Masha Mshomba, Mkurugenzi NSSF: Mfuko kwa mwaka 2023 umekuwa juu ya asilimia 20

Apr 9, 2022
66
32
Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF), Masha Mshomba ametoa ufafanuzi wa mwenendo wa ukuaji wa Mfuko katika kipindi cha miaka mitatu ya hivi karibuni kwamba wastani wa ukuaji wa Mfuko kwa mwaka umekuwa juu ya asilimia 20.

IMG-20230925-WA0534.jpg

Ameeleza hayo katika Mkutano wa kikao kazi na Wahariri wa Vyombo vya Habari, Mshomba ametoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kilichoanzia Machi, 2021 hadi Juni 2023.

Eidha amefafanua kuwa, Mwenendo mzuri wa ukuaji wa Mfuko ambao unathibitisha kuwa NSSF ipo imara na endelevu kwa ajili ya utoaji wa huduma za Hifadhi ya Jamii nchini.

"Makisio (projections) ya miaka 75 ijayo yaliyofanywa kupitia tathmini ya mwisho ya uhai na uendelevu wa Mfuko (actuarial valuation) iliyofanyika katika mwaka wa fedha 2020/21, yalibaini kuwa NSSF haina matatizo ya ukwasi ambao ungetilia shaka uendelevu wake na hatma ya wanachama wake" amesema Mshomba.

Ameendelea kwa kusema tathmini nyingine ya uhai na uendelevu wa Mfuko inatarajiwa kufanyika katika nusu ya pili ya mwaka huu wa fedha kwa kutumia taarifa za utendaji kwa kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni 2023.
 
Back
Top Bottom