Criss
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 1,944
- 3,090
Yawezekana wewe ni mstaafu , uliyewahi kulitumikia Taifa kwa moyo wako wote.
Yawezekana bado upo kwenye madaraka na bado unazitii order zote nakukiombea mema chama chako kiendelee kutawala.
Yawezekana wewe ni mwanachama wa kawaida unaeshiriki kupambana kuwabagaza wapinzani kwa uwezo wako wote .
Yawezekana wewe na wale waliyoupande wapili kunakipindi mliwahi kuwa upande mmoja aidha ndani au nje ya mfumo uliyomo wewe kwa sasa .
Kwa upole kabisa nakuuliza .
Wewe mwanaccm mwenzangu kwenye hili sakata la #Polepole unefanikiwa kujifunza nini?
Yawezekana ukasema kaponzwa na kamdomo kake , siyo?
Unaamini wewe siku zote utaweza kuishi kwenye uelekeo wautakao?
Unaamini ndugu na watoto wako wataweza kuishi kwenye uelekeo wautakao?
Jiulize , ikiwa adhabu za kila atakae kengeuka iwe ni hii iliyomkuta Polepole ,wewe umejiandaaje?
Hebu fumba macho kisha jiulize ,Unautazama uelekeo wa Taifa lako kwa sura gani?
Bilashaka unaiona picture ya Taifa la mazombie ,au wewe unaonaje? Litakuwa Taifa la watu wasiyo na uwezo wakuchalange chochote , yeah ,ndiyo , maana atakaechalange atatoka wapi? Hadithi za waliyochalange zitakuwa zimejazwa vichwani mwao , majina ya kina Polepole ,Soka ,Mdude ,Mawazo ,Sativa ,Ben Saa nane na wengine wengi yatatumika kama fimbo za kuwaangamiza kiroho .
Lakini tujiulize , kwanini hatuna upendo na Taifa letu?
CCM ni chama cha siasa tukipendacho kweli kweli lakini kama kweli tunakipenda ,kwanini tusiwasihi viongozi wetu wakashiriki uwepo wa katiba ambayo haitatuelekeza kubaya ili hata tutakapostaafu bado tuendelee kuwa salama ?
Kwanini tusiwaombe viongozi wetu wakatengeneza mazingira yanayotambua haki na kumthamni kila Mtanzania bila upendeleo?
Ikiwa vyote ni upuuzi , hivi tunamjua aliye nyuma yetu?
Tumejiandaa vyakutosha kuja kuinywa dawa tunayoshiriki kuikoroga?
Muwe na wakati mwema .