Hi members
Maisha ya mjini yalinishinda, niliamua kurudi kijijini. Sas huko hata umeme hakuna, Computers hakuna. ndio miaka 50 ya Uhuru Tanzania. Mambo kama haya ya mtandao yapo mijini tu.
Kumbe na maisha mazuri nimegundua yapo mijini tu. KWani kijijini sasa hivi hata Sukari ni Tsh. 3,500/= Ndio miaka 50 ya Uuuru Tanzania. Mawasiliano ya Simu kule kwetu Morogoro hadi upande juu ya Mlima ndipo uongee. Ndio miaka 50 ya Uhuru Tanzania. Kilimo chenyewe nilichofikiri kitanitoa kumbe ni jembe la mkono hata matrekta hakuna na pia barabara ya kupitisha trekta hakuna. ndio miaka 50 ya uhuru Tanzania.
Nikagundua kumbe ndio maana Waluguru wengi tumehamia Mijini kufanya biashara ya kuuza bidhaa Sokoni. Kule kijijini tumewaacha Wazee tu.
maisha ni magumu sana huko. Hivyo Mimi Sirudi Kijijini!!!!!!!
MIZAMBWA
INANIUMA SANA.