Technology
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 769
- 284
Mimi nakubaliana na wewe bwana Mohamed Mtoi inawezekana hata taratibu zikapindwa wakati fulani pale ambapo kuna dharura. Inawezekana huo mkopo aliuchukua kwa ajili ya matibabu, mazishi, au dharura nyingine za kibinaadamu.
kwa hiyo hoja za msingi ni:
1) Lengo la huo mkopo ni lipi kwa sababu chama hakiwezi kutoa mkopo kwa ajili ya kwenda kuoa!
2) Qualification criteria za hiyo mikopo ni ipi ili na wanachama wengine waende kukopa
3) Kukopa kama utaratibu umefuatwa sio ufisadi lakini ukiukwaji wa taratibu katika mambo ya fedha kama haya ndio hupelekea ufisadi kutokea.
Mkuu Ritz for sure ulikuwa na close coordination na post ukahakikisha unakuwa wa kwanza kurusha post!!! Ha ha ha!! Dr, Slaa atawalaza macho na mwisho wa siku ni mshindi tu mtu wangu!! Mnapiga kila upande but watanzania tumemshikilia kwa kuwa tunafahamu mchezo wenu mchafu!! Mwenzako Nape anachanwa live humu kumbe ni HARAMU na baba mwenyewe ni wa kubandikiwa na familia imeshamkataa!!! Khaa!! SSM viongozi wenu bwana!! Mara mafisadi, mara majambazi wa nyara za serikali na vitalu vyake haramu. By the way, mwenzake mmoja kakamatwa huko Manyara na gari ya JW!! Kumbe wizi wa nyara umeanzia mbali kabisa!! Halafu eti mnamfanya kiongozi!! Na mpiga vuvuzela ni haramu!! Na mfalme wao dhaifu!! Hamuiwezi CDM!! Hata mkitaka kuipasua vipande mara moja intelligenzia inawafichua!! Wapokeeni sasa kina Shonza na huyu mlilia hapa na vimilion 20 mbona mafisadi wenu ni mabilioni tu na hamuwasemi!!! SSM nyie mna auditing kweli!!! Hakuna maana pesa yenu yote ni emergence kwa kununua wapiga kura tu!!! Ha ha!! Long live CDM!!! Sina Chama ila ni mpiga kura safi wa kiongozi safi bila kufungamana na the so called Chama!!
Tatizo siyo kumsikiliza Mwampamba tatizo kwa nini Dr Slaa akope pesa za ruzuku katibu ya Chadema inasemaje.
Endelea kuwadharau vijana wa vijiweni lakini kumbuka hao ndiyo wapiga kura.
Mtela kama una hoja jaribu kuwa na staha, huwezi kutukana kiasi hicho kwa mtu anaye kuzidi umri alafu ukaachwa tu uendelee dogo nakwambia hivi utapata laana ambayo hukuitegemea, nimeamini ya kuwa kweli ulipogombea umbunge mbozi mashariki na vijana wengi wakakuunga mkono , hukuwa na nia hiyo ila ulikuwa na malengo fulani ( Hasa ya kutumika)
Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.
Ni busara kwa independent parties kutolea maelezo juu ya huu mkopo wa DR Slaa. Inawezekana alitumia undue influence kuupata. Ni muhimu ili kujua ukweli wake katika mapambano dhidi ya ufisadi. 'Ni rahisi kujisifu kuwa unasimamia maadili lakiniikawa vigumu kuyatekeleza kivitendo'Mkuu.
Naomba urudi usome tena hoja zangu kwa makini ukiwa umetulia na akili ikiwa sober. Hasa ile nukta ya kwanza.
1. Mwampamba mwenyewe hakusema mkopo ulikuwa wa nini wewe umetaja "kuolea" hapa umepoteza sifa ya GT maana umeamua kufanya kazi ya utabiri. (Sina hakika kama sheikh Yahya kakuachia mikoba)
Tambua kuwa anaeweza kujua faida ya mkopo ni mkopaji mwenyewe kutegemeana na malengo yake binafsi kwenye huo mkopo. Inshu hapa sio kaufanyia nini (malengo), swala la msingi, je kalipa?!
2. Qualification/criteria za mkopo huwa baina ya mkopaji na mkopeshwaji na mara nyingi huwa haziko static bali hutegemeana na makubaliano na vigezo kati ya part 1 and part 2. Kwa kuwa nilisha sema kuwa katiba za vyama vingi hazina kanuni au sheria za kukopesha/kukopeshana qualification/criteria zitakuwa kati yako na chama kwa maana ya makubaliano kati yenu maana kuto kuwa na kanuni/sheria haihalalishi kuto kukopesheka.
3. Kufuata taratibu maana yake ni nini?! Ni kuomba mkopo mkakubaliana terms and conditions za kulipa kisha ukalipa?! Kama kwenye katiba ya chama hakuna sheria/kanuni za kukopa/kukopeshana na bado kukawa na uhalali wa kukopa/kukopeshana maana hakuna sheria inayo kataza, then mkikubaliana kukopeshana kwa terms and condition mtakazo wekeana na mkazifuata hadi kulipana itakuwa ni ukame wa maono kuhoji taratibu.