Victor RM
New Member
- May 1, 2017
- 3
- 3
Mwambieni Lau Masha sisi Chadema hatukuwahi kuunga mkono wala kuhubiri utekaji watu( Ben-Rabiu Wa Saanane ),uuwaji(coco beach,mto ruvu kule bagamoyo)/upigaji watu risasi mchana kweupe na watendaji wa haya kutopatikana hadi leo na hutujui wapi na nini kimefanyika kuhusu hawa ndugu zetu na wala hatukuwahi kusema kuwa tutaenenda kinyume na katiba ya Taifa hili
Nendeni mkamwambie Lau Masha kuwa Chadema hatukuwahi hata siku moja kukaa majukwaani na kuwaambia waTanzania kuwa tutakuwa na double standard katika taifa hili na kuona baadhi ya watanzania wenzetu wanafaa kufukuza kazi tena kwa kudhalilishwa na wengine hata wasio na vyeti na majina sio yao tukasema tutawalinda
Tena mumkumbushe kabla hajafika Chadema na baada ya kuja na sasa ameondoka kamwe hatukuwahi kusema kuwa tutatumia fedha za walipa kodi kufanya matumizi pasipo kuidhinishwa na bunge ambalo lipo kuwawakilisha wananchi,
Kamwe hatukuwahi kusema popote kuwa tutakopa kwa wahisani pasipo bunge na watanzania kufahamu na kujua hizo fedha zimekopwa kwa matumizi gani katika Taifa letu
Mwambieni sisi tunaihubiri demokrasia ya kweli tena yenye tija na manufaa kwa kila mtanzania akiwamo yeye mwenyewe.
Namkumbusha Lau hatukuwahi kusema popote kuwa tutazuia uhuru wa habari na kujieleza(Freedom of speech) popote katika Chadema labda kama ni maono yake ya mika hamsini ijayo japo sijaona viongozi wa namna hii katika Chadema hata kwa miaka mia ijayo
Hatukuwahi kusema kuwa kama kiongozi wetu akiwa kiongozi atakataa kukosolewa ili afungie na kufuta baadhi ya magazeti yanayomkosoa
Tena akumbushwe kuwa katika uwepo wake kabla na baada hakuna sehemu yoyote tuliwahi kusema tutazuia mikutano ya vyama vya siasa kama ilivyo sasa mwambieni na mumkumbushe yote hata yale mengi aliyoaaandika katika barua yake
Yeye aondoke tu kama alivyokuja hatukumuita na asidhani kama tumemfukuza ni dhamira yake na asitudanganye kwa masuala ya kitoto namna hiyo labda wajinga tu ndio wanaoweza kumuelewa
Na maovu mengine mengi kama kuzuia bunge live,upatikanaji wa katiba mpya,wafanya kazi kutoboreshewa maslahi yao na kupandishwa madaraja na kuwafanya matajiri kuwa masikini pia hatuwahi kuwaambia watanzania haya
Tanzania Kwanza