Ogopa kilichomuua Samsoni

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Ikiwa mtaonana na Haji Manara mwambieni kuwa "asinene akamara" wahenga ndio walivyosema. Ikishatukuka shajara, hufaa kwa wakati lakini yakibadilika masaa huonekana ya kifala.

Ulimi huponza vingi, mkumbusheni atunze maneno na aweke akiba. Mwisho mwambieni asithubutu kumuamini mwanamke asilimia mia.

Hadithi nyingi za mapenzi huwa haziishi bila tone la huzuni na michirizi ya damu za majuto. Walioaminiwa husahau yote ya awali na kuvunja imani walizopewa. Mwisho wa siku akina Delila huwa ni wengi sababu wakimaliza kile walichokifuata, huondoka na kumuacha Samsoni akibwata.

Ni kweli hata mimi nakubali, katika kizazi cha sasa ni ngumu sana kumpata mwanamke bila fedha. Yaani wanawake watakutaka ikiwa tu una kitu wanachokitaka, ndio, ndoano tupu hainasi samaki hata kwa bahati mbaya.

Lakini iweje tuamini watu ambao hata sisi wenyewe tunajua kuwa wametufuata sababu ya kitu fulani ?? Kwanini tuwape uaminifu watu ambao tumeungana nao sababu ya kitu fulani ??

Kama ambavyo muamvuli huwa mzigo mara tu baada ya mvua kuisha kunyesha, basi vivyo hivyo hata watu watakuona mzigo baada ya kile walichokifuata kutoka kwako kikiisha/wakikizoea. Ndio, sababu utakuwa huna jipya tena mbele yao.

Hakuna maskini anaeaminiwa hasa ikiwa jambo linalohusu fedha likihusishwa. Binadamu watakutilia maanani ikiwa tu una kitu wanachokitilia maanani.

Ukiwa na fedha, unaweza ukammiliki mbwa yeyote mwenye njaa ila shida ni kwamba akitokea mwingine mwenye fedha zaidi yako basi anaweza akammliki mbwa huyo huyo, na huyo mbwa anaweza akatumika pia kukung'ata bila kukumbuka mema yako ya awali.

Aaaanh! Ama kweli "nyuma ya kila mwanamke unaetamani kuwa nae kwenye mahusiano basi kuna mwanaume aliechoka kumtumia"

Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Hakuna upepo unaovuma milele. Mkumbusheni kaka Manara maneno anayomtakia dada Zai aliwahi kuyatamka kwa Hamida na Rushayna na bado hadithi ya mapenzi yake ikaishia kuwa na doa.

Mwambieni ajikumbuke yeye, yeye yule wa miaka miwili nyuma. Upya na uzuri ni hadithi za mpito hata dada Rushayna alimuona mzuri na alimtungia mashairi mengi ya mahaba na chombwezo la huba kama haya anayoyatunga hivi sasa.

Aweke maneno ya akiba, kesho nayo ni siku asinene akamara . Hawezi kumridhisha mwanamke anaetumia asali na sukari kwenye chai Moja.

Muambieni asipokuwa makini, wembe uliomnyoa Adamu, ukamnyoa Samsoni, ukamnyoa Harmonize ndio huo huo utakuja kumnyoa yeye.

Bob Marley alisikika akisema "Fear Women"

Mwisho kwenu wanaume wenzangu, hatutakiwi kumuogopa Simba sababu Simba aliuwawa na Samsoni, tunakiwa kuogopa kile kilichomuua Samsoni.

Mwenye sikio na asikie

Muandishi ni yule Mtoto wa fundi mota, Amani Dimile

#amanidimile #misemoyahekima #mtotowafundimota #tungomaridadi #fikrazadimile
Screenshot_20240121-124902.jpg
 
Ujinga tu kumuoa social lite labda km nawe ni mjinga,ni sawa mpiga Bomu muchwari halafu ukajisifu kuwa ni komando!

Pathetic!
 
Back
Top Bottom