Mwalimu (wa primary) aliingia darasani;mara baada ya salamu,akawapa wanafunzi wake zoezi, na kuwaambia; "kila mmoja achukue kalamu na karatasi na amchore Tembo", kila mwanafunzi alitingwa na zoezi hilo. Baada ya kumaliza, akaanza kupitia dawati moja baada ya lingine;kwa tahayari,akamkuta mwanafunzi mmoja kwenye karatasi yake kachora nukta. Mwalimu kwa hasira akamuuliza mwanafunzi, "wewe, mbona hujamchora tembo?", mwanafunzi kwa kujiamini akamjibu mwalimu, " aaah, mi nimemchora tembo akiwa kwa mbaaaaaaali"...............