kinywaji ujue watu wanasema ovyo Tu lakini pale ujue kuna Jambo!

Mpaka hapo ikabidi nikae vizur kumsikiliza huyu mwanausalama wa kitaa.

Na mnukuu " Ujue sikia sio kila mtu anampenda mama,kwahiyo huenda Kule Malawi watu wake Kwa maana watu wa Usalama wamemwambia huenda kuna sintofahamu Fulani so mama awe na tahadhari Sana,ndio maana Mheshimiwa akaamua kama kuna ishu kwenye hii glass basi tutapata madhara wote na akaamua kumnywesha kile Kinywaji Yule mwamba" mwisho wa kunukuu.

Nikamuuliza Mzee wa Cuba," sasa je kama Yule Mheshimiwa huko mbele ya safari ikatokea kapata matatizo si huenda Mheshimiwa anaweza kudhaniwa vibaya?" Mwamba akiwa anajiamini na majibu yake akaniambia " Unajua hapo kuna matokeo matatu ima Mama ashinde yeye au apoteze au atoe droo"

Naamini wale mlio soma Cuba kama mshikaji mtakuwa mmemulewa vizur Sana. Kiukweli sikujuta kuacha kusikiliza Ngoma laini na kumsikiliza jamaa kwani alinipa Madini Mengi Sana. Mara paap! Adhana ikasikika kuashiria Mda wa Swala umefika hivyo nikaagana na Mzee wa Cuba na kuondoka,,,Ila next time nikikutana naye tena nitawapa yatayo jiri huko coz jamaa yupo na mambo mingi Sana!

Ni hayo Tu.
Halafu pia ulitakiwa ujiulize kwanini amekuja chap kwako na kuanza kukupa hiyo habari wakati wewe humjui na inaonyesha habari yenyewe ni makini sana.
 
Hadithi za vijiweni ambako hawajielewi hizi. Mnadhani rais anafakamia vitu hovyo hovyo bila utaratibu maalum? Kile unachoona kwenye hadhara ni sehemu ndogo sana ya mambo mengi yanayoendelea background.
Sikatai kuwa kuna mambo mengi nyuma ya pazia,,,,lkn tukio la mama kumnywesha Raisi mwenzake Kinywaji nalo linafikirisha Sana ujue,,,, huenda kuna ukweli Kwa haya niliyo ambiwa na Mzee wa Cuba
 
Halafu pia ulitakiwa ujiulize kwanini amekuja chap kwako na kuanza kukupa hiyo habari wakati wewe humjui na inaonyesha habari yenyewe ni makini sana.
7seven kila kitu kinawezekana,,,huenda hiyo ishu ni kweli na jamaa friji lake haligandishi Akaona anipe nyepesi nyepesi
 
7seven kila kitu kinawezekana,,,huenda hiyo ishu ni kweli na jamaa friji lake haligandishi Akaona anipe nyepesi nyepesi
Ndio maana nikasema kwanini akupatie wewe? Wasiwasi wangu asije kukupa msala wewe ukaonekana ndiye chanzo cha taarifa halafu ukajikuta uko matatizoni mzee

Au amejua una connection na vijiwe fulani fulani so ukiitoa hii habari itasambaa haraka, ila kikifuatiliwa chanzo itaonekana taarifa imetoka kinywani mwako
 
Daah inafikirisha Sana mkuu! Kuhusu vijiwe kwakweli sina kabisa.
 
Daah inafikirisha Sana mkuu! Kuhusu vijiwe kwakweli sina kabisa.
Dawa ya hizi kitu huwa unakaa nayo kimya baada ya muda inapita. Hii dunia bwana ina mambo mengi sana kama hayajakukuta mengine utaona ni hadithi za kufikirika tu. Ila kwa ushauri wangu hizi mambo uwe unazinyamazia ,wengine wanatafutaga pa kuangushia jumba bovu.
 
Sawa mkuu ushauri wako utazingatiwa
 
Subir sasa nikuelezee hasa hasa ilikuwaje.pale mama ile juis ilikua ya embe kwa vile nakumbuka wakat tupo koz camp david Virginia Langley kwenye koz ile walikuwako marines.hayo mambo tunayajua saan kiundan
 
Back
Top Bottom