Member wa JF ambaye pia huwa anapita sana kwenye jukwaa hili anayejulikana kwa jina la jerrytz amepata ajali muda si mrefu karibu na daraja la Rufiji akiwa safarini kuelekea Lindi na Mtwara. Kwa mujibu wa aliyenipa taarifa ni kwamba wamepata majeraha machache na wanashukuru wapo hai.
Chanzo ni lori kuhama upande wake na kuligonga gari walilikuwemo.
Tuwaombee wapate nafuu haraka.