Shin Lim
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 7,022
- 12,534
Mimi kuna siku nilikaa na watu wa heshima huku tukiongea mambo ya msingi tu, sasa tukiwa tunaendelea kuongea, nikajisikia kupumua.
Nikasema isiwe tabu kwa sababu nikitoka nje nitapoteza muda, wacha niachie kimya kimya. Sasa wakati naachia, nikashindwa kubalansi moto na klachi na badala yake nikakanyaga mafuta mazima na ukasikika mlio TO TO TOM hadi aliyekuwa anaongea akasimama kwanza kupisha nyuklia. Nilijaribu kuanzisha mada ya dharura lakini hakutokea mchangiaji kwa sekunde kadhaa.
Aisee nilihisi kichwa kikubwa lakini hakuna aliyecheka ingawa walibanwa na kicheko na wakaishia kukohoa tu.
Je, wewe mwanjamii forum umewahi kukutana na aibu ipi?