ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,534
- 21,547
Jioni ya Jana nikaamua niende zangu uwanjani nikacheki vijana wakifanya mazoezi,,,Kwa kawaida mi si mtu wa vijiweni kabisa kwahiyo nikiwa kitaa kama nikiamua kunyoosha miguu Sana Sana ntaenda uwanjani. Sasa hapo ndo tunaweza kutana na wadau tukabadilishana mawili matatu.
Nikiwa pale nikachukua Simu yangu na kufungua app moja ya burudani,Mimi ni mpenzi Sana WA miziki Ile ya taratibu ikiwa endapo nimejisikia kusikiliza mziki,Ile miziki ya kubembeleza na kutuliza akili/slow jam,ndo naanza kusikiliza Ngoma ya Kwanza ya Luther Vandrose inaitwa "Dance with my Father" mara paap mwamba mmoja kafika kanipa salam nami nikatoa ear phone na kumuitikia. Nikiwa katika process za kurudisha ear phone na kusikiliza Ngoma, mwamba akaanzisha story so nikasitisha zoezi la kupata vitu laini na kumsikiliza mshikaji.
Kwa namna alivyokuwa anaongea na kuchambua mambo nikajua huyu atakuwa miongoni mwa wale jamaa waliosomea Cuba Kwa Mzee Fider Castro,,,,mwamba akaniambia Ile ishu ya Mama Samia kumnywesha Raisi wa Malawi Kinywaji ujue watu wanasema ovyo Tu lakini pale ujue kuna Jambo!
Mpaka hapo ikabidi nikae vizur kumsikiliza huyu mwanausalama wa kitaa.
Na mnukuu " Ujue sikia sio kila mtu anampenda mama,kwahiyo huenda Kule Malawi watu wake Kwa maana watu wa Usalama wamemwambia huenda kuna sintofahamu Fulani so mama awe na tahadhari Sana,ndio maana Mheshimiwa akaamua kama kuna ishu kwenye hii glass basi tutapata madhara wote na akaamua kumnywesha kile Kinywaji Yule mwamba" mwisho wa kunukuu.
Nikamuuliza Mzee wa Cuba," sasa je kama Yule Mheshimiwa huko mbele ya safari ikatokea kapata matatizo si huenda Mheshimiwa anaweza kudhaniwa vibaya?" Mwamba akiwa anajiamini na majibu yake akaniambia " Unajua hapo kuna matokeo matatu ima Mama ashinde yeye au apoteze au atoe droo"
Naamini wale mlio soma Cuba kama mshikaji mtakuwa mmemulewa vizur Sana. Kiukweli sikujuta kuacha kusikiliza Ngoma laini na kumsikiliza jamaa kwani alinipa Madini Mengi Sana. Mara paap! Adhana ikasikika kuashiria Mda wa Swala umefika hivyo nikaagana na Mzee wa Cuba na kuondoka,,,Ila next time nikikutana naye tena nitawapa yatayo jiri huko coz jamaa yupo na mambo mingi Sana!
Ni hayo Tu.