Ndugu wana jamvi,
Mimi kama mzazi mwenye mtoto anayesoma Shule ya Sekondari ya wasichana Kibosho, nina wasiwasi sana na ufaulu wa watoto kwa somo la hesabu kidato cha nne mwaka huu 2014. Matokeo ya watoto waliopo kidato cha nne mwaka huu yamekuwa hayaridhishi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na pre mock ya mwaka huu watoto wamepata hadi asilimia 12%!
Mkuu wa shule haonyeshi kustushwa na matokeo haya lakini nina wasiwasi kwa mara ya kwanza shule ya wasichana ya Kibosho itatoa division 4 na 0 wengi kwa sababu ya somo la hesabu kuwa tatizo. Mkuu wa shule malengo yake ni kufuta division 3 ili ibaki 1 na 2. Hilo litawezekanaje wakati watoto walipata hadi asilimia 6%? kwa somo la hesabu kwa mtihani wa mwisho wa mwaka 2013?
Kwa utamaduni wa Kibosho, mwalimu wa hesabu huanza na watoto kidato cha kwanza na kwenda nao hadi kidato cha nne. Kulingana na matokeo ambayo tumeyashuhudia tangu mwaka jana (2013), mwalimu huyu wa hesabu anawapeleka watoto korongoni. Angalia matokeo haya ya mwaka jana (form 3) ambao sasa wapo kidato cha nne:A=0, B=8, C=24, D=36 na F=83. Haya matokeo ni mabaya mno kwa shule kama Kibosho. Hapa huwezi kusema watoto hawa wote ni wajinga kuliko mwalimu wao. Mwalimu ana tatizo. Mtoto anapata 6 au 12 hesabu wakati masomo mengine anapata A. Huyu mtoto huwezi kusema kwamba hana uwezo. Inawezekana anakatishwa tamaa na ufundishaji,
Japo kuwa muda umekwenda, kwa hawa waliopo kidato cha nne wakijiandaa na mitihani yao ya mwisho, naamini nafasi bado ipo ya hali hii kuangaliwa kwa makini angalau kunusuru aibu hii inayoenda kuonekana. Mwaka jana kwenye kikao cha wazazi Msimbazi Centre wazazi waliliongelea hili kwa uchungu lakini bado linanendelea kuonekana.
Kwakuwa hili suala ni la muhimu sana mjadala uendelee na uwafikie viongozi mbalimbali kama mwenyekiti wa bodi ya shule ili naye ahoji hili kwa undani zaidi na kumbana Mkuu wa shule. Naomba tuache mambo ya kejeli na mzaha kwenye hili suala.